GIROUD ATAFAKARI KUNG'OKA ARSENAL KWA KUSAGA BENCHI!

GIROUDBAADA kuanzia Benchi mara 23 na baadae kuingizwa kucheza Msimu uliokwisha Mei, Straika wa France Olivier Giroud sasa anatafakari kuondoka Arsenal.

Giroud, mwenye Miaka 30, alianza Mechi 11 tu Msimu uliopita licha kufunga Bao 12 na kujikuta mara nyingi akipigwa Benchi huku Meneja Arsene Wenger akimpanga Alexis Sanchez na pia Danny Welbeck.

Sasa Giroud, ambae ndie aliesuka Bao la ushindi alilofunga Aaron Ramsey na kuwabebesha FA CUP Wiki 2 zilizopita, anahisi sasa ni wakati sahihi kuangalia hatima yake.

Ameeleza: "Nitaongea na Wenger. Sikupata nafasi nyingi kucheza lakini utafika wakati kuna vitu sitakubali na hasa Mwaka mwingine wa kucheza Mechi chache."

Giroud pia ameeleza atakaa chini na Familia yake na Washauri wake kutafakari maamuzi yoyote yale.

Hata hivyo, Straika huyo amedokeza kuwa bado ana Miaka Mitatu ya Mkataba na Arsenal na angependa zaidi kutwaa Ubingwa wa England na Klabu hiyo.

Habari MotoMotoZ