UCL: PSG YAIFUMUA BARCA, BENFICA YAITUNGUA DORTMUND!

UEFA CHAMPIONZ LIGI

Raundi ya Mtoano ya Timu 16
Ratiba/Matokeo:
Mechi za Kwanza
Jumanne 14 Februari 2017
Benfica 1 Borussia Dortmund 0      
Paris Saint Germain 4 Barcelona 0          
Jumatano 15 Februari 2017
Bayern Munich v Arsenal                 
Real Madrid v Napoli              
+++++++++++++++++++++++++
UCL-16-17-SITJana huko Parc des Princes Jijini Paris Nchini France Mabingwa wa huko Paris St Germain waliifumua Barcelona 4-0 katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Kwenye Mechi nyingine ya Raundi hiyo Benfica iliichapa Borussian Dortmund 1-0.
Katika Mechi ya PSG na Barca, Bao za PSG zilipigwa na Angel Di Maria, Dakika za 18 na 55, Julian Draxler, 40', na Edinson Cavani, 71'.
PSG walitawala Mechi hii na Barca kupooza mno huku Mastaa wao Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar 'wakijificha'. 
Kipigo hiki kinaiweka Barca pagumu kufuzu kwenda Robo Fainali na wakishindwa hilo hii itakuwa mara ya kwanza kwao kutotinga Robo Fainali katika Miaka 10.
==========
JE WAJUA?
-Katika Historia ya UCL haijawahi kutokea Timu iliyopigwa 4-0 katika Mechi ya Kwanza na kupindua kipigo hicho katika Mechi ya Pili na kutinga Robo Fainali.
========== 
Huko Lisbon, Ureno, Benfica ilifunga Bao katika Dakika ya 48 kupitia Kostas Mitroglou na kuibwaga Borissia Dortmund 1-0.
Dortmund  walikosa Penati baada ya Pierre-Emerick Aubameyang kupiga na Kipa Ederson kuukoa.
UEFA CHAMPIONZ LIGI
Raundi ya Mtoano ya Timu 16
**Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku Saa za Bongo
Mechi za Kwanza
Jumanne 21 Februari 2017
Bayer 04 Leverkusen v Atlético Madrid              
Manchester City v Monaco               
Jumatano 22 Februari 2017
FC Porto v Juventus               
Sevilla v Leicester City           
Mechi za Pili
Jumanne 7 Machi 2017
Arsenal v Bayern Munich                 
Napoli v Real Madrid              
Jumatano 8 Machi 2017
Barcelona v Paris Saint Germain              
Borussia Dortmund v Benfica          
Jumanne 14 Machi 2017
Juventus v FC Porto               
Leicester City v Sevilla           
Jumatano 15 Machi 2017 
Atlético Madrid v Bayer 04 Leverkusen              
Monaco v Manchester City              
++++++++++++++++++++++++++++
TAREHE MUHIMU:
MECHI ZA MTOANO: 
14/15 na 21/22 Feb 2017: Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Mechi ya Kwanza
 7/8 na 14/15 Machi 2017: Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Mechi ya Pili
 11–12/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Kwanza
 18–19/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Pili
 02–03/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Kwanza
 09–10/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Pili
03/06/17: Fainali (National Stadium of Wales, Cardiff)