EPL: MKONO, TUTA, USHINDI KWA ARSENAL!

EPL – Ligi Kuu England

Ratiba/Matokeo:

Jumamosi Februari 11

Arsenal 2 Hull City 0         

1800 Manchester United v Watford                 

1800 Middlesbrough v Everton    

1800 Stoke City v Crystal Palace           

1800 Sunderland v Southampton

1800 West Ham United v West Bromwich Albion                 

2030 Liverpool v Tottenham Hotspur     

+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

ARSENAL-SANCHEZ-MKONOAlexis Sanchez Leo amefunga Bao 2, moja kwa Mkono na jingine kwa Penati, na kuipa Arsenal ushindi wa 2-0 walipocheza kwao Emirates na Hull City katika Mechi ya kwanza kabisa hii Leo ya EPL Ligi Kuu England.

Arsenal walifunga Bao la Kwanza Dakika ya 34 baada ya Mpira kumgonga Mkononi na kutinga kufuatia kizaazaa cha Krosi Kieron Gibbs.

Bao la Pili la Arsenal lilifungwa tena na Sanchez katika Dakika za Majeruhi, Dakika ya 92, kwa Penati iliyotolewa baada ya Sam Clucas kuushika Mpira wa Kichwa wa Lucas Perez kwenye Mstari wa Goli.

Refa Mark Clattenburg aliwapa Penati Arsenal na kumpa Kadi Nyekundu Sam Clucas na Sanchez kufunga Penati hiyo.

Ushindi huu umewaweka Arsenal Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 50 sawa na Tottenham ambao wako Nafasi ya Pili lakini wanacheza baadae Leo huko Anfield na Liverpool.

VIKOSI:

ARSENAL: Cech, Bellerin, Mustafi, Koscielny, Gibbs, Oxlade-Chamberlain, Coquelin, Walcott, Ozil, Iwobi, Sanchez.

Akiba: Gabriel, Lucas Perez, Giroud, Ospina, Monreal, Welbeck, Elneny.

Hull City: Jakupovic, Elabdellaoui, Ranocchia, Maguire, Robertson, Huddlestone, N’Diaye, Markovic, Grosicki, Clucas, Niasse.

Akiba: Meyler, Maloney, Diomande, Marshall, Elmohamady, Tymon, Evandro.

REFA: Mark Clattenburg

EPL – Ligi Kuu England

Ratiba

Jumapili Februari 12

1600 Burnley v Chelsea    

1900 Swansea City v Leicester City                 

Jumatatu Februari 13

2300 Bournemouth v Manchester City   

Jumamosi Februari 25

1800 Chelsea v Swansea City               

1800 Crystal Palace v Middlesbrough              

1800 Everton v Sunderland         

1800 Hull City v Burnley             

Southampton v Arsenal [IMEAHIRISHWA]

1800 West Bromwich Albion v Bournemouth              

2030 Watford v West Ham United         

Jumapili Februari 26

1630 Tottenham Hotspur v Stoke City             

Manchester City v Manchester United [IMEAHIRISHWA]

Jumatatu Februari 27

2300 Leicester City v Liverpool             

Jumamosi Machi 4

1530 Manchester United v Bournemouth         

1800 Leicester City v Hull City              

1800 Stoke City v Middlesbrough          

1800 Swansea City v Burnley                

1800 Watford v Southampton               

1800 West Bromwich Albion v Crystal Palace             

2030 Liverpool v Arsenal            

Jumapili Machi 5

1630 Tottenham Hotspur v Everton       

1900 Sunderland v Manchester City      

Jumatatu Machi 6

2300 West Ham United v Chelsea