MAN UNITED Vs WATFORD: MAN UNITED KUNG’OKA NAFASI YA 6?

>PATA RIPOTI/VIKOSI!

EPL – Ligi Kuu England

Ratiba

Jumamosi Februari 11

1530 Arsenal v Hull City             

1800 Manchester United v Watford                 

1800 Middlesbrough v Everton    

1800 Stoke City v Crystal Palace           

1800 Sunderland v Southampton

1800 West Ham United v West Bromwich Albion                 

2030 Liverpool v Tottenham Hotspur     

+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

MANUNITED-WATFORDMANCHESTER UNITED Jumamosi wako kwao Old Trafford Jijini Manchester kucheza Mechi ya EPL, Ligi Kuu England, na Watford ambayo Mwezi Septemba ilishinda 3-1 huko Vicarage Road.VIKOSI-MANUNITED-WATFORD

Lakini wakati huo Man United ilikuwa ikiyumba tofauti na sasa ambapo wapo kwenye wimbi la kutofungwa kati Mechi 15 za Ligi, wakishinda 8 na Sare 7, na hiyo ni Rekodi ambayo haina mfano kwenye Ligi kubwa 5 Barani Ulaya.

Mbali ya kusaka kisasi, Man United pia wanahitaji ushindi ili watoke Nafasi ya 6 walioshikilia kwa muda mrefu na kupanda hadi Nafasi ya 5 juu ya Liverpool na pengine kufika hadi Nafasi ya 4 ikiwa Arsenal atafungwa na Hull City katika Mechi yao ya mapema.

Mechi hii pia ni ya mwisho ya EPL kwa Man United kwa Mwezi huu kwani Mechi yao inayofuata ni hapo Machi 4 wakati Bournemouth watakapotua Old Trafford.

Baada Mechi hii na Watford, Man United watakabiliwa na Mechi 4 mfululizo za Makombe Matatu tofauti kwa kucheza na Saint-Etienne ya France Uwanjani Old Trafford kwenye Raundi ya Mtoano ya EPL-FEB5Timu 32 ya UEFA EUROPA LIGI hapo Februari 16, kisha Februari 19 kucheza Raundi ya 5 ya FA CUP huko Ewood Park na Blackburn Rovers na kufuata Februari 23 Marudiano na Saint-Etienne huko France na kumaliza Februari 26 Uwanjani Wembley Jijini London kwenye Fainali ya EFL CUP dhidi ya Southampton.

Man United, ambao kwenye Mechi yao ya mwisho waliichapa Leicester City 3-0, watatinga wakiwa hawana wasiwasi kuhusu hali ya Wachezaji wao huku wote wakiripotiwa ni fiti,

Watford, chini ya Meneja Walter Mazzarri, wanapaswa kucheki ufiti wa Miguel Britos na Valon Behrami huku wakiwakosa Majeruhi Nordin Amrabat, Camilo Zuniga, Costel Pantilimon na Christian Kabasele.

Safari hii Watfoord wana Wachezaji Wapya Wawili, Tom Cleverley, aliewahi kuichezea Man United na sasa yuko hapo kwa Mkopo toka Everton tangia Januari, na pia Straika wa Mkopo kutoka AC Milan M'Baye Niang.

EPL – Ligi Kuu England

Ratiba

Jumapili Februari 12

1600 Burnley v Chelsea    

1900 Swansea City v Leicester City                 

Jumatatu Februari 13

2300 Bournemouth v Manchester City