CHELSEA: NJIA UBWETE KUTWAA UBINGWA!

CHELSEA-COSTA-SITBAADA ya Chelsea kuwatwanga Arsenal 3-1 njia sasa ni nyeupe kwa Vinara hao wa EPL, Ligi Kuu England, ya kutwaa Ubingwa kwani Mechi zao 6 zijazo ni za nafuu ukilinganisha na Wapinzani wao wengine kwenye mbio za Ubingwa.

Chelsea, ambao wanaongoza EPL wakiwa Pointi 9 mbele ya Timu ya Pili Tottenham, Aprili 5 watacheza na Man City huko Stamford Bridge lakini kabla ya hapo wana Mechi 6 zenye Wapinzani ‘laini’.

Mechi zijazo kwa Chelsea ni Jumapili ijayo Ugenini kwa Burnley, kisha watacheza na Swansea Nyumbani), West Ham Ugenini), Watford (Nyumbani), Stoke (Ugenini) na Crystal Palace (Nyumbani).

Mapema Msimu huu, Chelsea walishinda Mechi 5 kati ya hizo 6 wakitoka Sare 2-2 Ugenini na Swansea.

++++++++++++++++++++++

Chelsea – Matokeo na hizo Timu 6:

-Ushindi 3-0 v Burnley

-Dare 2-2 v Swansea

-Ushindi 2-1 v West Ham

-Ushindi 2-1 v Watford

-Ushindi 4-2 v Stoke

-Ushindi 1-0 v Palace

++++++++++++++++++++++

Tofauti na Chelsea, zile Timu ambazo zipo 6 Bora zina Ratiba ngumu katika Mechi zao 6 zijazo.

Katika kipindi hicho, Tottenham wataenda Anfield kucheza na Liverpool na kisha kuwa Wenyeji wa Everton na Southampton.

Wakati huo huo, Arsenal watacheza Ugenini na Southampton na Liverpool kisha Nyumbani na Man City.

Liverpool watacheza na Tottenham, Arsenal, Man City na pia Dabi ya Merseyside dhidi ya Wapinzani wao wa Jadi Everton.

Nao Man City wataivaa Man United na Liverpool huko Etihad na kwenda Ugenini kucheza na Arsenal.

Mechi 6 zijazo za Man United kidogo zina ahueni nap engine ngumu kwao ni zile za Ugenini dhidi ya Man City na Southampton.

Wakati Chelsea wamebakisha Mechi 2 tu dhidi ya Timu ambazo zipo 6 Bora, ambazo ni dhidi ya Man City na Man United, Arsenal, Man City na Man United zimebakisha Mechi 4 dhidi ya Wapinzani toka Kundi hilo, wakati Liverpool na Tottenham zimebakisha 2 tu dhidi ya Timu za Kundi hilo.

Kama Chelsea watafanya vizuri katika Mechi zao 6 zijazo basi ni wazi hawakamatiki na Ubingwa Msimu huu upo Stamford Bridge.

EPL – Ligi Kuu England

Ratiba

Jumamosi Februari 11

1530 Arsenal v Hull City             

1800 Manchester United v Watford                 

1800 Middlesbrough v Everton    

1800 Stoke City v Crystal Palace           

1800 Sunderland v Southampton

1800 West Ham United v West Bromwich Albion                 

2030 Liverpool v Tottenham Hotspur               

Jumapili Februari 12

1600 Burnley v Chelsea    

1900 Swansea City v Leicester City                 

Jumatatu Februari 13

2300 Bournemouth v Manchester City