EPL: LEO MAN UNITED WAPO KING POWER STADIUM KWA MABINGWA LEICESTER!

EPL – Ligi Kuu England

Ratiba

**Saa za Bongo

Jumapili Februari 5

1630 Manchester City v Swansea City             

1900 Leicester City v Manchester United          

++++++++++++++++++++++++++

MANUNITED-MOU-MAJILEO zipo Mechi 2 za EPL, Ligi Kuu England, na mojawapo ni huko King Power Stadium kati ya Mabingwa Watetezi Leicester City na Manchester United.

Wakati Man United wakiwa kwenye wimbi la kutofungwa katika Mechi 14 na wapo Nafasi ya 6 kwenye EPL, Leicester wao wanasuasua na wapo Nafasi ya 16.

Mapema Msimu huu, katika Mechi yao ya kwanza huko Old Trafford, Man United iliichapa Leicester 4-1.

Hali za Timu

Mchezaji pekee ambae Man United watamkosa kwa Mechi hii ni Beki Phil Jones alieumia kwenye Mechi yao iliyopita na Hull City.

Leicester City wanaweza kuwa nae Fowadi wa Algeria Islam Slimani ambae amerejea kutoka Gabon alipokuwa akicheza AFCON 2017 na pia Mchezaji wao mpya wa Mkopo kutoka Udinese ya Italy, Molla Wague, huenda akaanza Mechi hii.

Fomu za Timu

Wakati Man United wakitoka kwenye Sare ya 0-0 na Hull City, Leicester wao walifungwa 1-0 na Burnley.

VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:

LEICESTER CITY: Schmeichel, Simpson, Morgan, Huth, Fuchs, Mahrez, Ndidi, Drinkwater, Albrighton, Okazaki, Vardy

MAN UNITED: De Gea, Valencia, Smalling, Rojo, Darmian, Carrick, Herrera, Mkhitaryan, Pogba, Martial, Ibrahimovic

REFA: Anthony Taylor