EMIRATES FA CUP – DROO RAUNDI YA 4: MABINGWA MAN UNITED OLD TRAFFORD NA WIGAN!

EMIRATES-FACUP-2017DROO YA RAUNDI YA 4 ya EMIRATES FA CUP imefanyika Leo Usiku huko BT Tower Mjini London ikiendeshwa na Wachezaji wa zamani wa Kimataifa wa England Michael Owen na Martin Keown na Mabingwa Watetezi Manchester United kupangwa kucheza kwao Old Trafford na Wigan Athletics.

Man City na Arsenal zote zimepangwa kucheza Ugenini kwa Arsenal kuivaa Southampton au Norwich na Man City kucheza na Mshindi kati ya Crystal Palace na Bolton.

Liverpool, kama wataifunga Plymouth katika Mechi yao ya Marudiano baada ya Sare, watakuwa kwao Anfield kucheza na Wolves.

Vinara wa Ligi Kuu England, Chelsea, wao wako kwao Stamford Bridge kuivaa Brentford.

Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu England, Leicester City, watacheza Ugenini na Derby County wakati Tottenham wakicheza Nyumbani White Hart Lane na Wycombe.

++++++++++++++++++++

JE WAJUA?

-FA CUP 2016/17, ambalo pia hujulikana kama FA Challenge Cup, ni mara ya 136 kushindaniwa kila Mwaka tangu lilipoanzishwe na linatambuliwa kama ndio Mashindano ya kale kupita yote Duniani.

-Kombe hili linadhaminiwa na Kampuni ya Ndege8k ya Emirates na kwa sababu za kiudhamini linaitwa Emirates FA Cup.

-Timu 736 zilikubaliwa kushiriki Mashindano haya Msimu huu na yalianza kwa Raundi ya Awali na yatafikia Tamati kwa Fainali itakayochezwa Uwanjani Wembley Jijini London hapo Mei 27, 2017.

-Mshindi wa FA CUP ataingizwa Hatua ya Makundi ya UEFA EUROPA LIGI Msimu wa 2017/18.

-Bingwa Mtetezi ni Manchester United.

+++++++++++++++++++

Mechi 16 za Raundi ya 4 zitachezwa Wikiendi ya Januari 28 na 29.

DROO KAMILI:

Crystal Palace au Bolton v Manchester City

Middlesbrough v Accrington Stanley

Fulham v Hull City

Blackburn v Barnsley au Blackpool

Burnley au Sunderland v Fleetwood au Bristol City

Rochdale v Huddersfield Town

Millwall v Watford

Manchester United v Wigan Athletic

Chelsea v Brentford

Lincoln au Ipswich v Brighton

Southampton au Norwich v Arsenal

Plymouth au Liverpool v Wolves

AFC Wimbledon au Sutton v Cambridge au Leeds

Oxford United v Newcastle au Birmingham

Derby County v Leicester City

Tottenham v Wycombe