PEP NJIA PANDA, SAGNA MASHAKANI, KULIKWAA RUNGU LA FA?

WAKATI Meneja wa Manchester City Pep Guardiola akikiri kuwa huu ni mwanzo wa mwisho kwa yeye kuwa Meneja, Mchezaji wa Timu hiyo Bacary Sagna ametakiwa na FA, Chama cha Soka England, kujieleza kuhusu Posti yake kwenye Instagram kuhusu Refa Lee Mason.

PEP GUARDIOLA – MWANZO WA MWISHO

PEPPep Guardiola amedokeza kuwa sasa ni mwanzo wa mwisho wake kwenye kazi ya Ukocha.

Bosi huyo wa zamani wa Barcelona na Bayern Munich sasa ametimiza Miezi 6 tu kwenye himaya yake na Man City ambako amekuwa na mafanikio mchanganyiko.

Hivi karibuni Guardiola alisema hawezi kumuiga Bosi wa Arsenal Arsene Wenger na kukaa Miaka 20 kazini.

Guardiola, mwenye Miaka 45, ameeleza: “Nitakuwa City kwa Misimu Mitatu, pengine zaidi, lakini nakaribia kufika mwisho wa Maisha yangu kama Kocha, hilo nina hakika!”

SAGNA – ATAKIWA KUJIELEZA NA FA KUHUSU POSTI YA INSTAGRAM KUHUSU REFA LEE MASON!

Bacary Sagna ametakiwa kujieleza na FA kuhusu Posti yake Mtandaoni Instagram alipohoji umakini wa Refa Lee Mason.

Kwenye Instagram, Sagna, Beki wa Man City, aliandika: “10 dhidi ya 12…lakini tulipigana na tulishinda kama Timu!”

Posti hiyo ilitoka mara baada ya City kuiofunga Burnley 2-1 huko Etihad Stadium kwenye Mechi ambayo City walibaki Mtu 10 kuanzia Dakika ya 32 kufuatia Kiungo wao Fernandinho kutolewa kwa Kadi Nyekundu na Refa Lee Mason kufuatia Rafu mbaya.

Fernandinho ametakiwa kutoa maelezo juu ya Posti yake si zaidi ya Ijumaa Saa 2 Usiku, Bongo Taimu.

Sheria za FA zinakataza Posti kwenye Mitandao ya Kijamiii zinazohoji uadilifu wa Marefa.