WENGER AUNGAMA CHELSEA NI ‘MABINGWA WATARAJIWA’!

>CHELSEA WAIKARIBIA REKODI YA ARSENAL LIGI KUU ENGLAND!

WENGER-ATAFAKARIArsene Wenger amekiri kuwa Chelsea ndio ‘Mabingwa Watarajiwa’ wa EPL, Ligi Kuu Vodacom, huku wakiwa mbioni kuikaribia Rekodi ya Arsenal ya Kushinda Mechi nyingi mfululizo waliyoiweka zaidi ya Muongo Mmoja uliopita.

Chelsea wanaongoza EPL wakiwa Pointi 6 mbele ya Timu ya Pili Liverpool baada ya kushinda Mechi 12 mfululizo.

Tangu wapigwe 3-0 na Arsenal Septemba 24, Meneja wa Chelsea Antonio Conte alibadili Fomesheni ya Timu yake na kutumia Mfumo wa 3-4-3 ambao umewapa mafanikio makubwa mno.

+++++++++++++++++++++++

EPL – Rekodi za Kushinda Mechi nyingi mfululizo:

Mechi 14, Arsenal, Februari-Agosti 2002

12, Manchester United, Machi-Agosti 2000

11, Chelsea, Aprili-Septemba 2009

11, Manchester United, Desemba 2008-Machi 2009

11, Liverpool, Februari-April1 2014

+++++++++++++++++++++++

Wenger, ambae Timu yake Arsenal wapo Nafasi ya 4 wakiwa Pointi 9 nyuma ya

Chelsea, ameungama: “Kwa sasa Chelsea ndio Mabingwa Watarajiwa. Ni Ubingwa wao labda waupoteze tu. Kwa sasa ni Mabingwa labda waupoteze tu!”

Lakini Wenger pia amekiri: “Bado mbio ni ndefu na ni ngumu kwa kila mtu hivyo Mechi za uso kwa uso zitakuwa muhimu mno!”

Wenger ametoboa kuwa Meneja wa Chelsea Antonio Conte amefanya kazi njema kuisuka upya Timu na pia kutaja kuwa ujio wa Mbrazil David Luiz umeimarisha Difensi yao na kuleta uwiano mzuri.

Msimu wa 2001/02, Arsenal walishinda Mechi 13 mfululizo wakielekea kutwaa Ubingwa wa England na Msimu uliofuatia waliivunja Rekodi hiyo kwa kushinda Mechi 14 mfululizo.

Wenger amekubali kuwa atapaswa kuipa Chelsea hongera wakiivunja Rekodi ya Arsenal.