EPL: LIVERPOOL YAIFYEKA STOKE, WASHIKA NAFASI YA PILI!

>JUMATANO ‘WATAKATIFU’ DHIDI YA SPURS!

LIVER-STOKE-GOLIKWENYE Mechi pekee ya EPL, Ligi Kuu England, iliyochezwa Jumatatu Usiku huko Anfield Liverpool wameichapa Stoke City 4-1 na kukamata Nafasi ya Pili ya Ligi hiyo.

Stoke walipata Bao lao Dakika ya 12 kutokana na Krosi ya Pieters kutoka kushoto na Jonathan Walters kutangulia mbele ya Beki Lovren na kuunganisha kwa Kichwa hadi wavuni.

Liverpool wakasawazisha Dakika ya 35 kwa Krosi ya Sadio Mane kumbabatiza Beki Johnson na kumrudia Adam Lallana aliekwamisha Mpira wavuni.

Liverpool wakaenda Haftaimu 2-1 mbele kwa Goli la Dakika ya 44 la Roberto Firmino kufuatia ushirikiano mzuri na James Milner.EPL-DES27

Bao la 3 la Liverpool lilifungwa Dakika ya 60 kwa Imbula kujifunga mwenyewe akitaka kuosha Krosi ya Origi.

Sekunde 54 tu tangu aingizwe Uwanjani kumbadili Origi, Daniel Sturridge aliipa Liverpool Bao la 4 alipoinasa Pasi ya nyuma ya Beki Shawcross kwa Kipa wake Grant na kufunga kilaini.

+++++

MAGOLI:

Liverpool 2

Adam Lallana, Dakika ya 34

Roberto Firmino, 44

Imbula, 60 [Kajifunga Mwenyewe]

Daniel Sturridge, 70

Stoke 1

Jonathan Walters, Dakika ya 12

+++++

Ushindi huu umewaweka Liverpool Nafasi ya Pili kwenye EPL wakiwa Pointi 6 nyuma ya Vinara Chelsea na Pointi 1 mbele ya Timu ya 3 Man City huku zote zikiwa zimecheza Mechi 18.

Mechi inayofuata kwa Liverpool ni tena Anfield Jumamosi Desemba 31 dhidi ya Man City.

EPL itaendelea tena Jumatano kwa Mechi moja tu huko Saint Mary kati ya Southampton na Tottenham Hotspur.

Mechi nyingine ni Ijumaa wakati Hull City ikicheza na Everton.

VIKOSI:

LIVERPOOL: Mignolet, Clyne, Klavan, Lovren, Milner, Lallana [Can 69'], Henderson, Wijnaldum, Mane, Origi [Sturridge 70'], Firmino

Akiba: Karius, Sturridge, Moreno, Lucas, Can, Ejaria, Woodburn

STOKE CITY: Grant, Johnson, Shawcross, Martins Indi, Pieters, Whelan [Sobhi 66'], Imbula, Walters, Allen, Diouf, Crouch

Akiba: Bony, Afellay, Adam, Shaqiri, Given, Krkic, Sobhi

REFA: Michael Oliver

EPL, LIGI KUU ENGLAND

Ratiba:

**Saa za Bongo

Jumatano Desemba 28

2245 Southampton v Tottenham Hotspur                  

Ijumaa Desemba 30

2300 Hull City v Everton             

Jumamosi Desemba 31

1800 Burnley v Sunderland         

1800 Chelsea v Stoke City          

1800 Leicester City v West Ham United           

1800 Manchester United v Middlesbrough                 

1800 Southampton v West Bromwich Albion              

1800 Swansea City v Bournemouth                 

2030 Liverpool v Manchester City         

Jumapili Januari 1

1630 Watford v Tottenham Hotspur                

1900 Arsenal v Crystal Palace               

Jumatatu Januari 2

1530 Middlesbrough v Leicester City               

1800 Everton v Southampton               

1800 Manchester City v Burnley            

1800 Sunderland v Liverpool                

1800 West Bromwich Albion v Hull City           

2015 West Ham United v Manchester United             

Jumanne Januari 3

2245 Bournemouth v Arsenal                

2300 Crystal Palace v Swansea City                

2300 Stoke City v Watford 20:00

Jumatano Januari 4

2300 Tottenham Hotspur v Chelsea                 

 

 

Habari MotoMotoZ