EPL: LEO LIVERPOOL KUITOA CITY NAFASI YA PILI?

>JUMATANO ‘WATAKATIFU’ DHIDI YA SPURS!

EPL, LIGI KUU ENGLAND

Ratiba:

**Saa za Bongo

Jumanne Desemba 27

2015 Liverpool v Stoke City        

++++++++++++++++++++++++++

LIVER-STOKELEO EPL, Ligi Kuu England, ipo Mechi 1 tu huko Anfield kati ya Liverpool na Stoke City.

Katika Mechi ya mwisho hapo Jana, Man City iliitandika Hull City 3-0 kwa Bao za Yaya Toure, Penati, Iheanacho na Davies aliejifunga mwenyewe.

Liverpool wanashikilia Nafasi ya 3 wakiwa na Pointi 37 sawa na Timu ya 4 Arsenal na kuzidiwa na Timu ya Pili Manchester City Pointi 2 huku Vinara wakiwa Chelsea wenye Pointi 46.

Stoke City wapo Nafasi ya 12 wakiwa na Pointi 21.EPL-DES26B

Liverpool wataingia kwenye Mechi hii wakimkosa Majeruhi Philippe Coutinho lakini Beki wao Joel Matip ameshapona na huenda akapewa nafasi.

Kwa Stoke, Fowadi wao Marko Arnautovic bado yupo Kifungoni baada ya kutolewa kwa Kadi Nyekundu kwenye Mechi na Southampton mapema Mwezi huu.

Uso kwa Uso

Liverpool wameshinda Mechi 5 kati ya 6 zilizopita za EPL dhidi ya Stoke na Msimu uliopita kwenye Mechi kama hii walishinda 4-1.

Katika kipindi hicho, Mechi pekee Stoke waliyoshinda ni Bao 6-1 kwenye Mechi ambayo ilikuwa ya mwisho kabisa kwa Nahodha wao maarufu Steven Gerrard.

Pia Stoke walishinda 1-0 Mwezi Januari katika Mechi ya Pili ya Nusu Fainali ya Kombe la Ligi ingawa walishindwa Nusu Fainali hiyo kwa Mikwaju ya Penati Tano Tano zilizopigwa baada ya Mechi 2 za Nusu Fainali kufungana.

VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:

LIVERPOOL: Mignolet, Clyne, Lovren, Klavan, Milner, Lallana, Henderson, Wijnaldum, Mane, Origi, Firmino

STOKE CITY: Grant, Johnson, Shawcross, Martins Indi, Pieters, Whelan, Imbula, Diouf, Allen, Krkic, Walters

REFA: Michael Oliver

EPL, LIGI KUU ENGLAND

Ratiba:

**Saa za Bongo

Jumatano Desemba 28

2245 Southampton v Tottenham Hotspur                  

Ijumaa Desemba 30

2300 Hull City v Everton             

Jumamosi Desemba 31

1800 Burnley v Sunderland         

1800 Chelsea v Stoke City          

1800 Leicester City v West Ham United           

1800 Manchester United v Middlesbrough                 

1800 Southampton v West Bromwich Albion              

1800 Swansea City v Bournemouth                 

2030 Liverpool v Manchester City         

Jumapili Januari 1

1630 Watford v Tottenham Hotspur                

1900 Arsenal v Crystal Palace               

Jumatatu Januari 2

1530 Middlesbrough v Leicester City               

1800 Everton v Southampton               

1800 Manchester City v Burnley            

1800 Sunderland v Liverpool                

1800 West Bromwich Albion v Hull City           

2015 West Ham United v Manchester United             

Jumanne Januari 3

2245 Bournemouth v Arsenal                

2300 Crystal Palace v Swansea City                

2300 Stoke City v Watford 20:00

Jumatano Januari 4

2300 Tottenham Hotspur v Chelsea                 

 

 

Habari MotoMotoZ