EPL – BOKSING DEI: LEO MOU NA MAN UNITED KUMBWAGA MOYES ANAEREJEA OLD TRAFFORD MARA YA KWANZA TANGU AFUKUZWE?

EPL, LIGI KUU ENGLAND

Ratiba:

**Saa za Bongo

Jumatatu Desemba 26

1530 Watford v Crystal Palace              

1800 Arsenal v West Bromwich Albion            

1800 Burnley v Middlesbrough              

1800 Chelsea v Bournemouth               

1800 Leicester City v Everton               

1800 Manchester United v Sunderland            

1800 Swansea City v West Ham United           

2015 Hull City v Manchester City 

++++++++++++++++++++++++++

MANUNITED-SUNDERLAND-DEC26LEO katika Moja ya Mechi 8 za EPL, Ligi Kuu England,ni ile itakayochezwa huko Old Trafford kati ya Manchester United na Sunderland na mvuto mkubwa ni kurejea tena Uwanjani hapo kwa David Moyes kwa mara ya kwanza tangu atimuliwe Umeneja na Man United Aprili 2014.

Mwenyewe Moyes ameshakiri kuwa ni kitu kisichowezekana kuendeleza urithi wa Meneja Lejendari Sir Alex Ferguson.

Lakini Meneja wa sasa wa Man United, Jose Mourinho, ametoboa anafurahia changamoto hizo na hataruhusu presha zimshinde.

Akiongea kuelekeaechi hii ya Leo, Mourinho ameeleza: “Sioni kama ni mzigo. Nahisi Historia kubwa ya Klabu hii ni kitu kizuri na siwazii mabaya. Tatizo ukipewa masharti ya kufuata!”

Alipoulizwa kama Moyes ndie alikuwa na chamoto kubwa kwani ndie alierithi moja kwa moja toka kwa Ferguson, Mourinho alijibu: “Sitajali kuwa kwenye Klabu yenye matumaini makubwa lakini kuwa nao Ryan Giggs, NemanjaEPL-DES25 Vidic, Patrice Evra na Chicharito kwenye Timu. Hilo sijali hata kidogo!”

Tahmini

Man United wanatinga kwenye Mechi hii wakiwa wameshinda Mechi 4 mfululizo katika Mashindano yote na kuzoa Pointi 9 kati ya 9 kwenye EPL.

Sunderland, walioanza Msimu vibaya, walijikongoja Mwezi Novemba wakishinda Mechi 2 kati ya 3 na Mwezi huu walishinda Mechi zao 2 za Nyumbani dhidi ya Leicester na Watford na kuleta matumaini mapya.

Wakati Man United wapo Nafasi ya 6, Pointi 3 nyuma ya Timu ya 5 Tottenham na 4 nyuma ya Arsenal ambao ni wa 4, Sunderland wapo Nafasi ya 18 wakiwemo kwenye zile 3 za Mkiani ambazo hushuka Daraja mwishoni mwa Msimu.

Msimu uliopita:

Man United waliichapa Sunderland 3-0 Uwanjani Old Trafford kwa Bao za Wayne Rooney, Memphis Depay na Juan Mata na kufungwa 2-1 huko Stadium of Light..

Hali za Wachezaji:

Man United:

Hatihati: Bailly, Mkhitaryan [Bado hawajawa fiti kwa Mechi]

Majeruhi: Luke Shaw, Wilson

Sunderland:

Majeruhi:Rodwell (hamstring, 14 Jan), Gooch (ankle, Mar), Cattermole (hip, Apr), Kirchoff (knee, Apr), McNair (knee, Aug), Watmore (knee, Aug)

**Adnan Januzaj haruhusiwi kuichezea Sunderland kwenye Mechi hii kutokana na Mkataba wake wa Mkopo kutoka Man United.

VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:

MAN UNITED: De Gea, Valencia, Jones, Rojo, Darmian, Carrick, Herrera, Mkhitaryan, Pogba, Martial, Ibrahimovic

Akiba: Romero, Depay, Lingard, Fosu-Mensah, Tuanzebe, Schneiderlin, Young, Blind, Fellaini, Schweinsteiger, Bailly, Rashford, Rooney, Mata, Smalling

SUNDERLAND: Pickford, Jones, Kone, Djilobodji, Van Aanholt, Denayer, Ndong, Khazri, Borini, Anichebe, Defoe

Akiba: Mannone, Love, Manquillo, O’Shea, Larsson, Pienaar, Honeyman, Asoro, E Robson, J Robson, T Robson

REFA: Martin Atkinson

EPL, LIGI KUU ENGLAND

Ratiba:

**Saa za Bongo

Jumanne Desemba 27

2015 Liverpool v Stoke City                  

Jumatano Desemba 28

2245 Southampton v Tottenham Hotspur                  

Ijumaa Desemba 30

2300 Hull City v Everton             

Jumamosi Desemba 31

1800 Burnley v Sunderland         

1800 Chelsea v Stoke City          

1800 Leicester City v West Ham United           

1800 Manchester United v Middlesbrough                 

1800 Southampton v West Bromwich Albion              

1800 Swansea City v Bournemouth                 

2030 Liverpool v Manchester City         

Jumapili Januari 1

1630 Watford v Tottenham Hotspur                

1900 Arsenal v Crystal Palace               

Jumatatu Januari 2

1530 Middlesbrough v Leicester City               

1800 Everton v Southampton               

1800 Manchester City v Burnley            

1800 Sunderland v Liverpool                

1800 West Bromwich Albion v Hull City           

2015 West Ham United v Manchester United             

Jumanne Januari 3

2245 Bournemouth v Arsenal                

2300 Crystal Palace v Swansea City                

2300 Stoke City v Watford 20:00

Jumatano Januari 4

2300 Tottenham Hotspur v Chelsea