EPL – BOKSING DEI: MECHI 8 ZA KUANZIA WIKI NGUMU KUELEKEA MWAKA MPYA!

EPL, LIGI KUU ENGLAND

Ratiba:

**Saa za Bongo

Jumatatu Desemba 26

1530 Watford v Crystal Palace              

1800 Arsenal v West Bromwich Albion            

1800 Burnley v Middlesbrough              

1800 Chelsea v Bournemouth               

1800 Leicester City v Everton               

1800 Manchester United v Sunderland            

1800 Swansea City v West Ham United           

2015 Hull City v Manchester City 

++++++++++++++++++++++++++

EPL-2016-17-LOGO2BOKSING DEI, Jumatatu Desemba 26, ni Siku ambayo EPL, Ligi Kuu England, itaanza mfululizo wa Mechi zake kuelekea Mwaka Mpya na Siku hiyo zipo Mechi 8.

Fungua dimba kwa Siku hiyo ni huko Vicarage Road wakati Watford wakicheza na Crystal Palace ambayo itakuwa ni Mechi ya kwanza kwa Meneja mpya Sam Allardyce tangu apewe madaraka huko Palace Wiki iliyopita.

Jioni Saa 12 zipo Mechi 6 wakati Arsenal wakiikaribisha West Bromwich Albion, Burnley EPL-DES25kucheza na Middeslbrough, Vinara wa Ligi hii Chelsea kuwa kwao Stamford Bridge kucheza na Bournemouth, Mabingwa watetezi, Leicester City, wakiwa bila Straika wao mkuu Jamie Vardy aliefungiwa Mechi 3, kucheza na Everton.

Nyingine ni huko Old Trafford wakati Manchester United ikiikaribisha Sunderland ambao Meneja wao ni David Moyes aliewahi kuwa Meneja wa Man United na kutimuliwa Mwaka 2014 na Swansea City kucheza na West Ham United.

Mechi ya mwisho kwa hiyo Boksing Dei ni ya Usiku kati ya Hull City na Manchester City.  

EPL, LIGI KUU ENGLAND

Ratiba:

**Saa za Bongo

Jumanne Desemba 27

2015 Liverpool v Stoke City                  

Jumatano Desemba 28

2245 Southampton v Tottenham Hotspur                  

Ijumaa Desemba 30

2300 Hull City v Everton             

Jumamosi Desemba 31

1800 Burnley v Sunderland         

1800 Chelsea v Stoke City          

1800 Leicester City v West Ham United           

1800 Manchester United v Middlesbrough                 

1800 Southampton v West Bromwich Albion              

1800 Swansea City v Bournemouth                 

2030 Liverpool v Manchester City         

Jumapili Januari 1

1630 Watford v Tottenham Hotspur                

1900 Arsenal v Crystal Palace               

Jumatatu Januari 2

1530 Middlesbrough v Leicester City               

1800 Everton v Southampton               

1800 Manchester City v Burnley            

1800 Sunderland v Liverpool                

1800 West Bromwich Albion v Hull City           

2015 West Ham United v Manchester United             

Jumanne Januari 3

2245 Bournemouth v Arsenal                

2300 Crystal Palace v Swansea City                

2300 Stoke City v Watford 20:00

Jumatano Januari 4

2300 Tottenham Hotspur v Chelsea