UBAGUZI WAMPA KIFUNGO MCHEZAJI MECHI 5, RUFAA YA VARDY YATUPWA SASA NI KIFUNGO MECHI 3!

WAKATI Fowadi wa England anaechezea kwa Mabingwa Leicester City Jamie Vardy akitakiwa kutumikia Kifungo cha Mechi 3 baada ya Rufaa yake kupinga Kadi Nyekundu kutupwa, Kiungo mwingine aliewahi kuichezea England amefungiwa Mechi 5 kwa Ubaguzi Uwanjani.

NJONJO SHELVEY AFUNGIWA MECHI 5 KWA UBAGUZI

NJONJO-MBAGUZIKiungo wa Newcastle Jonjo Shelvey amefungiwa Mechi 5 na kutwangwa Faini ya Pauni 100,000 na FA, Chama cha Soka England baada ya kupatikana na hatia ya kutumia Lugha chafu ya Kibaguzi Uwanjani.

Tukio lilomhukumu Njonjo, ambae alishawahi kukwaruzana na Sir Alex Ferguson Uwanjani kwenye Mechi alipokuwa akiichezea Liverpool walipobamizwa na Manchester United, lilitokea Dakika ya 87 kwenye Mechi ya Newcastle na Wolverhampton Wanderers Jumamosi Septemba 17 alipomkashifu Kiungo kutoka Morocco, Romain Saiss, na Mchezaji mwingine wa Wolves kuliripoti kwa Refa Tim Robinson mara tu baada ya Mechi.

Njonjo amepewa Siku 7 kukata Rufaa ikiwa anapinga Adhabu yake.

VARDY: RUFAA YATUPWA KIFUNGO MECHI 3!

Straika wa Mabingwa wa England Leicester City anaechezea England Jamie Vardy sasa atakosa Mechi 3 baada ya Rufaa yake kupinga Kadi Nyekundu aliyopewa Jumamosi Leicester ikitoka 2-2 na Stoke City kutupiliwa mbali.

Vardy, mwenye Miaka 29, atazikosa Mechi za Leicester dhidi ya Everton, West Ham na Middlesbrough.

Vardy alitolewa nje na Refa Craig Pawson katika Dakika ya 28 kwa Rafu ya Miguu Miwili kwa Straika wa Stoke Mame Diouf.

Habari MotoMotoZ