EPL: SPURS YAITANDIKA WBA 4-0, WAPO WA PILI!

> BIGI MECHI JUMAPILI OLD TRAFFORD MAN UNITED-LIVERPOOL!
EPL – Ligi Kuu England
Ratiba/Matojkeo:
**Saa za Bongo
Jumamosi Januari 14
Tottenham Hotspur 4 West Bromwich Albion 0
1800 Burnley v Southampton
1800 Hull City v Bournemouth
1800 Sunderland v Stoke City
1800 Swansea City v Arsenal
1800 Watford v Middlesbrough
1800 West Ham United v Crystal Palace
2030 Leicester City v Chelsea
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++
SPURS-KANE-HETITRIKI-SITEPL, Ligi Kuu England, imerejea Leo baada kukosekana tangu Januari 4 kwa Mechi ya mapema huko White Hart Lane Jijini London na Wenyeji Tottenham Hotspur kuifunga West Bromwich Albion 4-0.
Ushindi huu wa Spurs umewaweka Nafasi ya Pili kwenye EPL wakiwa Pointi 4 nyuma ya Vinara Chelsea ambao ndio waliwafunga hapo hapo White Hart Lane 2-0 kwenye Mechi yao ya mwisho Januari 4.
Spurs waliweka Bao lao la kwanza Dakika ya 12 baada Pasi ya Christian Eriksen kumkuta Harry Kane na kufunga.
Bao la Pili la Spurs lilifungwa Dakika ya 26 kufuatia Shuti la Christian Eriksen kumgonga Mchezaji wa WBA Jonas Olsson na kisha mwenzake Gareth McAuley na kutinga.
Hadi Haftaimu Spurs 2 WBA 0.
Kipindi cha Pili Harry Kane alikamilisha Hetitriki yake kwa kufunga Bao 2 Dakika za 77 na 82 na kuiweka Spurs 4-0 mbele.
Baadae Leo zipo Mechi kadhaa za EPL na Jumapili zipo Mechi 2 ikianza ile ya Goodison Park kati ya Everton, walio Nafasi ya 7,
na Man City ambao wako Nafasi ya 4.
Kisha utafuata mtanange huko Old Trafford wakati Man United ambao wapo kwenye wimbi la kushinda Mechi 9 mfululizo wakicheza na Mahasimu wao wa Jadi Liverpool.
Wimbi hili la ushindi kwa Man United ni refu tangu Msimu wa 2008/09 waliposhinda Mechi 11
mfululizo kati ya Januari na Februari na kuelekea kutwaa Ubingwa wa England na
Kombe la Ligi wakiwa chini ya Meneja Lejendari Sir Alex Ferguson.
VIKOSI VILIVYOANZA:
TOTTENHAM HOTSPUR (Mfumo 3-4-2-1): Lloris; Dier, Alderweireld, Vertonghen; Walker, Wanyama, Dembele, Rose; Eriksen, Dele; Kane
Akiba: Vorm, Trippier, Davies, Nkoudou, Sissoko, Winks, Son
WEST BROM (Mfumo 4-2-3-1): Foster; Dawson, McAuley, Olsson, Brunt; Fletcher, Yacob; Chadli, Morrison, Phillips; Rondon
Akiba: Myhill, Galloway, Leko, McClean, Field, Robson-Kanu, Wilson
REFA: Anthony Taylor
EPL – Ligi Kuu England
Ratiba
**Saa za Bongo
Jumapili Januari 15
1630 Everton v Manchester City
1900 Manchester United v Liverpool
Jumamosi Januari 21
1530 Liverpool v Swansea City
1800 Bournemouth v Watford
1800 Crystal Palace v Everton
1800 Middlesbrough v West Ham United
1800 Stoke City v Manchester United
1800 West Bromwich Albion v Sunderland
2030 Manchester City v Tottenham Hotspur
Jumapili Januari 22
1500 Southampton v Leicester City
1715 Arsenal v Burnley
1930 Chelsea v Hull City

BARCA YAKWAMA KUMUONGEZA DAU MESSI!

==KWA SASA, NEYMAR, SUAREZ WAZOA MKWANJA JUU KUPITA MESSI!
BARCA-MESSI-TODOSOMOSMKURUGENZI MTENDAJI MKUU wa FC Barcelona, Òscar Grau, ametoboa kuwa kwa sasa wameshindwa kumpa Lionel Messi Mkataba mpya baada kubanwa na Kanuni za La Liga.
Kwa sasa, Mkataba wa Messi unaokwisha baada ya Miezi 18, unampa Mshahara wa Euro Milioni 22 kwa Mwaka baada kukatwa Kodi.
Lakini wenzake, Neymar na Luis Suarez, ambao hivi karibuni walisaini Dili Mpya zinazoisha 2021, wanazoa kitita cha Euro Milioni 25 kwa Mwaka baada ya Kodi.
Mkataba wa Messi unamalizika Tarehe 30 Juni 2018 na baada ya hapo yupo huru kuondoka bila Barca kulipwa hata Senti.
Barca wamekwama kumuongeza Messi Mshahara kwa vile wanabanwa na Kanuni za La Liga zinazotaka kila Klabu kutozidi Asilimia 70 ya Bajeti yao kwa kulipia Mishahara.
Oscar Grau ameeleza: "Barcelona inabidi iwe makini. Barca hairuhusiwi kuvuka Asilimia 70 ya Bajeti kwa kulipia Mishahara!"
Kwa mujibu wa Takwimu, Barca ndio wanaolipa Mishahara mikubwa huko Spain na Duniani ni wa Pili nyuma ya Manchester United.
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Barca, Grau, amedokeza kuwa watapaswa kuuza Wachezaji na pia kuimarisha Mapato ya Kibiashara ikiwa watataka kuvuna Fedha zaidi ili kuboresha Maslahi ya Wachezaji waliopo.

SAGNA KIKAANGONI PILATO WA FA, RUFAA YA JOHN TERRY YATUPWA, SASA KIFUNGO, NAE AYALA WA BORO KIFUNGO MECHI 3!

SAGNAMchezaji wa Manchester City Bacary Sagna amefunguliwa Mashitaka na FA, Chama cha Soka England, kuhusu Posti yake Mtandaoni Instagram alipohoji umakini wa Refa Lee Mason na wakati huo huo Rufaa ya Nahodha wa Chelsea John Terry atatumikia Kifungo baada ya Rufaa yake kupinga Kadi Nyekundu kutupiliwa mbali.

Sagna aliandika kwenye Instagram: “10 dhidi ya 12…lakini tulipigana na tulishinda kama Timu!”

Posti hiyo ilitoka mara baada ya City kuifunga Burnley 2-1 Wiki iliyopita huko Etihad Stadium kwenye Mechi EPL, Ligi Kuu England, ambayo City walibaki Mtu 10 kuanzia Dakika ya 32 kufuatia Kiungo wao Fernandinho kutolewa kwa Kadi Nyekundu na Refa Lee Mason kufuatia Rafu mbaya.

Sheria za FA zinakataza Posti kwenye Mitandao ya Kijamiii zinazohoji uadilifu wa Marefa.

Sagna, ambae ameomba radhi kuhusu Posti hiyo, amepewa hadi Saa 3 Usiku, Saa za Bongo, Ijumaa Januari 13 kujibu Shitaka lake.

WAKATI HUO HUO, Rufaa ya Nahodha wa Chelsea John Terry kupinga Kadi Nyekundu aliyopewa Jumapili walipocheza na Peterborough kwenye FA CUP imegonga mwamba na sasa atatumikia Kifungo cha Mechi 1.

Adhabu hii itamfanya Terry aikose Mechi ya EPL dhidi ya Mabingwa Watetezi Leicester City hapo Jumamosi.

FA pia imethibitisha Beki wa Middlesbrough, Klabu ya EPL maarufu kama Boro, Daniel Ayala atatumikia Kifungo cha Mechi 3 baada ya Rufaa kupinga Kadi Nyekundu aliyopewa kwenye Mechi ya FA CUP na Sheffield Wednesday Wikiendi iliyopita kutupwa.

NINGEKUWA GEORGE LWANDAMINA…

Na Mwandishi Wetu

received 1116887348410041MOJA kati ya burudani kubwa watakayokutana nayo Wazanzibari kwa mwaka 2017, ni kuutazama mchezo wa kwanza wa ‘Dar es Salaam derby’ ukichezwa katika ardhi yao.
Simba watavaana na Yanga kwenye nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi, ni mchezo wa kikubwa unaohitaji maamuzi ya kikubwa kuuamua.
Mimi ningekuwa kwenye nafasi ya kocha mkuu wa Yanga, George Lwandamina, ningefanya mabadiliko kwenye mambo matatu makubwa ambayo kwa namna moja au nyingine yangeweza kuisaidia Yanga kupata ushindi dhidi ya Simba na kufuta aibu ya kichapo cha bao 4-0 walichokipata mbele ya Azam.
Kwanini Makapu na si Zulu?
Katika michezo michache aliyocheza akiwa na jezi ya Yanga, tayari Justine Zulu ameshaonyesha ni mchezaji wa aina gani.
Ni mtulivu, mbunifu asiye na haraka uwanjani. Anakaba kwenye njia, si kiungo wa kukaba mtu kwa mtu, kitaalamu inaitwa ‘man to man marking’.
Kwa aina yake ya uchezaji si mtu sahihi sana kwenye safu ya kiungo ya Yanga kwenye mchezo dhidi ya Simba. Kwanini? Ipo sababu moja tu ya msingi.
Dakika 90 za pambano la Azam zimetosha kabisa kuuonyesha udhaifu wa Zulu pindi anapokutana na viungo wasumbufu na wenye uwezo mkubwa wa kumiliki mpira.
Kuzidiwa kwa safu ya kiungo, kuliifanya safu ya ulinzi iliyokuwa ikiongozwa na Dante na Yondani kuelemewa na mashambulizi na wakati mwingine kupelekea kufanya makosa mengi yalioigharimu Yanga.
Uwepo wa Makapu utapunguza muda wa viungo wa Simba kukaa na mpira na kutengeneza nafasi, ni hatari zaidi kama utamwachia Muzamir sekunde tano za kukaa na mpira huku akilitazama lango lako.
Yanga wanamhitaji zaidi Makapu kuilinda safu yao ya ulinzi kwa kumnyima uhuru Muzamir, Zulu asubiri kwanza!
Kwanini Kaseke na si Msuva?
Unaweza ukawa umeshtuka hapa, lakini haya ndiyo mabadiliko ambayo ningeyafanya katika kikosi cha Yanga, kwanini Msuva hastahili kuanza kwenye pambano hili?
Kwanza Lwandamina anatakiwa afahamu presha waliyonayo Yanga kwenye pambano hili, ushindi dhidi ya Simba ni muhimu zaidi ya Kombe la Mapinduzi.
Ili kuikwepa presha ya mchezo huu unatakiwa kuwa na wachezaji wenye uwezo mkubwa wa kuhimili presha ya matokeo, rekodi ya Msuva dhidi ya Simba inafahamika.
Kwa faida yake na timu, Msuva si mtu sahihi kwa kuanza pambano hili. Hii ni sababu ya kwanza, ya pili ipo kiufundi zaidi.
Ni kama Yanga wameshazoeleka kimfumo na ni rahisi mno kupambana nao kwa kuwa kila kocha anajua kuwa uimara wao uko kwenye wingi za pembeni.
Unaweza kuwavuruga Simba kwa kumweka nje Msuva na kumpanga Kaseke ukiwa na mbinu nyingine ya kimchezo, mbinu gani? Tulia nikwambie.
Kwa kuitazama Simba, uimara wao umejengwa kupitia wachezaji wawili kwenye safu yao ya kiungo. Jonas Mkude na Muzamir Yassin.
Mkude ndiye anayetengeneza mashambulizi ya Simba kutoka nyuma na Muzamir ndiye anayemaliza kazi kwa kupiga asisti ya mwisho au kufunga, unahitaji kuwa na wachezaji wawili kuwapoteza watu hawa.
Muzamir tayari atakuwa kazini na Makapu na si mbaya ukampanga Kaseke kudili na Jonas Mkude, kuna faida inaweza kupatikana hapa, kivipi? Mfumo wangu utaeleza zaidi.
Kwanini 4-2-3-1?
Golini bado ningemweka Deogratius Munishi ‘Dida’, watu wanne wa nyuma ningeweka wale wale, Juma Abdul, Mwinyi Haji, Dante na Kelvin Yondani.
Viungo wawili wa kati, ningewapanga Makapu na Deus Kaseke, watatu wa mbele kidogo ningewasimamisha Haruna Niyonzima (akicheza kutoka upande wa kulia), Kamusoko na Donald Ngoma (akishambulia kutoka kushoto), mbele angesimama Amissi Tambwe.
Nini nategemea kwenye mfumo huu? Kwanza Lwandamina anatakiwa aamini kuwa Kamusoko si mkabaji, ni kiungo mchezeshaji anayetakiwa kuwa huru katikati ya uwanja.
Ukimpanga pamoja na Haruna ni lazima uhakikishe una watu wawili wenye mapafu ya mbwa kuusaka mpira, hapa ndipo ninapoiona faida ya Kaseke kwenye mfumo huu.
Kazi ya Kaseke ni kuhakikisha Mkude hapati nafasi ya kutulia na mpira na Makapu kazi yake ni kumpoteza Muzamir dimbani.
Ukimpoteza Mkude na Muzamir na ukamuweka Ngoma upande wa kushoto, ni wazi utaiua nguvu ya Simba katikati na upande wa kulia.
Omog amekuwa na tabia ya kumpanga Shiza Kichuya upande wa kulia, faida ya Kichuya ipo pale timu inaposhambulia lakini si mtu mwenye uwezo wa kushuka na kumsaidia Bukungu.
Ngoma akicheza kutoka kushoto, bila shaka utaua safari za Bukungu na utamfanya Abdi Banda kutumia muda mwingi pembeni ya uwanja.
Banda akisogea kushoto ni faida kwa Tambwe atakayesalia katikati na Method Mwanjali. 
Upande wa kushoto, Niyonzima atakuwa na Tshabalala. 
Unaijua faida ya Niyonzima upande huo? Kumzidi Tshabalala hutakiwi kuwa na mbio, asilimia 90 ya uchezaji wao inatakiwa iwe akili na nguvu.
Niyonzima atamfanya Tshabalala awe naye kwa makini zaidi na kutoa mwanya kwa Juma Abdul kucheza kwa urahisi na winga wa Simba, yoyote yule atakayepangwa, iwe Mo Ibrahim au Pastory Athanas, wote ni watu ambao Juma ana uwezo wa kucheza nao ‘one against one situation.’

MOURINHO: ‘BADO HATUJAPATA OFA ZA KURIDHISHA KWA MORGAN SCHNEIDERLIN NA MEMPHIS DEPAY’

MANUNITED-SCHNEIDERLIN-DEPAYWACHEZAJI WAWILI wa Manchester United, Morgan Schneiderlin na Memphis Depay, hawatakuwemo kwenye Vikosi vya Mechi za Timu yao hadi ijulikane nini hatima yao kwa mujibu wa Meneja Jose Mourinho.

Wawili hao hawajaichezea Man United tangu Novemba huku wakihusishwa na kuihama Timu hiyo kwenye Dirisha la Uhamisho la hii Januari.

Inategemewa Schneiderlin, mwenye Miaka 27, atakwenda Everton.

Lakini Mourinho amesema: “Ntawaruhusu wote Wawili kuondoka ikiwa tutapa Ofa safi. Hadi sasa hamna Ofa hiyo! Hatujapata Ofa inayolingana na ubora wa uchezaji wao!”

Jumamosi Man United wanacheza na Reading kwenye Mechi ya Raundi ya 3 ya FA CUP Uwanjani Old Trafford na Mourinho amesema hali ingekuwa kawaida Wachezaji hao Wawili wangekuwemo kwenye Kikosi cha Mechi hiyo.

Mourinho ameeleza: “Hawamo Kikosini kwa sababu tulikuwa tukingoja kitu ambacho Wiki kadhaa nyuma kilionekana kipo tayari Asilimia 100 lakini sasa ni Asilimia 0!”

Mbali ya Everton kumtaka Schneiderlin, West Bromwich Albion pia ilitoa Ofa ya Pauni Milioni 15 kumnunua na kukataliwa.

Vile vile Everton inamtaka Winga Depay, mwenye Miaka 22, ingawa pia Klabu kadhaa za Ulaya pia zinatajwa.

Habari MotoMotoZ