AFCON 2017: MABINGWA IVORY COAST SARE NA TOGO YA ADEBAYOR!

>KUFUATA MECHI YA CONGO DR NA MOROCCO!

AFCON2017-VIWANJA4AFCON 2017, Mashindano ya 31 ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, yameendelea tena huko Nchini Gabon na Sare tena kutawala katika Mechi ya Kundi C kati ya Mabingwa Ivory Coast walipotoka 0-0 na Togo huko Stade de Franceville Mjini Franceville.

Hiyo ni Mechi ya 4 ya Fainali hizi kumalizika kwa Sare na ni Mechi 1 tu iliyotoa Mshindi hapo Jana wakatiSenegal walipokuwa Nchi ya kwanza kuzoa Pointi 3 baada ya kuifunga Tunisia Bao 2-0 huko Port Gentil Stadium, Mjini Port Gentil, Nchini Gabon kwenye Mechi ya Kundi B.

++++++++++++++++++++

DONDOO ZA NDANI:

-Mvuto wa Mechi hii ilikuwa kumwona Winga wa Crystal Palace Wilfried Zaha, alieikana England, akiichezea Ivory AFCON-JAN15Coast kwa mara ya kwanza katika Mashindano rasmi wakianza kutetea Ubingwa wao huku Togo wakiongozwa na Kepteni wao Emmanuel Adebayor ambae sasa hana Klabu tangu aondoke Crystal Palace Mwezi Juni.

-Pia Kocha Mbelgiji Claude LeRoy, akionekana kwa mara ya 9 kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika akitwaa Ubingwa mara moja Mwaka 1988 akiwa na…., lakini safari hii akiwa na Togo ambayo haijawahi kuwa Bingwa.

-Ivory Coast wamekuwa Mabingwa wa AFCON mara 2 kwa kuibwaga Ghana huko Senegal (1992) na Equatorial Guinea (2015) zote kwa Penati Tano Tano baada Sare za 0-0.

++++++++++++++++++++

Baadae Leo ipo Mechi nyingine ya Kundi C kati ya Congo DR na Morocco.

Kesho Jumanne zipo Mechi mbili za Kundi D kati ya Ghana na Uganda na kisha ni

Mali na Egypt zote zikichezwa Oyem Stadium, Mjini Assok Ngomo huko Gabon.

VIKOSI VILIVYOANZA:

IVORY COAST: Gbohouo, Aurier, Bailly, Kanon, Traoré, Kessié, Serey Dié, Seri, Zaha, Kodjia, Kalou

Akiba: Mande, Pepe, N'Guessan, Koné, Angban, Doukoure, Bony, Sio, Gradel, Deli, Bagayoko, Sangaré

TOGO: Agassa, Gakpe, Romao, Ouro-Akoriko, Dakonam Ortega, Dossevi, Ayité, Atakora, Bebou, Fo-Doh Laba, Adebayor

Akiba: Mensah, Atchou, Ouro-Sama, Akakpo, Mamah, Agbégniadan, Bossou, Kouloum, Boukari, Segbefia, Eninful, Tchagouni

REFA: Eric Arnaud Otogo-Castane [Gabon]

AFCON 2017

Ratiba/Matokeo:

**Saa za Bongo

Mechi za Makundi

Jumamosi Januari 14

Kundi A

Gabon 1 Guinea-Bissau 1

Burkina Faso 1 Cameroon 1

Jumapili Januari 15

Kundi B

Algeria 2 Zimbabwe 2

Tunisia 0 Senegal 2

Jumatatu Januari 16

Kundi C

Ivory Coast 0 Togo 0

2200 Congo DR v Morocco

Jumanne Januari 17

Kundi D

1900 Ghana v Uganda

2200 Mali v Egypt

Jumatano Januari 18

Kundi A

1900 Gabon v Burkina Faso

2200 Cameroon v Guinea-Bissau

Alhamisi Januari 19

Kundi B

1900 Algeria v Tunisia

2200 Senegal v Zimbabwe

Ijumaa Januari 20

Kundi C

1900 Ivory Coast v Congo DR

2200 Morocco v Togo

Jumamosi Januari 21

Kundi D

1900 Ghana v Mali

2200 Egypt v Uganda

Jumapili Januari 22

Kundi A

2200 Cameroon v Gabon

2200 Guinea-Bissau v Burkina Faso

Jumatatu Januari 23

Kundi B

2200 Senegal v Algeria

2200 Zimbabwe v Tunisia

Jumanne Januari 24

Kundi C

2200 Morocco v­­ Ivory Coast

2200 Togo v Congo DR

Jumatano Januari 25

Kundi D

2200 Egypt v Ghana

2200 Uganda v Mali

Robo Fainali

Jumamosi Januari 28

1900 Mshindi Kundi A v Mshindi wa 2 Kundi B

2200 Mshindi Kundi B v Mshindi wa 2 Kundi A

Jumapili Januari 29

1900 Mshindi Kundi C v Mshindi wa 2 Kundi D

2200 Mshindi Kundi D v Mshindi wa 2 Kundi C

Nusu Fainali

Jumatano Februari 1

2200 Mshindi RF 1 v Mshindi RF 4

Alhamisi Februari 2

2200 Mshindi RF 2 v Mshindi RF 3

Mshindi wa 3

Jumamosi Februari 4

2200 Aliefungwa NF 1 v Aliefungwa NF 2

Fainali

Jumapili Februari 5

2200 Finalist 1 v Finalist 2

NCHI ZILIZOWAHI KUTWAA UBINGWA WA AFRIKA:

-Egypt-Mara 7
-Cameroon, Ghana-Mara 4
-Nigeria-Mara 3
-Congo DR-Mara 2
-Zambia, Algeria, Congo, Ethiopia, Ivory Coast, Morocco, South Africa, Sudan, Tunisia-Mara 1

++++++++++++++

MAKUNDI & VIWANJA:

KUNDI A: Gabon, Burkina Faso, Cameroon, Guinea-Bissau

-Uwanja: Stade de l’Amitié huko Libreville, Gabon

KUNDI B: Algeria, Tunisia, Senegal, Zimbabwe

-Uwanja: Port Gentil Stadium, Port Gentil

KUNDI C: Ivory Coast, DR Congo, Morocco, Togo

-Uwanja:Stade de Franceville, Franceville

KUNDI D: Ghana, Mali, Egypt, Uganda

-Uwanja:Oyem Stadium, Assok Ngomo

++++++++++++++

 

         

EPL: SPURS YAITANDIKA WBA 4-0, WAPO WA PILI!

> BIGI MECHI JUMAPILI OLD TRAFFORD MAN UNITED-LIVERPOOL!
EPL – Ligi Kuu England
Ratiba/Matojkeo:
**Saa za Bongo
Jumamosi Januari 14
Tottenham Hotspur 4 West Bromwich Albion 0
1800 Burnley v Southampton
1800 Hull City v Bournemouth
1800 Sunderland v Stoke City
1800 Swansea City v Arsenal
1800 Watford v Middlesbrough
1800 West Ham United v Crystal Palace
2030 Leicester City v Chelsea
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++
SPURS-KANE-HETITRIKI-SITEPL, Ligi Kuu England, imerejea Leo baada kukosekana tangu Januari 4 kwa Mechi ya mapema huko White Hart Lane Jijini London na Wenyeji Tottenham Hotspur kuifunga West Bromwich Albion 4-0.
Ushindi huu wa Spurs umewaweka Nafasi ya Pili kwenye EPL wakiwa Pointi 4 nyuma ya Vinara Chelsea ambao ndio waliwafunga hapo hapo White Hart Lane 2-0 kwenye Mechi yao ya mwisho Januari 4.
Spurs waliweka Bao lao la kwanza Dakika ya 12 baada Pasi ya Christian Eriksen kumkuta Harry Kane na kufunga.
Bao la Pili la Spurs lilifungwa Dakika ya 26 kufuatia Shuti la Christian Eriksen kumgonga Mchezaji wa WBA Jonas Olsson na kisha mwenzake Gareth McAuley na kutinga.
Hadi Haftaimu Spurs 2 WBA 0.
Kipindi cha Pili Harry Kane alikamilisha Hetitriki yake kwa kufunga Bao 2 Dakika za 77 na 82 na kuiweka Spurs 4-0 mbele.
Baadae Leo zipo Mechi kadhaa za EPL na Jumapili zipo Mechi 2 ikianza ile ya Goodison Park kati ya Everton, walio Nafasi ya 7,
na Man City ambao wako Nafasi ya 4.
Kisha utafuata mtanange huko Old Trafford wakati Man United ambao wapo kwenye wimbi la kushinda Mechi 9 mfululizo wakicheza na Mahasimu wao wa Jadi Liverpool.
Wimbi hili la ushindi kwa Man United ni refu tangu Msimu wa 2008/09 waliposhinda Mechi 11
mfululizo kati ya Januari na Februari na kuelekea kutwaa Ubingwa wa England na
Kombe la Ligi wakiwa chini ya Meneja Lejendari Sir Alex Ferguson.
VIKOSI VILIVYOANZA:
TOTTENHAM HOTSPUR (Mfumo 3-4-2-1): Lloris; Dier, Alderweireld, Vertonghen; Walker, Wanyama, Dembele, Rose; Eriksen, Dele; Kane
Akiba: Vorm, Trippier, Davies, Nkoudou, Sissoko, Winks, Son
WEST BROM (Mfumo 4-2-3-1): Foster; Dawson, McAuley, Olsson, Brunt; Fletcher, Yacob; Chadli, Morrison, Phillips; Rondon
Akiba: Myhill, Galloway, Leko, McClean, Field, Robson-Kanu, Wilson
REFA: Anthony Taylor
EPL – Ligi Kuu England
Ratiba
**Saa za Bongo
Jumapili Januari 15
1630 Everton v Manchester City
1900 Manchester United v Liverpool
Jumamosi Januari 21
1530 Liverpool v Swansea City
1800 Bournemouth v Watford
1800 Crystal Palace v Everton
1800 Middlesbrough v West Ham United
1800 Stoke City v Manchester United
1800 West Bromwich Albion v Sunderland
2030 Manchester City v Tottenham Hotspur
Jumapili Januari 22
1500 Southampton v Leicester City
1715 Arsenal v Burnley
1930 Chelsea v Hull City

BARCA YAKWAMA KUMUONGEZA DAU MESSI!

==KWA SASA, NEYMAR, SUAREZ WAZOA MKWANJA JUU KUPITA MESSI!
BARCA-MESSI-TODOSOMOSMKURUGENZI MTENDAJI MKUU wa FC Barcelona, Òscar Grau, ametoboa kuwa kwa sasa wameshindwa kumpa Lionel Messi Mkataba mpya baada kubanwa na Kanuni za La Liga.
Kwa sasa, Mkataba wa Messi unaokwisha baada ya Miezi 18, unampa Mshahara wa Euro Milioni 22 kwa Mwaka baada kukatwa Kodi.
Lakini wenzake, Neymar na Luis Suarez, ambao hivi karibuni walisaini Dili Mpya zinazoisha 2021, wanazoa kitita cha Euro Milioni 25 kwa Mwaka baada ya Kodi.
Mkataba wa Messi unamalizika Tarehe 30 Juni 2018 na baada ya hapo yupo huru kuondoka bila Barca kulipwa hata Senti.
Barca wamekwama kumuongeza Messi Mshahara kwa vile wanabanwa na Kanuni za La Liga zinazotaka kila Klabu kutozidi Asilimia 70 ya Bajeti yao kwa kulipia Mishahara.
Oscar Grau ameeleza: "Barcelona inabidi iwe makini. Barca hairuhusiwi kuvuka Asilimia 70 ya Bajeti kwa kulipia Mishahara!"
Kwa mujibu wa Takwimu, Barca ndio wanaolipa Mishahara mikubwa huko Spain na Duniani ni wa Pili nyuma ya Manchester United.
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Barca, Grau, amedokeza kuwa watapaswa kuuza Wachezaji na pia kuimarisha Mapato ya Kibiashara ikiwa watataka kuvuna Fedha zaidi ili kuboresha Maslahi ya Wachezaji waliopo.

SAGNA KIKAANGONI PILATO WA FA, RUFAA YA JOHN TERRY YATUPWA, SASA KIFUNGO, NAE AYALA WA BORO KIFUNGO MECHI 3!

SAGNAMchezaji wa Manchester City Bacary Sagna amefunguliwa Mashitaka na FA, Chama cha Soka England, kuhusu Posti yake Mtandaoni Instagram alipohoji umakini wa Refa Lee Mason na wakati huo huo Rufaa ya Nahodha wa Chelsea John Terry atatumikia Kifungo baada ya Rufaa yake kupinga Kadi Nyekundu kutupiliwa mbali.

Sagna aliandika kwenye Instagram: “10 dhidi ya 12…lakini tulipigana na tulishinda kama Timu!”

Posti hiyo ilitoka mara baada ya City kuifunga Burnley 2-1 Wiki iliyopita huko Etihad Stadium kwenye Mechi EPL, Ligi Kuu England, ambayo City walibaki Mtu 10 kuanzia Dakika ya 32 kufuatia Kiungo wao Fernandinho kutolewa kwa Kadi Nyekundu na Refa Lee Mason kufuatia Rafu mbaya.

Sheria za FA zinakataza Posti kwenye Mitandao ya Kijamiii zinazohoji uadilifu wa Marefa.

Sagna, ambae ameomba radhi kuhusu Posti hiyo, amepewa hadi Saa 3 Usiku, Saa za Bongo, Ijumaa Januari 13 kujibu Shitaka lake.

WAKATI HUO HUO, Rufaa ya Nahodha wa Chelsea John Terry kupinga Kadi Nyekundu aliyopewa Jumapili walipocheza na Peterborough kwenye FA CUP imegonga mwamba na sasa atatumikia Kifungo cha Mechi 1.

Adhabu hii itamfanya Terry aikose Mechi ya EPL dhidi ya Mabingwa Watetezi Leicester City hapo Jumamosi.

FA pia imethibitisha Beki wa Middlesbrough, Klabu ya EPL maarufu kama Boro, Daniel Ayala atatumikia Kifungo cha Mechi 3 baada ya Rufaa kupinga Kadi Nyekundu aliyopewa kwenye Mechi ya FA CUP na Sheffield Wednesday Wikiendi iliyopita kutupwa.

NINGEKUWA GEORGE LWANDAMINA…

Na Mwandishi Wetu

received 1116887348410041MOJA kati ya burudani kubwa watakayokutana nayo Wazanzibari kwa mwaka 2017, ni kuutazama mchezo wa kwanza wa ‘Dar es Salaam derby’ ukichezwa katika ardhi yao.
Simba watavaana na Yanga kwenye nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi, ni mchezo wa kikubwa unaohitaji maamuzi ya kikubwa kuuamua.
Mimi ningekuwa kwenye nafasi ya kocha mkuu wa Yanga, George Lwandamina, ningefanya mabadiliko kwenye mambo matatu makubwa ambayo kwa namna moja au nyingine yangeweza kuisaidia Yanga kupata ushindi dhidi ya Simba na kufuta aibu ya kichapo cha bao 4-0 walichokipata mbele ya Azam.
Kwanini Makapu na si Zulu?
Katika michezo michache aliyocheza akiwa na jezi ya Yanga, tayari Justine Zulu ameshaonyesha ni mchezaji wa aina gani.
Ni mtulivu, mbunifu asiye na haraka uwanjani. Anakaba kwenye njia, si kiungo wa kukaba mtu kwa mtu, kitaalamu inaitwa ‘man to man marking’.
Kwa aina yake ya uchezaji si mtu sahihi sana kwenye safu ya kiungo ya Yanga kwenye mchezo dhidi ya Simba. Kwanini? Ipo sababu moja tu ya msingi.
Dakika 90 za pambano la Azam zimetosha kabisa kuuonyesha udhaifu wa Zulu pindi anapokutana na viungo wasumbufu na wenye uwezo mkubwa wa kumiliki mpira.
Kuzidiwa kwa safu ya kiungo, kuliifanya safu ya ulinzi iliyokuwa ikiongozwa na Dante na Yondani kuelemewa na mashambulizi na wakati mwingine kupelekea kufanya makosa mengi yalioigharimu Yanga.
Uwepo wa Makapu utapunguza muda wa viungo wa Simba kukaa na mpira na kutengeneza nafasi, ni hatari zaidi kama utamwachia Muzamir sekunde tano za kukaa na mpira huku akilitazama lango lako.
Yanga wanamhitaji zaidi Makapu kuilinda safu yao ya ulinzi kwa kumnyima uhuru Muzamir, Zulu asubiri kwanza!
Kwanini Kaseke na si Msuva?
Unaweza ukawa umeshtuka hapa, lakini haya ndiyo mabadiliko ambayo ningeyafanya katika kikosi cha Yanga, kwanini Msuva hastahili kuanza kwenye pambano hili?
Kwanza Lwandamina anatakiwa afahamu presha waliyonayo Yanga kwenye pambano hili, ushindi dhidi ya Simba ni muhimu zaidi ya Kombe la Mapinduzi.
Ili kuikwepa presha ya mchezo huu unatakiwa kuwa na wachezaji wenye uwezo mkubwa wa kuhimili presha ya matokeo, rekodi ya Msuva dhidi ya Simba inafahamika.
Kwa faida yake na timu, Msuva si mtu sahihi kwa kuanza pambano hili. Hii ni sababu ya kwanza, ya pili ipo kiufundi zaidi.
Ni kama Yanga wameshazoeleka kimfumo na ni rahisi mno kupambana nao kwa kuwa kila kocha anajua kuwa uimara wao uko kwenye wingi za pembeni.
Unaweza kuwavuruga Simba kwa kumweka nje Msuva na kumpanga Kaseke ukiwa na mbinu nyingine ya kimchezo, mbinu gani? Tulia nikwambie.
Kwa kuitazama Simba, uimara wao umejengwa kupitia wachezaji wawili kwenye safu yao ya kiungo. Jonas Mkude na Muzamir Yassin.
Mkude ndiye anayetengeneza mashambulizi ya Simba kutoka nyuma na Muzamir ndiye anayemaliza kazi kwa kupiga asisti ya mwisho au kufunga, unahitaji kuwa na wachezaji wawili kuwapoteza watu hawa.
Muzamir tayari atakuwa kazini na Makapu na si mbaya ukampanga Kaseke kudili na Jonas Mkude, kuna faida inaweza kupatikana hapa, kivipi? Mfumo wangu utaeleza zaidi.
Kwanini 4-2-3-1?
Golini bado ningemweka Deogratius Munishi ‘Dida’, watu wanne wa nyuma ningeweka wale wale, Juma Abdul, Mwinyi Haji, Dante na Kelvin Yondani.
Viungo wawili wa kati, ningewapanga Makapu na Deus Kaseke, watatu wa mbele kidogo ningewasimamisha Haruna Niyonzima (akicheza kutoka upande wa kulia), Kamusoko na Donald Ngoma (akishambulia kutoka kushoto), mbele angesimama Amissi Tambwe.
Nini nategemea kwenye mfumo huu? Kwanza Lwandamina anatakiwa aamini kuwa Kamusoko si mkabaji, ni kiungo mchezeshaji anayetakiwa kuwa huru katikati ya uwanja.
Ukimpanga pamoja na Haruna ni lazima uhakikishe una watu wawili wenye mapafu ya mbwa kuusaka mpira, hapa ndipo ninapoiona faida ya Kaseke kwenye mfumo huu.
Kazi ya Kaseke ni kuhakikisha Mkude hapati nafasi ya kutulia na mpira na Makapu kazi yake ni kumpoteza Muzamir dimbani.
Ukimpoteza Mkude na Muzamir na ukamuweka Ngoma upande wa kushoto, ni wazi utaiua nguvu ya Simba katikati na upande wa kulia.
Omog amekuwa na tabia ya kumpanga Shiza Kichuya upande wa kulia, faida ya Kichuya ipo pale timu inaposhambulia lakini si mtu mwenye uwezo wa kushuka na kumsaidia Bukungu.
Ngoma akicheza kutoka kushoto, bila shaka utaua safari za Bukungu na utamfanya Abdi Banda kutumia muda mwingi pembeni ya uwanja.
Banda akisogea kushoto ni faida kwa Tambwe atakayesalia katikati na Method Mwanjali. 
Upande wa kushoto, Niyonzima atakuwa na Tshabalala. 
Unaijua faida ya Niyonzima upande huo? Kumzidi Tshabalala hutakiwi kuwa na mbio, asilimia 90 ya uchezaji wao inatakiwa iwe akili na nguvu.
Niyonzima atamfanya Tshabalala awe naye kwa makini zaidi na kutoa mwanya kwa Juma Abdul kucheza kwa urahisi na winga wa Simba, yoyote yule atakayepangwa, iwe Mo Ibrahim au Pastory Athanas, wote ni watu ambao Juma ana uwezo wa kucheza nao ‘one against one situation.’