HERRERA AZOA TUZO YA SIR MATT BUSBY, NDIE BORA MAN UNITED 2016/17!

>GOLI BORA MKHITARYAN, KIJANA BORA ANGEL GOMES!

MANUNITED-HERRERA-BORA1Ander Herrera ametwaa Tuzo ya Sir Matt Busby inayoashiria yeye ndio Mchezaji Bora wa Mwaka wa Klabu ya Manchester United.

Herrera, ambae yuko kwenye Msimu wa 3 na Man United, aliwabwaga Antonio Valencia na Zlatan Ibrahimovic kwenye Kura zilizopigwa akizoa Kura 242 zaidi ya Valencia alieshika Namba 2.

Herrera, ambae amecheza Mechi 49 Msimu huu, ni Kiungo Mpiganaji aliekonga mioyo ya Mashabiki wengi kwa mtindo wake wa Uchezaji wa ‘Hapa Kazi Tu’!

Kiungo huyo, alieanza kuichezea Timu ya Taifa ya Kwanza ya Spain Novemba Mwaka Jana, anarithi Taji hili kutoka kwa Kipa David De Gea ambae ameshinda Tuzo hii mfululizo kwa Miaka Mitatu iliyopita.

+++++++++++++++

JE WAJUA?

-Sir Matt Busby alikuwa ni Meneja wa zamani wa Manchester United alietumikia Vipindi Viwili vya 1945 hadi 1969 na kile cha 1970 hadi 1971.

-Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Man United ilibatizwa Jina la Sir Matt busby Mwaka 1996 kufuatia Kifo cha Meneja huyo Mwaka 1994.

-Tuzo yenyewe ni Mfano wa Sanamu ileile kubwa iliyosimikwa nje ya Uwanja wa Old Trafford upande wa Mashariki.

+++++++++++++++

Akiongea mara baada ya kupokea Tuzo yake kwenye Sherehe iliyofanyika Old Trafford Jana Usiku, Herrera alinena: “Ni kitu speshoMANUNITED-MKHITARYAN-GOLIBORA kushinda Tuzo hii hasa ukitazama Washindi wa Tuzo hii na hilo linakufanya ujue umuhimu wake. Na sasa nimesimamisha Rekodi ya David De Gea!”

Akaongeza: “Nahisi mapenzi ya Mashabiki na nawashukuru sana lakini nadhani Mchezaji wa Manchester United hasimami, lazima tuonyeshe upendo kwa Mashabiki kwani si Siku zote tunacheza vizuri lakini wanatupenda tu!”

De Gea, ambae ni Rafiki wa karibu wa Herrera ambae alikuwepo Stejeni, alieleza: “Yeye ni Mtu wa juu na ni Rafiki. Yeye ni Mchezaji anaecheza kwa Moyo wote Uwanjani na ni Mchezaji mzuri!”

Kwenye Tuzo nyingine, Henrikh Mkhitaryan alitunukiwa ile ya Goli Bora la Msimu kwa lile ‘Goli la N’nge’ alilofunga 26 Desemba 2016 Man United walipoipiga Sunderland 3-1.

Kijana Angel Gomes, anaechezea Kikosi cha U-18, kubeba ile ya Kijana Bora wa Mwaka.

MAN UNITED – TUZO MCHEZAJI BORA WA MWAKA -Washindi waliopita Miaka ya hivi karibuni:

MSIMU

MCHEZAJI

UTAIFA

2000–01

Teddy Sheringham

England

2001–02

Ruud van Nistelrooy

Netherlands

2002–03

Ruud van Nistelrooy

Netherlands

2003–04

Cristiano Ronaldo

Portugal

2004–05

Gabriel Heinze

Argentina

2005–06

Wayne Rooney

England

2006–07

Cristiano Ronaldo

Portugal

2007–08

Cristiano Ronaldo

Portugal

2008–09

Nemanja Vidić

Serbia

2009–10

Wayne Rooney

England

2010–11

Javier Hernández

Mexico

2011–12

Antonio Valencia

Ecuador

2012–13

Robin van Persie

Netherlands

2013–14

David de Gea

Spain

2014–15

David de Gea

Spain

2015–16

David de Gea

Spain

2016–17

Ander Herrera

Spain

 

ZABALETA AAGWA CITY, CARRICK KUBAKI OLD TRAFFORD!

MANUNITED-CARRICK-ABEBA-FACUPWAKATI Manchester City Jana wakimuaga Beki wao mkongwe Pablo Zabaleta amvae anaondoka Klabuni mwishoni.mwa Msimu, habari kutoka huko Manchester United zimesema kuwa Kiungo wao Mkongwe Michael Carrick ataongezwa Mkataba wa Mwaka Mmoja ili abaki kwa Msimu ujao.
Jana huko Etihad, Pablo Zabaleta aliagwa kwa kishindo wakati City inaichapa West Brom 3-1 katika Mechi ya EPL, LIGI KUU ENGLAND.
Zabaleta, Mchezaji mwenye Miaka 32 kutoka Argentina, ameitumikia City kwa Miaka 9 na Jana aliingizwa kucheza Dakika ya 62 na kukaribishwa kwa shangwe.
Zabaleta ndie alieteuliwa Mchezaji Bora wa Mechi hiyo aliyoimaliza kama Kepteni baada kukabidhiwa Utepe wa Nahodha kutoka kwa Kepteni Vincent Kompany ambae alipumzishwa.
Mara baada ya Mechi kwisha, Zabaleta, ambae ni Mchezaji wa 3 kwa Utumishi wa muda mrefu nyuma ya Joe Hart na Kompany, alitoa Hotuba akiwa Uwanjani pamoja na Mkewe na Mwanawe na kisha kusindikizwa na Gwaride la Heshima la Wachezaji wenzake.
HUKO Old Trafford, zipo habari kuwa Kiungo Michael Carrick yuko mbioni kuongezewa Mkataba ili abaki kwa Mwaka Mmoja zaidi.
Carrick, mwenye Miaka 35, anatimiza Misimu 11 hapo Man United na Juni ipo Mechi Maalum ya kuuenzi Utumishi wake uliotukuka.
Carrick alijiunga Man United kutoka Tottenham Mwaka 2006 kwa Dau la Pauni Milioni 18.6.
Tangu wakati huo, Carrick ameichezea Man United Mechi 457 akifunga Goli 24 na yeye ni Namba 17 kwenye Listi ya Wachezaji waliotumikia muda mrefu.
Kwenye utumishi wake na Man United, Cartick, ambae pia alikuwa Mchezaji wa Kimataifa wa England, alitwaa Ubingwa wa England mara 5, UEFA CHAMPIONZ LIGI, FA CUP na Kombe la Ligi mara 2.

UEFA EUROPA LIGI-FAINALI MAN UNITED NA AJAX REFA NI YULE ALIEPONDWA NA MOURINHO!!

>MGAO TIKETI KILA TIMU 9,500 TU!

REFA-SKOMINAUEFA Leo imemtangaza Refa kutoka Slovenia Damir Skomina kuwa ndie atachezesha Fainali ya 2017 ya UEFA EUROPA LIGI kati ya Ajax Amsterdam na Manchester United itakayochezwa huko Stockholm, Sweden hapo Mei 24.

Uteuzi huu huenda usimfurahishe Meneja wa Man United Jose Mourinho kwani aliwahi kumbatukia Refa huyo na kumwita ‘dhaifu’ na ‘asiejua kitu’ baada ya Refa huyo ‘kuidhulumu’ Chelsea Penati ya wazi Mwaka 2015 walipocheza na Dynamo Kiev.

Refa Skomina pia ashawahi kuichezesha Man United Mwaka 2012 Uwanjani Old Trafford walipofungwa 2-1 na Ajax kwenye Mechi ya EUROPA LIGI lakini wakasonga kwa Jumla ya Mabao 3-2.

TIKETI ZA FAINALI

Wakati huo huo, UEFA pia imetangaza mgao wa Tiketi za Fainali hii ambapo Manchester United will receive no more thanitapa si zaidi ya Tiketi 9,500 kwa Washabiki wake idadi ambayo Ajax pia watapewa.

Fainali hii itachezwa Uwanja wa Friends Arena Mjini Stockholm unaopakia Watu 50,000.

Idadi ya Tiketi zilizobaki zitauzwa Mtandaoni kwa Washabiki huko Sweden, Vyama vya Soka vya Nchi husika, Washirika wa Kibiashara wa UEFA, Watangazi wa TV/Radio wa Mechi hiyo na Kampuini maalum za kuhudumia Wateja.

UEFA EUROPA LIGI

FAINALI

24 Mei 2017: Friends Arena, Solna, Sweden

Ajax Amsterdam v Manchester United

FIFA -UCHUNGUZI UHAMISHO WA PAUL POGBA, NINI UNDANI WAKE?

MANUNITED-POGBA-RAIOLA

JUZI kuliibuka stori kuwa Uhamisho wa Rekodi ya Dunia wa Dau la Pauni Milioni 89.3 wa Paul Pogba kutoka Juventus kwenda Manchester United Mwezi Agosti Mwaka Jana unachunguzwa na FIFA.

Ingawa FIFA wamesisitiza kuwa huu si uchunguzi rasmi licha kutaka maelezo zaidi toka kwa Vilabu vilivyohusika.

Lakini hatua hiyo imeshangaza kwani FIFA hao hao ndio wanaobariki Uhamisho wa Wachezaji Kimataifa kupitia Mfumo wao wa International Transfer Matching System (ITMS) ambao huhitaji taarifa zaidi ya 20 zikiwemo aina ya Uhamisho, Mawakala wanaohusika, Ulipwaji wa Ada zote na namna zitakavyolipwa.

Baada ya hayo kutimizwa FIFA hutoa Kibali na hilo ndilo lililofanywa kwenye Uhamisho wa Pogba na hivyo ndivyo ambavyo Klabu ya Manchester United ilivyoijibu FIFA kwamba hawana cha ziada mbali yay ale yaliyokuwemo kwenye ITMS.

Man United ilipewa Cheti cha Uhamisho wa Kimataifa, ITC International Transfer Certificate, mara baada ya kukamilisha taratibu zote za Uhamisho wa Pogba kupitia Mfumo wa ITMS.

Lipi limejiri mpaka sasa FIFA kutaka Taarifa zaidi?

Mpaka sasa haijulikani kwanini FIFA wameibua haya kwa wakati huu.

Lakini Wachambuzi wanahisi kuwa hilo limetokana na kuchapishwa kwa Kitabu huko Germany Wiki hii, kiitwacho The Football Leaks: The Dirty Business of Football, ambacho, miongoni mwa kulipua mengi nyuma ya pazia kuhusu Soka, pia kiligusia ada kubwa mno aliyolipwa Wakala wa Pogba, Mino Raiola, kiasi cha kudaiwa kuvunja Kanuni za FIFA za Uhamisho wa Wachezaji.

YAVUMAYO: MAN UNITED YAANDAA £40M KWA DIER, CITY YAWEKA CHAMBO CHA SANCHEZ!

ERIC DIERWAKATI EPL, LIGI KUU ENGLAND, ikielekea ukingoni tetesi zimezagaa kuhusu Uhamisho wa Wachezaji huku ikisemwa kuwa Manchester United wapo tayari kulitoa Dau la Pauni Milioni 40 ili kumnunua Kiungo wa Tottenham Eric Dier.

Lakini unumuzi huo huenda ukakumbana na pingamizi la Mwenyekiti wa Spurs, Daniel Levy, ambae ameshasema hauzi Staa yake yoyote mkubwa wa Kikosi chao.

Meneja wa Man United Jose Mourinho anamtaka Dier awe mrithi wa Michael Carrick ambae Umri umeanza kumtupa mkono.

Dier, mwenye Miaka 23, huenda akavutika kwenda Man United kutokana na Mshahara mkubwa kwani hivi sasa analipwa Pauni 50,000 kwa Wiki.

Man City kumtoa Denayer chambo ili kumnasa Sanchez!

Manchester City wanatarajia kumnasa Alexis Sanchez kutoka Arsenal huku pia wakimtoa Jason Denayer kwenda Arsenal ili kuwa kivutio.

City wapo tayari kuilipa Arsenal Pauni Milioni 50 nankuwapa Denayar juu yake.

Sanchez amehusishwa nabkuhamia Klabu za Juventus, PSG, Chelsea na Bayern Munich.

Pep Guardiola, Meneja wa City, anataka sana kuungana na Sanchez ambae walikuwa wote huko Barcelona.

Everton kusaini Wawili kwa mpigo!

Meneja wa Everton Ronald Koeman amepania kumsaini Straija wa Malaga Sandro Ramirez na Kiungo wa Ajax Davy Klaassen kwa ajili ya Msimu ujao.

Dau la kumnunua Sandro Ramirez, mwenye Miaka 21, ni dogo na linakadiriwa kuwa Pauni Milioni 5.

Nae Klaassen, mwenye umri wa Miaka 24, anakadiriwa kugharimu Pauni Milioni 20.