CHELSEA TUZO: HAZARD NDIE BORA, KANTE 'MCHEZAJI WA WACHEZAJI'!

CHELSEA-TUZOKIUNGO wa Chelsea Eden Hazard ameteuliwa kuwa ndie Mchezaji Bora wa Mwaka na N'Golo Kante kutwaa Tuzo ya 'Mchezaji wa Wachezaji' katika Hafla maalum ya kugawa Tuzo za Mabingwa Wapya wa England Chelsea zilizofanyika Jana Usiku Jijini London.
Mbali ya Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mabingwa hao, pia Hazard alizoa Tuzo ya Goli Bora la Msimu kwa Goli lake alilofunga Februari 4 kwa juhudi binafsi dhidi ya Arsenal.
Pia, Kepteni wa Chelsea, John Terry, ambae ndie anastaafu hivi sasa baada kuitumikia Chelsea kwa Miaka 22, amepewa Tuzo maalum kwa Utumishi wake.
Meneja wa Mabingwa hao Antonio Conte ndie aliekabidhi Tuzo hizo ambazo Washindi wake walipatikana kwa Kura za Washabiki.
Mbali ya Mshindi Hazard, Wagombea wengine wa Tuzo ya Mchezaji Bora walikuwa Cesar Azpilicueta, David Luiz na Kante.
CHELSEA - Washindi wa Tuzo:
GOLI LA MSIMU: Eden Hazard
MCHEZAJI WA WACHEZAJI: N'Golo Kante
MCHEZAJI BORA KINAMAMA: Karen Carney
MCHEZAJI BORA CHUONI: Mason Mount
MCHEZAJI BORA WA MWAKA: Eden Hazard
TUZO MAALUM: John Terry

MAN CITY YAWAACHA GAEL CLICHY, BACARY SAGNA, JESUS NAVAS NA WILLY CABALLERO!

CITY-PEP-6Gael Clichy, Bacary Sagna, Jesus Navas na Willy Caballero wanaondoka Manchester City baada ya Mikataba yao kumalizika.

Wachezaji hao hawakupewa Mikataba Mipya.

Clichy, Fulbeki wa Kushoto, ameichezea City zaidi ya Mechi 200 tangu ajiunge nao Mwaka 2011 akitokea Arsenal na Mwaka 2012 alikuwemo Kikosini walipotwaa Ubingwa wa England kwa mara ya kwanza baada Miaka 44.

Fulbeki wa Kulia, Bacary Sagna, alijiunga na City Mwaka 2014 akitokea Arsenal na kuichezea Mechi 85.

Winga Navas, aliejiunga kutoka Sevilla Mwaka2013, alitwaa Ubingwa wa England akiwa na City Mwaka 2014 na kuanza Mechi 117.

Kipa Caballero amechuza Mechi 48 na kati ya hizo 27 chini ya Meneja Pep Guardiolla Msimu huu.

City haijatangaza akina nani Wapya watakuja kuziba mapengo hayo ingawa sasa inaonyesha Wamiliki Matajiri wa City wanataka Guardiolla asuke upya Kikosi chao.

LAURENT KOSCIELNY ‘JELA’, KUIKOSA FAINALI YA FA CUP ARSENAL-CHELSEA JUMAMOSI!

>SASA DIFENSI ARSENAL YAPARAGANYIKA, GABRIEL, MUSTAFI ‘GONJWA’!

ARSENAL-KOSCIELNY-REDLaurent Koscielny ataikosa Mechi ya Fainali ya FA CUP ya Timu yake Arsenal ambao watacheza na Mabingwa Wapya wa England Chelsea Jumamosi Uwanjani Wembley Jijini London.

Leo, FA, Chama cha Soka England, kimethibitisha kuwa Rufaa ya Arsenal ya kupinga kufungiwa Mechi 3 kwa Beki wao huyo imetupwa.

Koscielny alitolewa nje kwa Kadi Nyekundu Jumapili iliyopita Uwanjani Emirates baada kumchezea Rafu mbaya Enner Valencia wakati wa Mechi yao ya mwisho ya Msimu wa EPL, LIGI KUU ENGLAND, walipoitwanga Everton 3-1.

Arsenal walikata Rufaa wakidai Rafu hiyo haikustahili Kadi Nyekundu lakini Kamisheni Huru imepitia Rufaa hiyo na kuitupilia mbali.

Sasa Koscielny atatumikia Adhabu ya Kufungiwa Mechi 3 na inaanza mara moja na Mechi ya Kwanza kuikosa ni hiyo Fainali ya FA CUP.

Mechi nyingine ambazo Koscielny atazikosa ni zile mbili za kwanza za Arsenal za Msimu Mpya wa 2017/18 ambao Mechi za EPL zitaanza Agosti 12.

Hili ni pigo kubwa kwa Arsenal kwenye hii Fainali ya FA CUP kwani Koscielny ndie Jabali wa Difensi yao ambayo pia inaweza kuwakosa Mabeki wengine Wawili ambao ni Majeruhi.

Mabeki hao ni Gabriel, ambae alitolewa kwa Machela kwenye Mechi hiyo na Everton, na mwingine ni Shkodran Mustafi aliepata dhoruba Kichwani na kusumbuliwa na kizunguzungu.

FA CUP

Fainali

Wembley Stadium, London

1930 Arsenal v Chelsea

KROENKE – HISA ARSENAL HAZIUZWI! MOYES ATIMKA SUNDERLAND ILIYODONDOKA!

MMILIKI wa Hisa nyingi wa Klabu ya Arsenal Mmarekani Stan Kroenke amesema Hisa za Klabu hiyo ‘si biashara’.

Hivi Juzi, Mrusi Alisher Usmanov, ambae anamiliki Hisa Asilimia 30 dhidi ya 67 za Kroenke, alitoa Ofa ya Pauni Bilioni 1 kununua Hisa za Kroenke.

Leo Kampuni ya Kroenke, Sports and Entertainment, imetoa tamko kwamba wao ni Wawekezaji wa muda mrefu na watabaki hivyo hivyo.

Wakati Kroenke anaketi kwenye Bodi ya Klabu ya Arsenal, Usmanov si memba wa Bodi hiyo na hivyo hahusiki lolote na maamuzi ya Klabu hiyo na hilo linamkera mno.

SUNDERLAND-MOYESJuzi, Usmanov alibatuka na kudai Kroenke na Bodi wanawajibika kwa Arsenal kukosa mafanikio.

Msimu huu, Arsenal imemaliza Nafasi ya 5 kwenye EPL, LIGI KUU ENGLAND, na hivyo kukosa kushiriki UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao ikiwa ni mara yao ya kwanza katika Miaka 20 na badala yake watacheza UEFA EUROPA LIGI.

Jumamosi hii Arsenal wako Wembley Jijini London kuwavaa Mabingwa Wapya wa England Chelsea katika Fainali ya FA CUP.

DAVID MOYES AJIUZULU UMENEJA SUNDERLAND BAADA KUSHUSHWA DARAJA!

MENEJA wa Sunderland David Moyes amejiuzulu kufuatia Klabu hiyo kushushwa Daraja kutoka EPL, LIGI KUU ENGLAND.

Moyes, mwenye Miaka 54, alimjulisha Mwenyekiti wa Sunderland Ellis Short kuhusu uamuzi wake hii Leo.

Meneja huyo, ambae aliwahi kuwa na Klabu za Everton na Manchester United, alishika wadhifa wa Umeneja hapo Sunderland Julai Mwaka Jana mara baada ya Sam Allardyce kuondoka ili kuwa Meneja wa Timu ya Taifa ya England.