LEO NI SUPERCLÁSICO – NI BRAZIL BILA NEYMAR V ARGENTINA YENYE MESSI!

LEO, Saa 7 Dakika 5 Mchana, Saa za Bongo, Watani wa Jadi toka Marekani ya Kusini, Brazil na Argentina, wanapambana kwenye Mechi ya Kirafiki huko Melbourne Cricket Ground Nchini Australia.

BRAZIL-ARGENTINAMechi kati ya Nchi hizi hubatizwa Jina ‘Superclasico de las Americas’.

Mechi hii ni ya Kirafiki, tena Brazil itacheza bila Staa wao mkubwa Neymar ambae amepewa Mapumziko, lakini imeleta mvuto mkubwa Duniani na hasa Wadau wakitaka kuiona Argentina chini ya Kocha Mpya Jorge Sampaoli itafanya nini.

Mara ya mwisho kwa Timu hizi kukutana ni Novemba huko Belo Horizonte Nchini Brazil kwenye ya Kundi la Nchi za Marekani ya Kusini kusaka kufuzu Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 na Brazil kuinyuka Argentina 3-0 kwa Bao za Coutinho, Neymar na Paulinho.

Ili kuikabili nguvu ya Brazil inayocheza Kitimu zaidi, Kocha Sampaoli, ambae ametokea kuzifundisha Timu ya Taifa ya Chile na Klabu ya Spain Sevilla, amebuni Mfumo Mpya kabisa wa 3-4-3 kwa Argentina huku akitumia Mtu 3 za Fowadi Lionel Messi, Paulo Dybala na Gonzalo Higuain.

Sampaoli amesisitiza Mfumo huo, hasa Wachambuzi wanadai ni 3-4-2-1, utamfungua Staa wao mkubwa Lionel Messi na kumpa uhuru kuhaha mbele Uwanja mzima.

Sampaoli amenena: “Lazima Argentina tutafute kitu kinachofanana na Staili ya Barcelona ili Messi acheze vizuri!”BRAZIL-ARGENTINA-6-ZILIZOPITA

Hii ni Mechi ya kwanza kwa Sampaoli baada ya kumrithi Edgardo Bauza aliefukuzwa Mwezi Aprili baada Argentina kunyukwa 2-0 na Bolivia na kuachwa wapo Nafasi ya 5 kwenye Kanda ya Nchi za Marekani ya Kusini kusaka kufuzu Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huku wakibakisha Mechi 4 tu.

Kanda hiyo, ambapo Timu 4 hufuzu moja kwa moja nay a 5 kwenda Mchujo, inaongozwa na Brazil ambao tayari washafuzu Fainali za Kombe la Dunia wakiwa na Mechi 4 mkononi.

Kwa upande wa Brazil chini ya Kocha Tite ambae mambo yake ni burdani tangu atwae wadhifa, wameamua kuwapumzisha Wachezaji wao kadhaa wakiwemo Neymar, Fowadi wa Liverpool Roberto Firmino, na Mabeki Dani Alves, Marcelo na Marquinhos.

Lakini Kikosini wamo Wachezaji Wawili wa Chelsea, David Luiz na Willian, Wawili wa Man City, Fernandinho na Gabriel Jesus, pamoja na Fowadi wa Liverpool Philippe Coutinho.

Kipa Mpya Ederson, aliesainiwa kutoka Benfica Jana Alhamisi, ataikosa Mechi hii baada kuruhusiwa kutoka Kambini kuhudhuria kuzaliwa kwa Binti yake.

VIKOSI VILIVYOTEULIWA AWALI:

BRAZIL

Makipa: Diego Alves (Valencia), Weverton (Atletico Paranaense), Ederson (Benfica/Man City)
Mabeki: Alex Sandro (Juventus), David Luiz (Chelsea), Fagner (Corinthians), Filipe Luis (Atletico Madrid), Gil (Shandong Luneng), Jemerson (Monaco), Rafinha (Bayern Munich), Rodrigo Caio (Sao Paulo), Thiago Silva (Paris Saint-Germain)
Viungo: Fernandinho (Manchester City), Giuliano (Zenit St Petersburg), Lucas Lima (Santos), Paulinho (Guangzhou Evergrande), Philippe Coutinho (Liverpool), Renato Augusto (Beijing Gouan), Rodriguinho (Corinthians), Willian (Chelsea)
Mafowadi: Diego Souza (Sport), Douglas Costa (Bayern Munich), Gabriel Jesus (Manchester City), Taison (Shakhtar Donetsk)

ARGENTINA

Makipa: Sergio Romero (Manchester United), Nahuel Guzman (Tigres), Geronimo Rulli (Real Sociedad)

Mabeki: Javier Mascherano (Barcelona), Emanuel Mammana (Lyon), Gabriel Mercado (Sevilla), Nicolas Otamendi (Manchester City)
Viungo: Eduaro Salvio (Benfica), Lucas Rodrigo Biglia (Lazio), Ever Banega (Inter Milan), Manuel Lanzini (West Ham United), Leandro Paredes (Roma), Guido Rodriguez (Tijuana)
Mafowadi: Leo Messi (Barcelona), Gonzalo Higuain (Juventus), Joaquin Correa (Sevilla), Alejandro Dario Gomez (Atalanta), Mauro Icardi (Inter Milan), Angel Di Maria (Paris Saint-Germain), Paulo Dybala (Juventus)

REAL YAIGOMEA OFA YA MAN UNITED KWA ALVARO MORATA!

OFA ya Manchester United kumnunua Straika wa Real Madrid Alvaro Morata kwa Dau la Pauni Milioni 52.4 imekataliwa na Mabingwa hao wa Spain na Ulaya.

Kwa mujibu wa Sky Sports TV, Ofa hiyo haikumjumuisha Kipa wa Man United David de Gea ambae anatakiwa na Real.
REAL-MORATAIliaminika Dili ni De Gea kwenda Real na Morata kutua Man United ambao pia wangeongezewa pesa juu.
Real wanataka ukimnunua Morata ulipe Pauni Milioni 78.
Morata, mwenye Umri wa Miaka 24 na ambae pia yupo Timu ya Taifa ya Spain, Msimu huu ulioisha Majuzi aliifungia Real Bao 20 na kuisaidia kubeba Ubingwa wa La Liga na UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Habari toka ndani huko Old Trafford zimedai kuwa ikiwa Man United itashindwa kumpata Morata basi watamgeukia Andrea Belotti wa Torino ya Italy ambae Mkataba wake una Kipengele cha Kuuzwa kwa Dau la Pauni Milioni 87.3.
Morata ni Mzawa wa Jiji la Madrid huko Nchini Spain ambae alichipukia kwenye Vyuo vya Soka vya Real na kuibuka kuichezea Timu ya Kwanza Desemba 2010.
Julai 2014 Morata aliuzwa kwa Juventus kwa Pauni Milioni 17.5 na akiwa hapo aliisaidia Juve kutwaa Serie A mara 2, Coppa Italia 2 na pia kuifikisha Fainali ya 2015 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI walipofungwa 3-1 na Barcelona huku yeye akifunga hilo Bao 1.
Juni 2016, Real, wakitumia Kipengele cha Mkataba waliomuuza Morata kwa Juve kinachowapa uhuru wa kumnunua tena, wakailipa Juve Pauni Milioni 26.2 na kumrudisha Mchezaji huyo kwao Jijini Madrid.
 

UEFA SUPER CUP 2017: KUPIGWA AGOSTI 8 KATI YA MABINGWA ULAYA REAL NA MAN UNITED!

BAADA kutwaa UEFA EUROPA LIGI,  Jose Mourinho sasa ataiongoza Timu yake Manchester United kuivaa Timu yake ya zamani Real Madrid kwenye Mechi ya kuanua Msimu Mpya wa Mashindano ya Klabu Ulaya kwa kugombea UEFA SUPERCUP.
PATA YOTE KUHUSU HII UEFA SUPER.CUP:
NANI WAGOMBEA?
UEFA-SUPERCUP17UEFA SUPER CUP hugombewa kila Mwaka na Washindi wa UEFA CHAMPIONZ LIGI na wale wa UEFA EUROPA LIGI.
Jana Real Madrid walibeba UEFA CHAMPIONZ LIGI kwa kuibwaga Juventus 4-1 wakati Man United walibeba UEFA EUROPA LIGI kwa kuifunga Ajax Amsterdam 2-0.
Msimu uliopita Real walibeba UEFA SUPER CUP kwa kuitoa Sevilla kwa Bao.la Beki wao Dani Carvajal kwenye Dakika za mwisho za Muda wa Nyongeza.
Real walicheza Fainali hiyo kwa kutwaa UEFA CHAMPIONZ LIGI na Sevilla walibeba UEFA EUROPA LIGI.
ITACHEZWA LINI?
UEFA SUPER itachezwa Jumanne Agosti 8.
ITACHEZWA WAPI?
Uwanja wa Fainali hii ni National Arena (Philip II Arena) Mjini Skopje Nchini Macedonia.
Ni Uwanja ambao unachukua Watazamaji 33,000 na hutumiwa na Klabu za FK Vardar na FK Rabotnički kama Uwanja wa Nyumbani.
Nchi hii inapakana na Nchi 4 ambazo bazo ni Greece, Albania, Bulgaria na Serbia. 
Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Macedonia kuwa Mwenyeji wa Fainali kubwa ya Ulaya.
USHINDI ULIOPITA
Previous form?
Man United, chini ya Meneja Sir Alex Ferguson walitwaa UEFA SUPER Cup Mwaka 1991 walipowabwaga waliokuwa Mabingwa wa Ulaya Red Star Belgrade kwa Bao la Brian McClair.
Man United pia waligombe hili Mwaka 1999 na 2008 na kufungwa na Lazio Zenit Saint Peterburg.
 

MANCHESTER UNITED NDIO KLABU YENYE THAMANI KUBWA ULAYA – KPMG!

OLD-TRAFFORD-12Manchester United ndio Klabu yenye Thamani kubwa Ulaya kwa mujibu wa Takwimu zilizotolewa na Magwiji wa Biashara, KPMG.

Utafiti wa KPMG umeonyesha Man United, ambao ni Mabingwa wa UEFA EUROPA LIGI, wapo mbele ya Klabu Vigogo za Spain, Real Madrid na Barcelona wakiwa na Thamani ya Euro Bilioni 3.09.

Utafiti huo ulichunguza Haki za Matangazo na Mapato yatokanyo, Faida, Umaarufu, Uwezo Kimichezo na Umiliki wa Viwanja.

Utafiti huo ulipitia Mahesabu ya Klabu 32 huko Ulaya na 6 kati ya zile 10 Bora zinatoka England.

Mahesabu yaliyopitiwa ni yale ya Misimu ya 2014/15 na 2015/16.

Mkuu wa Michezo wa KPMG, Andrea Sartori, ambae ndie Mwandishi wa Ripoti ya Utafiti huu, amesema Kibiashara Sekta ya Soka imekua mno kwa Mwaka Mmoja uliopita.

Kuhusu Haki za Matangazo, Sartori amesema England inaongoza kwa mbali mno kwenye Mapato ya eneo hili.

+++++++++++++++++++++

10 BORA kwa Thamani Ulaya:

Manchester United – Euro Bilioni 3.09

Real Madrid - 2.97

Barcelona - 2.76

Bayern Munich - 2.44

Manchester City - 1.97

Arsenal - 1.95

Chelsea - 1.59

Liverpool - 1.33

Juventus - 1.21

Tottenham - 1.01

**Chanzo: KPMG

+++++++++++++++++++++

Kwa mujibu wa KPMG, Mwaka huu Klabu 10 zimewezwa kuvuka Thamani ya Euro Bilioni 1 huku Tottenham Hotspur na Juventus zikitinga 10 Bora kwa mara ya kwanza.

Tottenham imeing’oa Klabu ya France Paris Saint-Germain kutoka Nafasi ya 10 na kukaa wao.

Licha ya England kuwa na Klabu 6 kwenye 10 Bora, Spain ndio Nchi pekee yenye Klabu 2 zenye Thamani ya Zaidi ya Euro Bilioni 2.

KIPA, STRAIKA WA CHELSEA KUSAINI BOURNEMOUTH NA LIVERPOOL!

>MAHREZ ADAI KUHAMA LEICESTER!

MAHREZ-KUNGOKASASA ni kile kipindi kitamu cha gumzo, uvumi na tetesi wakati Msimu wa EPL, LIGI KUU ENGLAND, ukiwa umeisha na Timu kujiandaa kwa Msimu mpya wa 2017/18 unaoanza Agosti 12 kwa harakati za kubadili na kuimarisha Vikosi vyao.

Ni wakati wa kupata Habari Mpya kila kukicha!

PATA MPYA ZA LEO!

BOURNEMOUTH YAMSAINI KIPA WA CHELSEA!

Bournemouth imemsaini Kipa Asmir Begovic kutoka kwa Mabingwa Wapya wa England, Chelsea, kwa Ada ambayo haikutajwa.

Begovic, mwenye Miaka 28 na Raia wa Bosnia-Herzegovina, amesaini ‘Mkataba wa Muda Mrefu’ na Bournemouth kama habari zilivyochomoza hii Leo zinavyodai ikiwa ni Miaka 10 tangu aliposaini na Klabu hiyo kwa Mkopo.

Kipa huyo alinunuliwa na Chelsea Julai 2015 kutoka Stoke City na kuanza Mechi 17 tu katika Misimu Miwili na Mabingwa hao huku Msimu huu akianza Mechi 2 tu.

Akiongelea kuhusu Uhamisho huu, Begovic amenena: “Nimefikia hatua muhimu ya Maisha yangu ya Soka. Nataka sasa kuonyesha uwezo wangu!”

LIVERPOOL KUMSAINI STRAIKA WA CHELSEA!

Nao Liverpool wapo njiani kumsaini Straika Tineja kutoka Chelsea, Dominic Solanke, ambae ameshindwa kuafikiana na Mabingwa hao kuhusu Mkataba Mpya.

Ada ya Uhamisho wa Kijana huyo wa Miaka 19 itabidi iamuliwe na Tume Maalum ya Masuala kama haya yanayohusu Uhamisho wa Vijana lakini inaaminika Liverpool watapaswa kulipa kiasi kisichopungua Pauni Milioni 3.

Solanke, kwa sasa yuko huko South Korea na Kikosi cha England U-20 wakicheza Fainali za Kombe la Dunia za Vijana U-20.

Kijana huyu amewahi kuichezea Timu ya Kwanza ya Chelsea mara 1 tu na Msimu wa 2015/16 alipelekwa kwa Mkopo huko Holland kuichezea Vitesse Arnhem ambako alifunga Bao 7 katika Mechi 25.

Hivi sasa Liverpool wapo kwenye Kifungo cha Miaka Miwili kinachowabana kusaini Vijana Chipukizi kutoka Klabu nyingine za England lakini kwa vile Solanke amevuka Miaka 17 Adhabu hiyo haihusu Uhamisho wake.

Solanke anatarajiwa kuwa Mchezaji rasmi wa Liverpool hapo Julai 1.

MAHREZ ADAI KUHAMA LEICESTER!

FOWADI wa Leicester City Riyad Mahrez ametangaza anataka kuihama Klabu hiyo.

Mahrez, Raia wa Algeria mwenye Miaka 26, alijiunga na Leicester Mwaka 2014 kutoka Klabu ya France Le Havre kwa Dau la Pauni 400,000, amedai alibaki Leicester baada ya kuwasaidia kuwapa Ubingwa na kucheza Msimu uliopita baada ya kukubaliana na Mwenyekiti wa Klabu.

Leo amesisitiza sasa ni wakati muafaka kuhama kwa sababu ana ari kubwa kupata mafanikio kwingineko.

Msimu huu, Mahrez, ambae alizoa Tuzo ya Mchezaji Bora wa ya 2016 ya PFA, Chama Cha Wachezaji Soka wa Kulipwa, ameichezea Leicester Mechi 48 na kufunga Bao 10 na kutoa msaada wa Mabao mara 7 akiisaidia Leicester kuamka toka Nafasi za chini na kumaliza EPL, LIGI KUU ENGLAND, Nafasi ya 12 na pia kufikia Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.