RAFAEL AAGA MAN UNITED: ‘ASANTE SIR ALEX!’

SIRALEX-RAFAELBEKI kutoka Brazil Rafael amethibitisha kuihama Manchester United lakini hakusita kutoa shukrani kwa Mashabiki wa Klabu hiyo na Meneja wake wa zamani Sir Alex Ferguson kwa kumjalia mengi katika Miaka yake 8 huko Old Trafford.

Rafael, mwenye Miaka 25, alijiunga na Man United akiwa na Nduguye Pacha mwenzake Fabio kutoka Klabu ya Fluminense ya Brazil tangu Januari 2007 chini ya himaya ya Sir Alex Ferguson lakini Fabio akauzwa kwa Cardiff City Januari 2014.

Mapema Jumatatu, Rais wa Lyon ya France, Jean-Michel Aulas, alieleza kuwa Rafael yuko France kukamilisha Uhamisho wake baada ya kutemwa na Meneja wa Manchester United Louis van Gaal ambae hata hakumchukua kwenye Ziara ya Timu huko USA iliyokamilika hivi Juzi.

Msimu uliopita, Rafael alicheza Mechi 11 tu chini ya Louis van Gaal lakini hilo halikumfanya Mbrazil huyo kutoishukuru Man United na hasa Sir Alex Ferguson kwa kumwendeleza.

Alinena: “Ni bahati kubwa kuichezea Klabu kubwa kabisa Duniani. Asante Mashabiki na Wafanyakazi wote wa Klabu. Asante Sir Alex Ferguson kwa Siku zote kuamini kazi yangu na kufungua Milango yote kwangu mimi!”

RAFA-FABIO

VAN GAAL AOSHA MIKONO KWA DE GEA, DI MARIA, AITAKA BODI KUWAUZA HARAKA!

LVG-AONGEALVG-AONGEAHUKU kukiwa na ripoti kuwa Angel Di Maria atapimwa afya yake Klabuni Paris Saint-Germain ndani ya Masaa 24 yajayo, Meneja wa Manchester United Louis van Gaal amedaiwa kuitaka Bodi ya Klabu kuwauza haraka Muargentina huyo pamoja na Kipa David De Gea.
Inaaminika Man United imemruhusu Di Maria kuongea na PSG ili kuafikiana maslahi yake binafsi baada ya Klabu hizo mbili kuafikiana Dau la Uhamisho linalosemekana kuwa Pauni Milioni 44.3.
Man United ilimnunua Di Maria mwanzoni mwa Msimu uliopita kwa Dau la Rekodi ya Uingereza la Pauni Milioni 59.7 lakini Mchezaji huyo baada ya kuwika katika Mechi zake chache za kwanza alififia vibaya na kuanza Mechi 1 tu katika 10 zake za mwisho.
Di Maria alipaswa kujiunga na Man United Ziarani huko USA hapo Julai 25 lakini hakutokea na hata Van Gaal alikiri hajui alipo huku kukiwa na taarifa Man United inamlima Mshahara wake kwa Siku zote ambazo ameingia mitini.
Hali hiyo imemfanya Van Gaal aitake Bodi imuuze haraka Di Maria ili wachangamke kupata Mchezaji mwinngine mpya ambae kwa sasa anatajwa sana Fowadi wa Barcelona Pedro.
Wakati huo huo imedaiwa kuwa Van Gaal pia ameishauri Bodi kumuuza haraka Kipa David De Gea ambae anataka kurudi kwao Spain kuichezea Real Madrid.
Ingawa awali Van Gaal alipendelea kumshawishi De Gea abaki lakini baada ya kuchoshwa na uchezaji wake hasa walipofungwa 2-0 na PSG huko USA katika Mechi yao ya mwisho huku Kipa huyo akilaumiwa kwa kufungisha, Van Gaal ameamua kumtosa haraka Kipa huyo.
Tayari Man United wameshamchukua Kipa wa Argentina Sergio Romero lakini zipo habari pia wanamtaka Kipa wa Holland Jasper Cillessen anaedakia Ajax.
MECHI ZA MAN UNITED:
-ZIARA USA
Ratiba/Matokeo:
18 Jul: Man United 1 Club America 0
22 Jul: Man United 3 San Jose Earthquakes 1
25 Jul: Man United 3 FC Barcelona 1
30 Jul: Man UNited 0 Paris Saint-Germain 2
LIGI KUU ENGLAND
Agosti 8 [Saa 1445]: Tottenham Hotspur [Old Trafford]
Agosti 14 [Saa 2145]: Aston Villa [Villa Park]
UCL
Agosti 18/19 [Saa 2145]: UEFA Championz Ligi-Mechi ya Kwanza Raundi ya Mchujo
LIGI KUU ENGLAND
Agosti 22 [Saa 1445]: Newcastle United [Old Trafford]
UCL
Agosti 25/26 [Saa 2145]: UEFA Championz Ligi-Mechi ya Marudiano Raundi ya Mchujo
LIGI KUU ENGLAND
Agosti 30 [Saa 1800]: Swansea City [Liberty Stadium]

MAN UNITED YAANUA JEZI MPYA ZA ADIDAS!

MAN-UNITED-KITADIDAS wameungana tena na Klabu ya Manchester United na Jana kuzionyesha hadharani kwa mara ya kwanza Jezi mpya kwa ajili ya Msimu mpya wa 2015/16.
Wakiwa na Mashabiki zaidi ya Milioni 659 Dunia nzima, Man United ni moja ya Klabu mashuhuri Ulimwenguni kote.
Wakiiga Jezi zao za Miaka ya 1980, Man United na Adidas wametoa Jezi za Mechi za Nyumbani zenye Kola ya V na Mistari Mitatu Begani.
MECHI ZA MAN UNITED:
-ZIARA USA
Ratiba/Matokeo:
18 Jul: Man United 1 Club America 0
22 Jul: Man United 3 San Jose Earthquakes 1
25 Jul: Man United 3 FC Barcelona 1
30 Jul: Man UNited 0 Paris Saint-Germain 2
LIGI KUU ENGLAND
Agosti 8 [Saa 1445]: Tottenham Hotspur [Old Trafford]
Agosti 14 [Saa 2145]: Aston Villa [Villa Park]
UCL
Agosti 18/19 [Saa 2145]: UEFA Championz Ligi-Mechi ya Kwanza Raundi ya Mchujo
LIGI KUU ENGLAND
Agosti 22 [Saa 1445]: Newcastle United [Old Trafford]
UCL
Agosti 25/26 [Saa 2145]: UEFA Championz Ligi-Mechi ya Marudiano Raundi ya Mchujo
LIGI KUU ENGLAND
Agosti 30 [Saa 1800]: Swansea City [Liberty Stadium]

MAUNITED-JEZI MPYA

LVG AONGELEA KIPIGO, AGUSIA TIMU, FOMESHENI!

LVG-AONGEALicha ya kuhuzunishwa kufungwa 2-0 na Paris Saint-Germain huko Soldier Field, Chicago, USA, Meneja wa Manchester United Louis van Gaal ameridhika na Timu yake na kudai kufungwa huko kutawasaidia.

Kipigo hicho kimeifanya Man United washindwe kutetea Taji la International Champions Cup licha ya kushinda Mechi 3 ikiwemo ile waliyowatwanga 3-1 Mabingwa wa Ulaya Barcelona.

Lakini Van Gaal amesema kufungwa kwao kunatokana na makosa binafsi walipofungwa Bao la kwanza kwa kujifunga mwenyewe Luke Shaw alipojichanganya na Kipa wake David de Gea.

Van Gaal amesema: "Ndio tumefungwa pengine hiyo ni viziri kwani Mwaka Jana tulishinda Mechi zote tukaja kufungwa Mechi ya Kwanza ya Ligi."

Mechi ijayo kwa Man United ni hapo Jumamosi Agosti 8 Uwanjani Old Trafford na Tottenham  ikiwa ni Mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu England.

Pia, Van Gaal amedokeza kuitumia Fomesheni ya 4-3-2-1 kwa kuwachezesha Mafulbeki Luke Shaw na Matteo Darmian huku Sentahafu akiwa Daley Blind akisaidiwa na Mtu mwingine ambae hakumtaja.

Kuhusu kuntumia Blind kama Sentahafu Meneja huyo amesema Mchezaji huyo huanzisha vyema mipira na pia mzuri katika kujihami.

 

KAGAME CUP: GOR, AL KHARTOUM HIZO NUSU FAINALI, JUMATANO YANGA, AZAM NANI KIDUME?

KAGAME-CUP-2015-TZ-squareAl Khartoum ya Sudan na Gor Mahia ya Kenya Leo zimefanikiwa kutinga Nusu Fainali ya Kagame Cup, Kombe la Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na ya Kati baada ya kushinda Mechi zao za Robo Fainali.
Kwenye Nusu Fainali, Gor Mahia itapambana na Al Khartoum.
Kwenye Robo Fainali ya kwanza hii Leo, Al Khartoum iliiteketeza APR ya Rwanda kwa kuitandika Bao 4-0 na Gor Mahia kuibwaga Makakia ya South Sudan Bao 2-1 huku Bao zote mbili zikifungwa na Mchezaji wa KImataifa wa Uganda Godfrey Walusimbi.
Hapo Kesho Jumatano zipo Mechi 2 za Robo Fainali na ya kwanza ni kati ya Al Shandy ya Sudan na KCCA ya Uganda na kufuatiwa na mtanange wa Timu za Nyumbani Yanga na Azam FC.
Washindi wa Mechi hizi mbili watacheza Nusu Fainali ya Pili ya Michuano hii.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++
RATIBA
ROBO FAINALI 
Jumanne Julai 28, 2015 
APR 0 Al Khartoum 4
Gor Mahia 2 Malakia 1
Jumatano Julai 29, 2015
Al Shandy Vs KCCA [Saa 7 Dakika 45 Mchana]
Azam FC Vs Yanga [Saa 10 na Robo Jioni]
NUSU FAINALI
Ijumaa Julai 31, 2015 
Al Khartoum v Gor Mahia  [Mechi Na 27]
Mshindi 23 Vs Mshindi 24 [Mechi Na 28]
MSHINDI WA TATU NA FAINALI 
Jumapili Agosti 2, 2015 
Aliyefungwa 27 Vs Aliyefungwa 28
Mshindi 27 Vs Mshindi 28
 

Habari MotoMotoZ