JESUS NJE MIEZI KADHAA, AVUNJIKA MFUPA MGUUNI!

IMG-20170215-WA0000FOWADI mpya wa Manchester City kutoka Brazil Gabriel Jesus amevunjika Mfupa wa Mguu wake wa Kulia na sasa huenda akawa nje kwa Miezi kadhaa.City imethibitisha hilo lakini imeeleza anapaswa kuchunguzwa zaidi ili kupata undani.Jesus, mwenye Miaka 19, aliumia Juzi Jumatatu Usiku City ilipoifunga Bournemouth 2-0 huko Vitality Stadium kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England.Jesus aliumia na kutolewa nje kwenye Dakika ya 15.Inaaminika Jesus amevunjika mmoja wa ile Mifupa Mitano ya inayounganisha Kifundo cha Enka na Vidole vya Mguu (Metatarsal).Jesus, ambae alihamia rasmi City akitokea Palmeiras ya Brazil Januari kwa Dau la Pauni Milioni 27, ameichezea City Mechi 5 na kufunga Bao 2 akichukua Namba ya Sentafowadi wa Argentina Sergio Aguero.Straika huyo alikuwa mbioni kuifikia Rekodi ya City ya kuwa Mchezaji wa 3 mpya aliefunga Bao katika kila Mechi katika Mechi zake 3 za mwanzo za Ligi.Wanaoshikilia Rekodi hiyo ya City ni Straika wao wa zamani Emmanuel Adebayor na Mchezaji wao wa sasa.Kevin de Bruyne.

EPL: VINARA CHELSEA NGOMA DROO NA BURNLEY HUKO TURF MOOR!

EPL – Ligi Kuu England

Ratiba/Matokeo:

Jumapili Februari 12

CHELSEA-BURNLEYBurnley 1 Chelsea 1

1900 Swansea City v Leicester City       

+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

VINARA wa EPL, Ligi Kuu England, Chelsea Leo wameikosa nafasi ya kwenda Pointi 12 mbele baada ya kutoka Sare na Burnley huko Turf Moor.

Chelsea sasa wako Pointi 10 mbele ya Timu ya Pili Tottenham lakini Jumatatu Usiku Manchester City wanaweza kutwaa Nafasi ya Pili na pengo lao na Chelsea kuwa Pointi 8 ikiwa wataifunga Bournemouth Ugenini.

Hii Leo Chelsea walitangulia kufunga Dakika ya 7 kwa Bao la Pedro lakini Robbie Brady akaisawazishia Burnley Dakika ya 24 kwa Frikiki kali.EPL-FEB12

Matokeo haya yanawaweka Burnley Nafasi ya 12 na kudumisha rekodi yao ya kuwa wagumu mno wakiwa kwao Turf Moor.

VIKOSI:

BURNLEY (Mfumo 4-4-2): Heaton; Lowton, Keane, Mee, Ward; Boyd, Barton, Westwood, Brady; Gray, Barnes.

Akiba: Flanagan, Arfield, Vokes, Darikwa,Gudmundsson, Tarkowski, Robinson.

CHELSEA (Mfumo 3-4-3): Courtois; Azpilicueta, David Luiz, Cahill (c); Moses, Kante, Matic, Alonso; Pedro, Diego Costa, Hazard.

Akiba: Begovic, Zouma, Ake, Chalobah, Fabregas, Willian, Batshuayi.

REFA: Kevin Friend

EPL – Ligi Kuu England

Ratiba

Jumatatu Februari 13

2300 Bournemouth v Manchester City   

Jumamosi Februari 25

1800 Chelsea v Swansea City               

1800 Crystal Palace v Middlesbrough              

1800 Everton v Sunderland         

1800 Hull City v Burnley             

Southampton v Arsenal [IMEAHIRISHWA]

1800 West Bromwich Albion v Bournemouth              

2030 Watford v West Ham United         

Jumapili Februari 26

1630 Tottenham Hotspur v Stoke City             

Manchester City v Manchester United [IMEAHIRISHWA]

Jumatatu Februari 27

2300 Leicester City v Liverpool             

Jumamosi Machi 4

1530 Manchester United v Bournemouth         

1800 Leicester City v Hull City              

1800 Stoke City v Middlesbrough          

1800 Swansea City v Burnley                

1800 Watford v Southampton               

1800 West Bromwich Albion v Crystal Palace             

2030 Liverpool v Arsenal            

Jumapili Machi 5

1630 Tottenham Hotspur v Everton       

1900 Sunderland v Manchester City      

Jumatatu Machi 6

2300 West Ham United v Chelsea

VPL: SIMBA YAIFUNGA PRISONS NA KUITOA YANGA KILELENI!

VPL – Ligi Kuu Vodacom

Matokeo:

Jumamosi Februari 11 

Simba 3 Tanzania Prisons 0

Stand United 0 Majimaji 0

Ndanda FC 0 Toto African 0

Ruvu Shooting 0 Azam FC 0

+++++++++++++++++++++

VPL-DTB-SITSimba Leo wamekaa kileleni mwa VPL, Ligi Kuu Vodacom, baada ya kuichapa Tanzania Prisons 3-0 Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Simba sasa wana Pointi 51 kwa Mechi 22 wakifuata Mabingwa Watetezi Yanga wenye Pointi 49 kwa Mechi 21.

Katika Mechi ya Leo, Simba waliongoza 2-0 hadi Mapumziko kwa Bao za Juma Luizio na Ibrahim Ajib .

Simba walipiga Bao la 3 Dakika ya 67 Mfungaji akiwa Laudit Mavugo.

Jumapili zipo Mechi 3 za VPL na Mwadui FC itacheza na Mbeya City kwenye Uwanja wa Mwadui wakati African Lyon itacheza na Mtibwa Sugar Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na pia JKT Ruvu itakuwa mwenyeji wa Mbao FC kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.

VIKOSI:

SIMBA: Daniel Agyei, Janvier Bokongu, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Novaty Lufunga, Method Mwanjali [Mwinyi Kazimoto, 62’], James Kotei, Said Ndemla, Muzamil Yassin, Laudit Mavugo, Ibrahim Ajib [Pastory Athanas, 74’], Juma Luizio [Shiza Kichuya, 70’]

PRISONS: Laurian Mpalile, Aaron Kalambo, Salum Kimenya, James Mwasote, Nurdin Chona, Jumanne Elfadhil, Lambert Sibiyanka, Kazungu Nchinjayi Kassim Hamisi, 38’], Victor Hangaya [Salum Bosco, 76’], Mohammed Samatta na Benjamin Asukile [Meshack Suleiman, 56’]

REFA: Alex Mahagi [Mwanza]

VPL – Ligi Kuu Vodacom

Ratiba

Jumapili Februari 12

Mwadui vs Mbeya City

African Lyon vs Mtibwa Sugar

JKT Ruvu vs Mbao FC

VPL: LEO SIMBA KUIFUNGA PRISONS NA KUITOA YANGA KILELENI?

VPL-DTB-SITSIMBA hii Leo wana nafasi murua ya kutwaa uongozi wa VPL, Ligi Kuu Vodacom, ikiwa wataifunga Tanzania Prisons kwenye Mechi itakayochezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Ushindi kwa Simba, chini ya Kocha kutoka Cameroon Joseph Omog, utawafanya wawe na Pointi 51 na kuwatoa Yanga, walio na Pointi 49, uongozini.

Wikiendi hii Yanga hawachewzi VPL kwa vile Jumapili wako huko Comoro kucheza na Ngaya kwenye Mechi yao ya Kwanza ya Raundi ya Awali ya CAF CHAMPIONZ LIGI.

Simba watatinga kwenye Mechi hii wakiwa na ari kubwa kwani, baada ya kuyumba kwa kipigo, waliibuka Wikiendi iliyopita kwa kuitwanga Majimaji 3-0 huko Songea.

Leo pia zipo Mechi nyingine 3 za VPL ambazo Stand United watakuwa wenyeji wa Majimaji y Songea kwenye Uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga wakati Ndanda FC ikiialika Toto Africans kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara na Ruvu Shooting ikichea na Azam FC kwenye Uwanja wa Mabatini, Pwani.

Jumapili, Mwadui FC itacheza Mbeya City kwenye Uwanja wa Mwadui wakati African Lyon itacheza na Mtibwa Sugar Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na pia JKT Ruvu itakuwa mwenyeji wa Mbao FC kwneye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.

VPL-FEB10

VPL – Ligi Kuu Vodacom

Ratiba

Jumamosi Februari 11 

Stand United vs Majimaji

Simba vs Tanzania Prisons

Ndanda FC vs Toto African

Ruvu Shooting vs Azam FC

Jumapili Februari 12

Mwadui vs Mbeya City

African Lyon vs Mtibwa Sugar

JKT Ruvu vs Mbao FC

EPL 4 BORA: CHELSEA BINGWA MTARAJIWA, SPURS, CITY, LIVERPOOL, ARSENAL NA MAN UNITED NANI NDANI NANI NJE?

EPL-SOKATAMU-SITUPO mjadala mkali miongoni mwa Wachambuzi wa Soka huko England kuhusu Timu zipi 4 zitakuwemo kwenye 4 Bora ya EPL, Ligi Kuu England, mwishoni mwa Msimu.
Wengi wa Wachambuzi hao tayari wanaipa Chelsea Ubingwa kwa vile inaongoza Ligi hii kwa muda mrefu na sasa wapo Pointi 9 mbele ya Timu ya Pili Tottenham Hotspur.
Lakini ni Pointi 5 tu zinaitenganisha Spurs walio Nafasi ya Pili na Manchester United ambao ni wa 6 huku Manchester City, Arsenal na Liverpool wakishikilia Nafasi za 3 hadi ya 5.
Swali kubwa waliopewa Wachambuzi wakubwa wa SKY SPORTS TV ya huko England ni huku kila Timu imebakisha Mechi 14 kumaluza Ligi je Timu zipi 4 zitafuzu 4 Bora na kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao?
YAFUATAYO NI MAONI YA WACHAMBUZI HAO:
Matt Le Tissier:
-Nadhani njiani Chelsea watapepesuka kidogo lakini watakuwa Mabingwa. 
4 Bora watakuwemo pia Manchester City na Tottenham pamoja na Manchester United ambao wako kwenye wimbi refu la kutofungwa.
Le Tiss - Ubashiri wake: Chelsea Namba 1, Manchester City 2, Tottenham 3, Manchester United 4.
Phil Thompson
-Ni ngumu kwa sasa na Arsenal au Man United wanaweza kirahisi kuwa wa Pili na wa 3.
Thompson - Ubashiri wake: Chelsea 1, Manchester City 2, Tottenham 3, Liverpool 4.
Charlie Nicholas
-Sasa inaanza kuvutia na Arsenal kila mara wako hivi wanateleza lakini wanakuwemo 4 Bora.
Kwa hali ilivyo Chelsea ni Bingwa na Man City ambae sasa wana Gabriel Jesus wamo. Nadhani Spurs pia watakuwemo.
Charlie - Ubashiri wake: Chelsea 1, Manchester City 2, Tottenham 3, Arsenal 4.
Paul Merson
-Nadhani Chelsea watatwaa Ubingwa. Tizama walichokifanya kwa Timu za nje ya 6 Bora wakishinda 15 na Sare 1 tu na sasa wamebakisha Mechi 2 tu dhidi ya Timu zilizomo 6 Bora.
Merson - Ubashiri wake: Chelsea 1, Tottenham 2, Manchester City 3, Manchester United 4
EPL – Ligi Kuu England
Ratiba
Jumamosi Februari 11
1530 Arsenal v Hull City             
1800 Manchester United v Watford          
1800 Middlesbrough v Everton    
1800 Stoke City v Crystal Palace           
1800 Sunderland v Southampton
1800 West Ham United v West Bromwich Albion                 
2030 Liverpool v Tottenham Hotspur        
Jumapili Februari 12
1600 Burnley v Chelsea    
1900 Swansea City v Leicester City           
Jumatatu Februari 13
2300 Bournemouth v Manchester City