UEFA EUROPA LIGI: KRC GENK YA SAMATTA YASONGA, SPURS NJE!

EUROPA-LIGI-2016-17-SAMAMechi za Pili za Raundi ya Mtoano ya Timu 32 za UEFA EUROPA LIGI zimekamilika Usiku huu na sasa Timu Washindi 16 wakisubiri Droo ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 kufanyika Ijumaa huku miongoni mwao ni Klabu ya Straika wa Tanzania, Mbwana Samatta,

Klabu ya Samatta, KRC Genk ya Belgium, wakicheza Nyumbani, imefanikiwa kusonga kwa Bao la Dakika ya 67 la Pozuelo walipoifunga Astra Giurgiu ya Romania 1-0 huku Samatta akicheza Dakika zote 90.

Timu hizo zilitoka 2-2 huko Romania Wiki iliyopita.    

Huko White Hart Lane, London, Tottenham Hotspur, wakicheza Mtu 10 kuanzia Dakika ya 39 kufuatia Kadi Nyekundu kwa Dele Alli, wametoka Sare 2-2 na KAA Gent ya Belgium na kutupwa nje kwa vile walifungwa 1-0 katika Mechi ya kwanza.

Bao za Mechi hiyo zilifungwa na Eriksena, Dakika ya 10, na Wanyama, 61’, kwa Spurs na Gent kufunga kupitia Harry, 20’, akijifunga mwenyewe na Perbet, 82’.

UEFA EUROPA LIGI – Raundi ya Mtoano ya Timu 3

Matokeo:

Mechi za Pili

**Kwenye Mabano Jumla ya Magoli kwa Mechi 2

Alhamisi Februari 23

Osmanlispor 0 Olympiakos 3 (0-3)

Ajax 1 Legia Warsaw 0 (1-0)

Apoel Nicosia 2 Athletic Bilbao 0 (4-3)

Besiktas 2 Hapoel Be'er Sheva 1 (5-2)

AS Roma 0 Villarreal 1 (4-1)

Zenit St Petersburg 3 RSC Anderlecht 1 (3-3, Anderlecht wasonga, Goli la Ugenini)

FC Copenhagen 0 Ludogorets Razgrad 0 (2-1)

Fiorentina 2 Borussia Mönchengladbach 4 (3-4)

KRC Genk 1 Astra Giurgiu 0 (3-2)

Lyon 7 AZ Alkmaar 1 (11-2)

Shaktar Donetsk 0 Celta Vigo 1 (Dakika 90 1-1, Zimeongezwa Dak 30)

Sparta Prague 1 FC Rostov 1 (1-5)

Tottenham Hotspur 2 KAA Gent 2 (2-3)

Jumatano Februari 22

FC Schalke 04 1 PAOK Salonika 1 (4-1)

Fenerbahçe 1 FK Krasnodar 1 (1-2)

Saint-Étienne 0 Manchester United 1 (0-4)

+++++++++++++++++++++++++++++

UEFA EUROPA LIGI

Tarehe Muhimu:

09/03/17: Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Mechi za Kwanza

16/03/17: Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Marudiano

13/04/17: Robo Fainali, Mechi za Kwanza

20/04/17: Robo Fainali, Mechi za Pili

04/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Kwanza

11/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Pili

FAINALI

24 Mei 2017: Friends Arena, Solna, Sweden

UEFA EUROPA LIGI: LEO MBWANA SAMATTA NA GENK YAKE KUUNGANA NA MAN UNITED RAUNDI IJAYO?

EUROPA-LIGI-2016-17BAADA ya Jana Timu 3 kufuzu kutinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA EUROPA LIGI, Leo Usiku zipo Mechi 13 za Marudiano za Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ambazo zitatoa Washindi 13.
Timu 3 ambazo zilicheza Marudiano Jana Usiku na kufuzu ni Manchester United, FC Schalke na FK Krasnodar.
Miongoni mwa Mechi za Leo ni ile itakayochezwa huko Belgium kati ya KRC Genk ambao ni Wenyeji na Klabu ya Romania Astra Giurgiu.
KRC Genk ni maarufu kwa Watanzania kwa vile Straika wao mahiri, Mbwana Samatta, huichezea.
Wiki iliyopita iliyopita Timu hizo zilutoka Sare ya 2-2 huko Romania na sasa Genk wanahitaji tu Sare ya 0-0 au 1-1 ili wasonge.
Nayo Timu maarufu ya England Tottenham Hotspur wana kazi ngumu Uwanjani kwao White Hart Lane Jijini London wakirudiana na Timu nyingine ya Belgium KAA Gent ambayo ilishinda 1-0 katika Mechi ya Kwanza.
Droo ya kupanga Mechi za Raundi ijayo itafanyika Ijumaa.
UEFA EUROPA LIGI – Raundi ya Mtoano ya Timu 32
Mechi za Pili
Jumatano Februari 22
Matokeo:
**Kwenye Mabano Jumla ya Magoli kwa Mechi 2
FC Schalke 04 1 PAOK Salonika 1 (4-1)
Fenerbahçe 1 FK Krasnodar 1 (1-2)
Saint-Étienne 0 Manchester United 1 (0-4)
UEFA EUROPA LIGI – Raundi ya Mtoano ya Timu 32
Ratiba
Mechi za Pili
**Saa za Bongo
**Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza
Alhamisi Februari 23
1900 Osmanlispor v Olympiakos (0-0)
2100 Ajax v Legia Warsaw (0-0)
2100 Apoel Nicosia v Athletic Bilbao (2-3)
2100 Besiktas v Hapoel Be'er Sheva (3-1)
2100 Roma v Villarreal (4-0)
2100 Zenit St Petersburg v RSC Anderlecht (0-2)
2305 FC Copenhagen v Ludogorets Razgrad (2-1)
2305 Fiorentina v Borussia Mönchengladbach (1-0)
2305 KRC Genk v Astra Giurgiu (2-2)
2305 Lyon v AZ Alkmaar (4-1)
2305 Shaktar Donetsk v Celta Vigo (1-0)
2305 Sparta Prague v FC Rostov (0-4)
2305 Tottenham Hotspur v KAA Gent (0-1)
UEFA EUROPA LIGI
Tarehe Muhimu:
16/02/17: Raundi ya Mtoano ya Timu 32, Mechi za Kwanza
23/02/17: Raundi ya Mtoano ya Timu 32, Marudiano
09/03/17: Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Mechi za Kwanza
16/03/17: Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Marudiano
13/04/17: Robo Fainali, Mechi za Kwanza

MAN UNITED NA MSONGO WA RATIBA LIGI KUU, EFL CUP, FA CUP, EUROPA LIGI!

>WAO MECHI 25, CHELSEA 16, LIVERPOOL 13!

TAYARI Meneja wao Jose Mourinho ameshalamikia Timu yake Manchester United kusongwa na Mechi nyingi za EPL, Ligi Kuu MANUNITED-WOODWARD-MOURINHO-MIPANGONIEngland, EFL Cup, FA Cup na Europa Ligi.

Ukweli ni kuwa ikiwa watasonga mbele kwenye Mashindano yote ya Makombe ambayo wamo basi hadi mwishoni mwa Msimu kuanzia sasa wanaweza kucheza Mechi 25 wakati Wapinzani wao Chelsea na Liverpool wakicheza Mechi 16 na 13 tu.

Klabu nyingine ambazo zinaikaribia Man United kwa kukabiliwa na Mechi nyingi ni Tottenham, Man City na pia Arsenal.

Kwa sababu Jumapili ijayo Man United wanacheza Fainali ya EFL Cup na Southampton, ile Dabi yao na Man City imeahirishwa na pia kuingia kwao kucheza Robo Fainali ya FA CUP na Chelsea hapo Machi 11 kumefanya Mechi yao ya EPL na Southampton pia iahirishwe.

Jumatano Man United wanasafiri kwenda huko France kucheza Mechi ya Pili ya UEFA EUROPA LIGI na St-Etienne ambayo waliichapa 3-0 na ikiwa watasonga mbele basi itawaletea athari kubwa kwenye azma yao ya kumaliza ndani ya 4 Bora ya EPL na kusonga kwenye FA CUP.

JUMLA YA MECHI HADI MWISHONI MWA MSIMU:

Klabu

Jumla ya Mechi

Man United

25

Tottenham

24

Man City

24

Arsenal

22

Chelsea

16

Liverpool

13

Hii inakuja kwa sababu Mechi yao ya kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya EUROPA LIGI itachezwa Alhamisi Machi 9 ikiwa ni Siku 2 tu kabla ya kuivaa Chelsea kwenye FA CUP.

Na Mechi ya Marudiano ya EUROPA LIGI itachezwa Mechi 16 ikiwa ni Siku 3 tu kabla ya tripu yao kwenda kuivaa Middlesbrough kwenye EPL.

Ikiwa watatinga Robo Fainali ya EUROPA LIGI basi watacheza Mechi yao Siku chache kabla kucheza na Chelsea kwenye Ligi na wakisonga Nusu Fainali ya EUROPA LIGI basi pia Mechi zake za EPL dhidi ya Arsenal na Tottenham zitafuatia hizo za Nusu Fainali.

Na ikiwa watatinga Fainali za EUROPA LIGI na FA CUP basi watacheza Mechi yao ya mwisho ya EPL hapo Mei 21 dhidi ya Crystal Palace na Mei 24 watapaswa kusafiri kwenda Stockholm, Sweden kucheza Fainali ya EUROPA LIGI na Mei 27 kurudi Wembley Jijini London kucheza Fainali ya FA CUP.

MAN UNITED – Ratiba inayoweza kuwakabili hadi mwishoni mwa msimu:

Mashindano

Mpinzani

Tarehe

Europa Ligi

St-Etienne

22 Februari

EPL

Man City

Imeahirishwa

EFL Cup

Southampton

26 Februari

EPL

Bournemouth

4 Machi

Europa Ligi

?

9 Machi

FA Cup

Chelsea

11 Machi

EPL

Southampton

Imeahirishwa

Europa Ligi

?

16 Machi

EPL

Middlesbrough

19 Machi

EPL

West Brom

1 Aprili

EPL

Everton

4 Aprili

EPL

Sunderland

8 Aprili

Europa Ligi

?

13 Aprili

EPL

Chelsea

15 Aprili

Europa Ligi

?

20 Aprili

FA Cup

?

22 Aprili/ 23 Aprili

EPL

Burnley

22 Aprili

EPL

Swansea

29 Aprili

Europa Ligi

?

4 Mei

EPL

Arsenal

6 Mei

Europa Ligi

?

11 Mei

EPL

Tottenham

13 Mei

EPL

Crystal Palace

21 Mei

Europa Ligi

?

24 Mei

FA Cup

?

27 Mei

 

MAN UNITED, PLANI YA PAUNI BILIONI 1, MOURIMHO MKATABA MPYA, WACHEZAJI WAPYA KUTUA!

MANUNITED-WOODWARD-MOURINHO-MIPANGONIHABARI zimevuja huko England kuwa Mtendaji Mkuu wa Manchester United, Ed Woodward, amesuka Mpango kabambe wa Miaka Mitano utakaogharimu Pauni Bilioni 1 kuisuka upya Timu na kumpa Mkataba Mpya Meneja wao Jose Mourinho.

Inaaminika Mpango huo unaanza mwishoni mwa Msimu huu ambapo Mourinho atapewa Mkataba Mpya wa Miaka Mitano wenye masurufu makubwa kwake.

Hivi sasa Mourinho yupo kwenye Mkataba wa Miaka Mitatu wenye nyongeza ya Mwaka Mmoja juu yake.

Kwa mujibu wa Jarida moja huko Uingereza, Man United inamtambua Mourinho kama kitega uchumi cha muda mrefu na tayari Ed Woodward ameshaongea na Wamiliki wa Klabu hiyo, Familia ya Glazier, kuhusu kumfunga zaidi Mourinho kwa kuboresha Mkataba wake.

Sambamba na mipango ya kumbakisha Mourinho kwa muda mrefu, pia inasadikiwa mwishoni mwa Msimu Man United itachota Mastaa kadhaa wa Soka ili kuimarisha Kikosi chao.

Mourinho yupo kwenye Msimu wake wa kwanza na Man United ambao umeonyesha mabadiliko makubwa kwa sasa kwa kuwa na wimbi la kutofungwa katika Mechi 16 lililoanza Oktoba na kuwemo kwenye Makombe Matatu ambayo ni EFL CUP wakiwa Fainali, FA CUP wapo Raundi ya Tano na UEFA EUROPA LIGI wapo mguu mmoja kutinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16.

Mwanzoni mwa Msimu, Man United walitwaa Ngao ya Jamii.

Kwenye EPL, Ligi Kuu England, Man United wapo Nafasi ya 6 walikoganda tangu Novemba 6, ukiondoa Siku 1 tu walipopanda Nafasi ya 5, lakini pengo lao na Timu ya 5 Liverpool ni Pointi 1 tu, pengo na Timu za 4 na 3, Arsenal na Tottenham, ni Pointi 2 wakati lile na Timu ya Pili Man City ni Pointi 4 huku Chelsea, ambao ndio Vinara, wako Pointi 12 mbele yao.

MOURINHO ‘HATAMWAGA KUSUDI’ FA CUP!

>>JUMAPILI ROVERS v MAN UNITED EWOOD PARK!

BLACKBURN-MANUNITEDBOSI wa Manchester United Jose Mourinho amesema amejifunza huko nyuma hasara ya ‘kulitupa FA CUP’ na hatafanya kosa hilo tena Jumapili wakiwa Ugenini kucheza na Blackburn Rovers katika Raundi ya 5 ya Kombe hilo.

Man United ndio Mabingwa wa FA CUP walipolitwaa Mei Mwaka Jana wakiwa chini ya Meneja Louis van Gaal.

Mwaka 2005, akiwa na Chelsea, Chelsea walitupwa nje ya FA CUP na Newcastle katika Wiki hiyo hiyo ambayo waliifunga Liverpool na kubeba Kombe la Ligi na pia kuifunga Barcelona katika UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI.

Mourinho ameeleza: “Nilicheza mno kamari na kuzitilia mkazo Barcelona na Liverpool. MANUNITED-MOU-PLAYERS-TRAININGIlikuwa poa kuifunga Barcelona na kushinda Fainali kwa kuifunga Liverpool lakini sikujisikia vyema kwa kutolewa FA CUP kwani nilihisi ‘nimeitupa’ Mechi ile! Sasa sitatupa Mechi!”

Aliongeza: “Sasa tukifungwa ni kwamba Wapinzani ni bora au hatukucheza vizuri lakini ‘sitatupa’ Mechi!”

Safari hii tena yupo katika hali kama hiyo alipokuwa na Chelsea kwani Man United Alhamisi inarudiana na St-Etienne huko France wakisaka kuingia Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA EUROPA LIGI na Jumapili ijayo wapo Wembley Jijini London kuivaa Southampton kwenye Fainali ya EFL CUP, Kombe la Ligi la England.

Ameeleza: “Naenda Blackburn na heshima. Nakwenda nikiwa makini mno. Nitabadili Wachezaji wachache lakini Timu itakuwa nzuri kwa sababu naheshimu Mashindano haya na daima Manchester United inataka uwe makini na kutilia mkazo kila Gemu!”

Hivi sasa Blackburn, ambao waliwahi kutwaa Ubingwa wa EPL, Ligi Kuu England, wakiwa ni moja ya Timu 6 tu kufanya hivyo, wanacheza Daraja la chini Championship tangu walipoporomoka toka EPL mwishoni mwa Msimu wa 2011/12.

Kwa sasa Blackburn wapo wa pili toka mkiani kwenye Msimamo wa Championship na mara ya mwisho kukutana na Man United ni Aprili 2012 walipofungwa 2-0.

Kwenye Ligi yao, Blackburn, wakiwa chini ya Meneja Owen Coyle, wameshinda Mechi 2 tu kati ya 10 walizocheza mwisho na Jumanne iliyopita walitwangwa 2-1 na Sheffield Wednesday.

Man United wao hawajafungwa katika Mechi 16 zilizopita tangu wafungwe Oktoba Mwaka Jana.

Mshindi wa Mechi hii anatinga Raundi ya 6 ya FA CUP ambayo ndiyo Robo Fainali.

FA CUP

Raundi ya 5

**Saa za Bongo

Jumamosi Februari 18

1530 Burnley v Lincoln City

1800 Huddersfield Town v Manchester City               

1800 Middlesbrough v Oxford United              

1800 Millwall v Leicester             

2030 Wolverhampton Wanderers v Chelsea               

Jumapili Februari 19

1700 Fulham v Tottenham Hotspur                 

1915 Blackburn Rovers v Manchester United             

Jumatatu Februari 20

2255 Sutton United v Arsenal