KOMBE LA DUNIA 2018 – MAREKANI KUSINI: BRAZIL YAITEKETEZA URUGUAY, JICHO KODO FAINALI RUSSIA!

WC-2018-SA-QUALIFIERSVINARA wa Kanda ya Marekani ya Kusini chini ya Mwamvuli wa Shirikisho lao CONMEBOL kusaka Nchi 4 zitakazotinga moja kwa moja huko Russia Mwaka 2018 kwenye Fainali za Kombe la Dunia, Brazil, wameendeleza ubabe wao kwa kuifyeka Uruguay waliokuwa kwao Montevideo Bao 4-1.

Uruguay walitangulia Bao 1-0 kwa Bao la Penati iliyofungwa Dakika ya 9 na Edinson Cavani.

Brazil walisawazisha Dakika ya 19 kwa kigongo cha Paulinho cha Mita 30 alipopokea Pasi ya Neymar.

Hadi Mapumziko, Uruguay 1 Brazil 1.

Kipindi cha Pili Dakika ya 52 Paulinho aliipa Brazil Bao la Pili na Neymar kupiga Bao tamu na la 3 kwa Brazil.

Kwenye Dakika za Majeruhi, Paulinho alipiga Bao la 4 na Brazil kushinda 4-1.

++++++++++++++++++++++++

JE WAJUA?

-CONMEBOL itatoa Nchi 4 kutinga Fainali za Kombe la Dunia huko Russia Mwaka 2018.

-Nchi hizo zinaweza kuwa 5 ikiwa Timu itakayomaliza Nafasi ya 5 kwenye Kundi lao itashinda Mechi ya Mchujo dhidi ya Timu nyingine toka Bara jingine ambayo itakuwa ni moja toka Kanda ya Oceania yenye Nchi za Visiwani ambazo ni New Zealand, New Caledonia, Fiji, Papua New Guinea, Solomon Islands na Tahiti.

++++++++++++++++++++++++

Baada ya kucheza Mechi 13, Brazil wamezidi kupaa kileleni wakiwa na Pointi 30 wakifuata Uruguay wenye 23.

Baadae huko Buenos Aires Argentina watacheza na Chile.

Raundi nyingine ya Kanda hii itaanza kuchezwa Jumanne Machi 28 na Siku inayofuatia ambapo Vinara Brazil watakuwa kwao kuivaa Paraguay.

VIKOSI:

URUGUAY (Mfumo 4-4-2): M. Silva; M. Pereira, Coates, Godin, G. Silva; Sanchez, Vecino, Arevalo, Rodriguez; Cavani, Rolan

Akiba: Gimenez, Conde, De Arrascaeta, Hernandez, Alvaro, Laxalt, Fucile, Urretaviscaya, Campana, Corujo, Stuani, Lodeiro

BRAZIL (Mfumo 4-3-3): Alisson; Alves, Marquinhos, Miranda, Marcelo; Paulinho, Casemiro, Renato; Coutinho, Neymar, Firmino

Akiba: Fagner, Dudu, Diego, Luis, Fernandinho, Ederson, Diego Souza, Willian, Gil, Silva, Giuliano, Weverton.

REFA: Patricio Loustau [Argentina]

MSIMAMO:

CONMEBOL

Kombe la Dunia – Russia 2018

Mechi za Makundi

Ratiba/Matokeo:

Alhamsi Machi 23, 2017      

Colombia 1 Bolivia 0

Ijumaa Machi 24, 2017   

Paraguay 2 Ecuador 1

Uruguay 1 Brazil 4     

Venezuela 2 Peru 2     

Argentina 1 Chile 0

**Saa za Bongo

Jumanne Machi 28, 2017         

2330 Bolivia  v Argentina

Jumatano Machi 29, 2017         

0001 Ecuador v Colombia

0100 Chile v Venezuela     

0345 Brazil v Paraguay     

0515 Peru v Uruguay        

BRAZIL: TITE AENDELEA KUZUNGUSHA UTEPE WA KEPTENI, SASA MIRANDA KUUVAA!

WC-2018-SA-QUALIFIERSBEKI wa Inter Milan Miranda ndie amepewa Utepe wa Kepteni wa Brazil wakati Ijumaa Alfajiri ikicheza Ugenini huko Mjini Montevideo na Uruguay katika Mechi ya Kundi lao la Nchi za Marekani ya Kusini ya kusaka Washiriki wa Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia.
Baada ya Kepteni wa Brazil Neymar kujiuzulu wadhifa huo Julai Mwaka Jana na tangu ashike madaraka Juni 2016 Kocha wa Brazil Tite alisema atakuwa hana Nahodha wa kudumu na badala yake kuuzungusha Utepe wa Kepteni miongoni mwa Wachezaji vingunge wa Kikosi chake.
Miranda ndie alikuwa Kepteni wa kwanza wa Kikosi cha kwanza kabisa cha Tite Brazil ilipoichapa Ecuador 3-0 huko Quito Septemba 2016.
Wengine waliowahi kuuvaa Utepe huo ni Dani Alves mara 2 (dhidi ya Colombia na  Argentina), Fernandinho (Peru), Filipe Luis (Venezuela) na Renato Augusto (Bolivia) zote zikiwa Mechi za Kundi lao za Kombe la Dunia 2018.
Pia, Robinho na Diego walikuwa ndio Manahodha Brazil ilipocheza Kirafiki na Colombia Mwezi Januari kwenye Mechi ambayo Kikosi cha Tite kiliundwa na Wachezaji waliokuwa wakicheza ndani Nchini Brazil pekee.

BRAZIL: TITE ADOKEZA 11 YAKE BILA JESUS KUIVAA URUGUAY BILA LUIS SUAREZ!

WC-2018-SA-QUALIFIERSKOCHA wa Brazil Tite amedokeza Kikosi chake ambacho kitacheza Ugenini na Uruguay huko Estadio Centenario Montevideo hapo Ijumaa ikiwa ni moja ya Mechi za Nchi za Kanda ya Marekani ya Kusini chini ya Mwamvuli wa Shirikisho lao CONMEBOL kusaka Nchi 4 zitakazotinga moja kwa moja huko Russia Mwaka 2018 kwenye Fainali za WC-SA-TEBO-MAR20Kombe la Dunia.
Baada ya Mechi 12 kwa kila Timu, Brazil ndio wanaongoza wakiwa na Pointi 27 wakifuata Uruguay wenye 23, Ecuador wana 20, Chile 20 na Argentina 19.
Akiwa na Kikosi cha Wachezaji 23, Tite anatarajiwa kumtumia tena Kiungo wa Real Madrid Casemiro ambae alikosa Mechi zao 4 zilizopita na Nafasi yake kushikwa na Fernandinho wa Man City katika Mechi hizo 4.
++++++++++++++++++++++++

JE WAJUA?

-CONMEBOL itatoa Nchi 4 kutinga Fainali za Kombe la Dunia huko Russia Mwaka 2018.

-Nchi hizo zinaweza kuwa 5 ikiwa Timu itakayomaliza Nafasi ya 5 kwenye Kundi lao itashinda Mechi ya Mchujo dhidi ya Timu nyingine toka Bara jingine ambayo itakuwa ni moja toka Kanda ya Oceania yenye Nchi za Visiwani ambazo ni New Zealand, New Caledonia, Fiji, Papua New Guinea, Solomon Islands na Tahiti.

++++++++++++++++++++++++

BRAZIL-ZOEZI
Pia Tite anatarajiwa kumbadili Straika Majeruhi wa Man City Gabriel Jesus na Roberto Firmino wa Liverpool au yule wa Sport Recife Diego Souza. 
Vile vile huenda Kiungo wa Chelsea Willian akapigwa Benchi ili kumtumia Philippe Coutinho wa Liverpool.
Kwa Timu ya Wenyeji Uruguay pigo kubwa kwao ni kumkosa Staa wao mkubwa anaechezea Barcelona, Luis Suarez, ambae ataikosa Mechi hii kwa kuwa Kifungoni Mechi 1 kwa kulimbikiza Kadi za Njano.
BRAZIL - KIKOSI KINATARAJIWA KUWA:
-Allison
-Dani Alves, Marquinhos, Miranda, Marcelo
-Paulinho, Casemiro, Renato Augusto
-Coutinho, Roberto Firmino, Neymar
CONMEBOL

Kombe la Dunia – Russia 2018

Mechi za Makundi

**Saa za Bongo

Alhamsi Machi 23, 2017      

2330 Colombia v Bolivia    

Ijumaa Machi 24, 2017   

0200 Paraguay v Ecuador

0200 Uruguay v Brazil      

0230 Venezuela v Peru     

0230 Argentina v Chile

Jumanne Machi 28, 2017         

2330 Bolivia  v Argentina

Jumatano Machi 29, 2017         

0001 Ecuador v Colombia

0100 Chile v Venezuela     

0345 Brazil v Paraguay     

0515 Peru v Uruguay        

SIR ALEX FERGUSON KUREJEA TENA OLD TRAFFORD!

SIRALEX-CARRICK-MATCHSir Alex Ferguson atarudi tena Old Trafford kwenye Benchi wakati wa Mechi ya Kumtukuza Kiungo wa Manchester United Michael Carrick kwa Utumishi Ulitukuka wa muda mrefu Klabuni hapo.

Ferguson, aliestaafu Umeneja Mwaka 2013 baada ya kuitumikia Man United kwa Miaka 27, ataongoza moja ya Timu katika Mechi hiyo Maalum.

Timu atakayoongoza Sir Alex Ferguson itaitwa Manchester United 2008 XI na itaundwa na Wachezaji waliotwaa Ubingwa wa England na UEFA CHAMPIONZ LIGI Mwaka 2008 wakiwa chini yake.

Timu hiyo itacheza na Timu itakayoitwa Michael Carrick All-Star XI ikiongozwa na aliewahi kuwa mmoja wa Mameneja wa Michael Carrick, Harry Redknapp.

Carrick, mwenye Miaka 35 na ambae amedumu Man United kwa Miaka 11 hadi sasa, ameelezea kurejea kwa Sir Alex Ferguson: “Ni heshima kubwa kurejea kwake na kuwa sehemu ya hiyo Gemu. Yeye pengine ndio sababu pekee nilijiunga na Man United, sina uwezo kumshukuru inavyostahili!”

Miongoni mwa Majina makubwa ya Wachezaji Soka watakaoshiriki Mechi hiyo maalum ni Edwin van der Sar, Gary Neville, Rio Ferdinand, Paul Scholes na Ryan Giggs wakiichezea Man United na upande wa Michael Carrick All-Star XI watakuwemo Steven Gerrard, Frank Lampard na Michael Owen.

ENGLAND: JERMAIN DEFOE, MARCUS RASHFORD, JAKE LIVERMORE, LUKE SHAW KIKOSI CHA GARETH SOUTHGATE!

ENGLAND-DEFOE-RASHFORDGareth Southgate Leo ameshangaza Wadau wa Timu ya Taifa ya England alipotangaza uteuzi wake wa Kikosi chake cha Kwanza kabisa tangu athibitishwe kuwa Meneja wa kudumu kwa kuwaita Jermain Defoe, Jake Livermore na Luke Shaw pamoja na Wachezaji wengine Wanne wapya kabisa.

Kikosi kilichoitwa Leo ni Wachezaji 26 ambacho kitacheza na Mabingwa wa Dunia Germany na kisha Lithuania na wamo Wachezaji Wawili wa Southampton, James Ward-Prowse na Nathan Redmond, waliowahi kucheza chini ya Southgate alipokuwa Kocha Mkuu wa England U-21 lakini hawajahi kuchezea Kikosi cha Kwanza cha England.

Wengine wapya kabisa walioitwa Leo ni Michael Keane na Michail Antonio.

Marcus Rashford, Phil Jones na Ross Barkley wameitwa tena kuichezea Timu ya Taifa huku Straika wa Sunderland Jermaine Defoe, mwenye Miaka 34, ambae mara ya mwisho kuichezea England ni Novemba 2013, kuitwa tena kutokana na pengo la Mafowadi Majeruhi Wayne Rooney, Daniel Sturridge na Harry Kane.

Kwa mshangao wa wengi, Kiungo wa West Bromwich Albion, Jake Livermore, ameitwa baada ya kuichezea England mara moja tu Mwaka 2012 na 2015 kukumbwa na Skandali ya Matumizi ya Kokeni lakini akapata Msamaha baada ya Kifungo kifupi kwani wakati huo alifiwa na Mwanawe.

Pia, Luke Shaw, Fulbeki wa Kushoto wa Man United alieichezea Klabu yake mara 2 toka Novemba, amepata upenyo wa kuitwa tena kutoka na kuumia kwa Danny Rose wa Tottenham.

KIKOSI KAMILI:

MAKIPA: Fraser Forster (Southampton), Joe Hart (Torino, Mkopo kutoka Man City), Tom Heaton (Burnley).

MABEKI: Ryan Bertrand (Southampton), Gary Cahill (Chelsea), Nathaniel Clyne (Liverpool), Phil Jones (Man United), Michael Keane (Burnley), Luke Shaw (Man United), Chris Smalling (Man United), John Stones (Man City), Kyle Walker (Tottenham).

VIUNGO: Dele Alli (Tottenham), Michail Antonio (West Ham), Ross Barkley (Everton), Eric Dier (Tottenham), Adam Lallana (Liverpool), Jesse Lingard (Man United), Jake Livermore (West Brom), Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal), Nathan Redmond (Southampton), Raheem Sterling (Man City), James Ward-Prowse (Southampton).

MAFOWADI: Jermain Defoe (Sunderland), Marcus Rashford (Man United), Jamie Vardy (Leicester).