KINDA WA CHELSEA ATUA LIVERPOOL, EVERTON WAMTAKA BENTEKE, LUKAKU ASEMA ‘ATATOBO UKUTA’ KWA AJILI YA MOURINHO!

ZILIZOBAMBA ENGLAND HII LEO:

DOMINIC SOLANKE: LIVERPOOL YAMSAINI KINDA WA CHELSEA

SOLANKE ATUA LIVERPOOLLiverpool wamekamilisha kumsajili Straika Tineja wa Chelsea Dominic Solanke baada ya Mkataba wake na Chelsea kumalizika na Kinda huyo kugomea Mkataba Mpya.

Hata hivyo, Chelsea wanapaswa kulipwa Ada kwa vile walimkuza Kijana huyo wa Miaka 19 na Jopo Maalum litaamua kiasi cha kulipwa na kinakisiwa kuwa Pauni Milioni 3.

Mapema Mwezi huu, Solanke alifunga Bao 5 wakati Timu ya Taifa ya England U-20 ikitwaa Kombe la Dunia la U-20 huko South Korea.

Msimu wa 2015/16, Solanke alikuwa kwa Mkopo huko Belgium kwenye Klabu ya Vitesse Arnhem na kupachika Bao 7 katika Mechi 25.

Akiwa na Chelsea, Solanke aliichezea Mechi 1 tu akitokea Benchi kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI dhidi ya NK Maribor Oktoba 2014.

EVERTON WAJITAYARISHA KUMNUNUA CHRISTIAN BENTEKE

Baada ya kumuuza Romelu Lukaku kwa Manchester United, Everton sasa wako mbioni kumnunua Straika wa Crystal Palace Christian Benteke ili ajumuike na Wachezaji wao wengine Wapya Sandro Ramirez na Wayne Rooney.

Benteke, ambae pia anafuatiliwa na Chelsea, aliihamaLiverpool na kwenda Palace Msimu uliopita ambako aliifungia Bao 17.

MANUNITED LUKAKU LOSANGELES

ROMELU LUKAKU YUPO TAYARI 'KUTOBOA UKUTA' KWA AJILI YA JOSE MOURINHO

Mchezaji Mpya wa Manchester United Romelu Lukaku ametamba kuwa yupo tayari ‘kutoboa Ukuta’ kwa ajili ya Jose Mourinho.

Jana Lukaku alijumuika kwa mara ya kwanza na Kikosi cha Man United ambacho kipo Mazoezini huko UCLA Jijini Los Angeles, USA.

Hii itakuwa ni mara ya pili kwa Lukaku na Mourinho kufanya kazi pamoja baada ya kuwa wote huko        Chelsea.

Alipoulizwa kama Mourinho alichangia kwa yeye kuhamia Man United, Lukaku alijibu: Yeah, alichangia. Tuna uhusiano mzuri na nipo tayari kupenya Ukutani kwa ajili

DIEGO COSTA KUTOJUMUIKA NA CHELSEA ILIYOANZA HARAKATI ZA KUMPATA MORATA!

Diego Costa amepewa ruhusa ya kutojiunga na Kikosi cha Chelsea kilichoanza kukusanyika Leo kwa ajili ya Mazoezi ya kujitayarisha na Msimu Mpya unaoanza Agosti.
COSTA WAYAHivi sasa Klabu ya zamani ya Costa, Atletico Madrid, ipo mazungumzoni kumnunua Costa.
Meneja wa Chelsea, Antonio Conte, alishamtoa Costa kwenye Kikosi chake cha Msimu Mpya baada ya Mwezi uliopita kumpasulia kinagaubaga kuwa hayumo kwenye mipango yake.
Atletico Madrid tayari ishatoa Ofa ya Pauni Milioni 26 kumnunua Costa kiasi ambacho ni chini ya makisio ya Chelsea kuhusu thamani ya Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Spain.
 Wakati huo huo, zipo ripoti kuwa Chelsea imeanza harakati za kumnunua Alvaro Morata kutoka Real Madrid ya Spain ili ambadili Diego Costa.
Awali Chelsea ilitaka kumnunua Straika wa Everton Romelu Lukaku lakini Mchezaji huyo ameenda Manchester United.
Morata pia ilikuwa aende Man United lakini Uhamisho ukakwama kufuatia Real kutaka Pauni Milioni 70 badala ya Ofa ya Pauni Milioni 60 ya Man United.
Inaaminika Chelsea wapo tayari kulipa hizo Pauni Milioni 70.
Chelsea

Ndani

Willy Caballero Bure

Antonio Rudiger (AS Roma) Pauni Milioni 29

Nje

Juan Cuadrado (Juventus) Ada Haikutajwa

Christian Atsu (Newcastle United) Ada Haikutajwa

Asmir Begovic (AFC Bournemouth) Ada Haikutajwa

Dominic Solanke (Liverpool) Bure

Alex Kiwomya (Doncaster Rovers) Ada Haikutajwa

Bertrand Traore (Olympique Lyonnais) Ada Haikutajwa

Nathan Ake (AFC Bournemouth) Ada Haikutajwa

ROONEY ARUDI EVERTON, MABINGWA CHELSEA WAMSAINI BEKI ANTONIO RUDIGER

EVERTON ROONEYWAKATI Mfungaji Bora katika Historia ya Manchester United Wayne Rooney akijiunga tena na Everton kwa Uhamisho wa Bure, Mabingwa wa England Chelsea wamemsaini Beki wa Timu ya Taifa ya Mabingwa wa Dunia Germany kwa Uhamisho wa Dau la Awali la Pauni Milioni 29 kutoka Klabu ya AS Roma ya Italy.

WAYNE ROONEY

Wayne Rooney, mwenye Miaka 31, ameondoka Manchester United aliyoitumikia Miaka 13 na kurejea Everton alikoanzia Soka lake tangu akiwa Mtoto.

Rooney aliichezea Man United Mechi 559 na kufunga Bao 253 zikiwa ni Bao nyingi kupita Mtu yeyote katika Historia ya Man United.

Akiwa na Man United, Rooney alitwaa Ubingwa wa EPL, Ligi Kuu England, mara 5 na mara moja moja UEFA CHAMPIONZ LIGI, UEFA EUROPA LIGI na FA CUP.

Rooney, ambae aliihama Everton Mwaka 2004 kwa Dau la Pauni Milioni 27, sasa amesaini Mkataba wa Miaka Miwili na Everton.

BEKI ANTONIO RUDIGER

Mabingwa wa England Chelsea wamemsaini Beki wa Timu ya Taifa ya Germany Antonio Rudiger kutoka AS Roma ya Italy kwa Dau la Awali la Pauni Milioni 29.

Rudiger, mwenye Miaka 24, amekamilisha Uhamisho huu ukiwa ni Wiki 1 tu tangu aisaidie Germany kutwaa FIFA Kombe la Mabara kwa kuilaza Chile 1-0 kwenye Fainali.

CHELSEA RUDIGER

Chelsea imempa Rudiger Jezi Namba 2 ambayo alikuwa akiivaa Branislav Ivanovic aliehamia Zenit St Petersburg ya Urusi Mwezi Januari.

Kabla ya kujiunga na AS Roma, Rudiger alianza Soka lake Borussia Dortmund kisha kujiunga na Stuttgart Mwaka 2011.

Alijiunga na AS Roma Mwaka 2015 na Msimu wa 2015/16 aliichezea AS Roma Mechi 30 za AS Roma walipomaliza Ligi hiyo Nafasi ya 3 na Msimu wa 2016/17 kucheza Mechi 26 wakati AS Roma ikimaliza Nafasi ya Pili nyuma ya Mabingwa Juventus.

Rudiger ameichezea Germany Mechi 17.

WAYNE ROONEY – ANG’OLEWA UKEPTENI MAN UNITED!

>UTEPE WATUA KWA MICHAEL CARRICK, MSAIDIZI ANDER HERRERA!

MANUNITED ROONEY KEPTENIWayne Rooney ameondolewa kama Kepteni wa Manchester United huku kukiwa na kila dalili ataondoka na kurudi Klabu yake ya Utotoni Everton.

Rooney, ambae ndie anashikilia Rekodi ya kuwa Mfungaji Bora katika Historia ya Man United akiwa na Bao 253, amebadilishwa na Michael Carrick kama Nahodha na Msaidizi wa Nahodha ni Ander Herrera.

Mabadiliko haya ni dalili tosha kuwa zama za Rooney za Miaka 13 akiwa na Man United akitokea Everton sasa zimefikia tamati katika wakati ambao Meneja Jose Mourinho akisuka Kikosi kipya kwa Msimu Mpya wa 2017/18.

Carrick alipewa nyongeza ya Mwaka Mmoja katika Mkataba wake na sasa atabaki Old Trafford hadi Juni 2018.

Hivi sasa yapo mazungumzo mazito ya kumrudisha Rooney Everton ambako ndiko alikoanzia Soka lake tangu akiwa Mtoto.

Kikosi cha Man United kinakusanyika Leo Jumamosi na Jumapili kitaruka kwenda USA kwa Mazoezi na Ziara ya Mechi za Matayarisho kwa ajili ya Msimu Mpya.

EPL, LIGI KUU ENGLAND – Ratiba Mechi za Wikiendi ya Kwanza ya Ufunguzi

**Saa za Bongo

Ijumaa Agosti 11

2145 Arsenal v Leicester City

Jumamosi Agosti 12

1430 Watford v Liverpool

**Zote Saa 11 Jioni

Chelsea v Burnley

Crystal Palace v Huddersfield Town

Everton v Stoke City

Southampton v Swansea City

West Bromwich Albion v AFC Bournemouth

1930 Brighton & Hove Albion v Manchester City

Jumapili Agosti 13

1530 Newcastle United v Tottenham Hotspur

1800 Manchester United v West Ham United

 

EPL, LIGI KUU ENGLAND: KWA MATAKWA YA TV MUBASHARA, SASA KUANZA IJUMAA AGOSTI 11 EMIRATES ARSENAL v LEICESTER!

EPL 17 18 SITEPL, LIGI KUU ENGLAND, itaanza rasmi Msimu wake Mpya wa 2017/18 Ijumaa Agosti 11 kwa Mechi moja tu huko Emirates Jijini London kati ya Arsenal na Mabingwa wa zamani wa England Leicester City.

Tangu Msimu uliopita, EPL ilikuwa ikitumia Ijumaa kadhaa kwa Mechi zake chache lakini Msimu huu Mpya unaokuja Mechi za Ijumaa zimeongezeka baada ya Makampuni ya TV yenye haki ya kuonyesha Mechi Mubashara kuketi na Wasimamizi wa EPL kupangua na kupanga upya Ratiba hasusan Mechi zipi zitarushwa laivu huko England.

Baada ya Mechi hiyo ya Ijumaa, Jumamosi zipo Mechi 7 ambapo mojawapo ni Mabingwa Watetezi Chelsea kuanza utetezi wao wakiwa kwao Stamford Bridge dhidi ya Burnley.

Jumapili zipo Mechi Mechi 2 na ya kwanza ni kati ya Timu iliyopanda Daraja Newcastle United ambao watakuwa kwao Saint James Park kuivaa Timu iliyomaliza Nafasi ya Pili Msimu uliopita Tottenham Hotspur.

Kisha itafuata Mechi itakayopigwa Old Trafford kati ya Manchester United na West Ham United.

EPL, LIGI KUU ENGLAND – Ratiba Mechi za Wikiendi ya Kwanza ya Ufunguzi

**Saa za Bongo

Ijumaa Agosti 11

2145 Arsenal v Leicester City

Jumamosi Agosti 12

1430 Watford v Liverpool

**Zote Saa 11 Jioni

Chelsea v Burnley

Crystal Palace v Huddersfield Town

Everton v Stoke City

Southampton v Swansea City

West Bromwich Albion v AFC Bournemouth

1930 Brighton & Hove Albion v Manchester City

Jumapili Agosti 13

1530 Newcastle United v Tottenham Hotspur

1800 Manchester United v West Ham United