FIFA KOMBE LA MABARA: PORTUGAL, MEXICO SULUHU!

FIFACONFED17 RONALDOLEO Portugal na Mexico zimetoka Sare 2-2 katika Mechi ya Kundi A la Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara, Mashindano ambayo huandaliwa Mwaka Mmoja kabla ya Fainali za Kombe la Dunia kwenye Nchi ambayo ndiyo Wenyeji wa Fainali hizo.

Mechi hiyo ilichezwa Kazan Arena, Mjini Kazan huko Russia na Portugal, Mabingwa wa Ulaya ndio walitangulia kupata Bao Dakika ya 34 kupitia Ricardo Quaresma alielishwa na Cristiano Ronaldo na Mexici kusawazisha Bao Dakika ya 42 kupitia Javier Hernandez ‘Chicharito’ alieunganisha kwa Kichwa Krosi ya Carlos Vela.

Portugal walikwenda mbele 2-1 Dakika ya 86 kwa Bao la Cedric Soares na Mexico kusawazisha tena kwa Bao la Dakika ya 91 la Hector Moreno.

Hadi Mwisho, Portugal 2 Mexico 2, Matokeo ambayo yamewaacha Wenyeji Russia waongoze Kundi A kwani Jana waliichapa New Zealand 2-0.

Baadae Leo ipo Mechi ya kwanza ya Kundi B kati ya Cameroun na Chile itakayochezwa huko Spartak Stadium, Moscow.

Kesho Jumatatu pia ipo Mechi moja ya Kundi B kati ya Mabingwa wa Dunia Germany na Australia.

VIKOSI:

Portugal: Rui Patrício, Soares, Pepe, Fonte, Guerreiro, Quaresma [Valente Silva 82'], João Moutinho [Adrien Silva 58'], Carvalho, André Gomes, Nani [Batalha Martins 58'], Ronaldo

Mexico: Ochoa, Salcedo [Araújo 67'minutes], Reyes, Moreno, Layún, dos Santos, Herrera, Guardado, Vela [dos Santos 57'], Jiménez [Peralta 79'], Hernández

REFA: Néstor Pitana [Argentina]

++++++++++++++++

FIFA KOMBE LA MABARA

Ratiba/Matokeo:

Hatua ya Kwanza

Jumamosi Juni 17

KUNDI A

Saint Petersburg Stadium, Saint Petersburg

Russia 2 New Zealand 0

Jumapili Juni 18

KUNDI A

Kazan Arena, Kazan

Portugal 2 Mexico 2

KUNDI B

Spartak Stadium, Moscow

2100 Cameroon v Chile 

Jumatatu Juni 19

KUNDI B

Fisht Stadium, Sochi

1800 Australia v Germany

Jumatano Juni 21

KUNDI A

Spartak Stadium, Moscow

1800 Russia v Portugal

Fisht Stadium, Sochi

2100 Mexico v New Zealand

Alhamisi Juni 22

KUNDI B

Saint Petersburg Stadium, Saint Petersburg

1800 Cameroon v Australia

Kazan Arena, Kazan

2100 Germany v Chile

Jumamosi Juni 24

KUNDI A

Kazan Arena, Kazan

1800 Mexico v Russia

Saint Petersburg Stadium, Saint Petersburg

1800 New Zealand v Portugal

Jumapili Juni 25

KUNDI B

Fisht Stadium, Sochi

1800 Germany v Cameroon

Spartak Stadium, Moscow

1800 Chile v Australia

Hatua ya Pili

Nusu Fainali

Jumatano Juni 28

Kazan Arena, Kazan

2100 Mshindi Kundi A v Mshindi wa Pili Kundi B [NF1]

Alhamisi Juni 29

Fisht Stadium, Sochi

2100 Mshindi Kundi B v Mshindi wa Pili Kundi A [NF2]

Mshindi wa 3

Jumapili Julai 2

Spartak Stadium, Moscow

1500 Atakaefungwa NF1 v Atakaefungwa NF2

FAINALI

Jumapili Julai 2

Saint Petersburg Stadium, Saint Petersburg

2100 Mshindi NF1 v Mshindi NF2

Habari MotoMotoZ