JOE HART MASHAKANI, COSTA AIBWAGIA ZIGO CHELSEA KUAMUA!

PATA FUPI ZILIZOBAMBA:
KIPA JOE HART MASHAKANI! 
COSTA-HARTKIPA wa England Joe Hart ambae Klabu yake ni Manchester City ambayo imemtoa kwa Mkopo huko Torino ya Italy amedai hajapata Ofa toka kokote.
Hart, mwenye Miaka 30, alikaa Msimu mzima uliopita kwa Mkopo huko Torino na sasa ameambiwa yuko huru kuondoka City na Meneja Pep Guardiola.
Guardiola hakumtaka Hart tangu atue hapo City mwanzoni mwa Msimu uliopita na alimleta Claudio Bravo kumbadili Kipa huyo wa England na Wiki hii kumnunua Kipa wa Brazil Ederson Moraes kutoka Benfica kwa Dau kubwa la Pauni Milioni 35.
COSTA: "CHELSEA ITAAMUA!"
STRAIKA wa Chelsea Diego Costa, mwenye Miaka 28,  ambae Juzi alidai Meneja Antonio Conte alimtumia ujumbe wa Simu kuwa hatakiwi sasa amedai Klabu hiyo ndio itaamua nini hatima yake.
Ameeleza: "Sijuo hatima yangu. Nina Mkataba na Chelsea na wao ndio wataamua!"
Jana Costa ndie aliifungia Spain Bao la ushindi walipoifunga Macedonia 2-1 huko Skopje kwenye Mechi ya Kundi G la Nchi za Ulaya kuwania kucheza Kombe la Dunia huko Russia Mwaka 2018.
Bao la Kwanza la Spain lilifungwa na David Silva.
Spain ndio wanaongoza Kundi G wakiwa Pointi sawa na Italy ambao Jana waliibamiza Liechtenstein Bao 5-0.
 

  
 

Habari MotoMotoZ