KOMBE LA DUNIA 2018 – MAKUNDI ULAYA: LEO MACEDONIA v SPAIN, ITALY v LIECHTENSTEIN!

WC-RUSSIA2018-LOGO-FBLEO Spain na Italy, ambazo zote ziko Kundi G la Nchi za Ulaya kuwania kutinga Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 zitakazochezwa huko Russia, zipo dimbani kucheza Mechi zao za 6.
Spain wamefungana kwa Pointi na Italy, zote zina Pointi 13 kila mmoja, lakini Spain wako juu kwa Ubora wa Magoli.
Hii Leo Spain wako Ugenini kucheza na Macedonia ambao wapo Nafasi ya 5 na wana Pointi 3.
Italy wapo Nyumbani kucheza na Liechtenstein ambao wako mkiani na wana Pointi 0.

++++++++
JE WAJUA?
-Ulaya itakuwa na Nafasi 13 kwenye Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia
-Washindi wa Makundi 9 watatinga moja kwa moja Fainali za Kombe la Dunia
-Washindi wa Pili 8 Bora toka Makundi hayo 9 watacheza Mechi za Mchujo kupata Washindi Wanne kwenda Fainali za Kombe la Dunia
++++++++
Mechi nyingine ya Kundi G ni kati ya Israel, walio Nafasi ya 3 na wana Pointi 9, wakicheza na Albania ambao wako Nafasi ya 4 na wana Pointi 6.
KOMBE LA DUNIA 2018 – MAKUNDI ULAYA
Ratiba:
**Saa za Bongo
Jumapili Juni 11
19:00 0Moldova v Georgia [Kundi D]
19:00 Finland v Ukraine [Kundi I]
19:00 0Ireland v Austria [Kundi D]
21:45 Israel v Albania [Kundi G]
21:45 Iceland v Croatia [Kundi I]
21:45 Macedonia v Spain [Kundi G]
21:45 Italy v Liechtenstein [Kundi G]
21:45 Serbia v Wales Kundi D]
21:45 Kosovo v Turkey [Kundi I]

Habari MotoMotoZ