LEO NI SUPERCLÁSICO – NI BRAZIL BILA NEYMAR V ARGENTINA YENYE MESSI!

LEO, Saa 7 Dakika 5 Mchana, Saa za Bongo, Watani wa Jadi toka Marekani ya Kusini, Brazil na Argentina, wanapambana kwenye Mechi ya Kirafiki huko Melbourne Cricket Ground Nchini Australia.

BRAZIL-ARGENTINAMechi kati ya Nchi hizi hubatizwa Jina ‘Superclasico de las Americas’.

Mechi hii ni ya Kirafiki, tena Brazil itacheza bila Staa wao mkubwa Neymar ambae amepewa Mapumziko, lakini imeleta mvuto mkubwa Duniani na hasa Wadau wakitaka kuiona Argentina chini ya Kocha Mpya Jorge Sampaoli itafanya nini.

Mara ya mwisho kwa Timu hizi kukutana ni Novemba huko Belo Horizonte Nchini Brazil kwenye ya Kundi la Nchi za Marekani ya Kusini kusaka kufuzu Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 na Brazil kuinyuka Argentina 3-0 kwa Bao za Coutinho, Neymar na Paulinho.

Ili kuikabili nguvu ya Brazil inayocheza Kitimu zaidi, Kocha Sampaoli, ambae ametokea kuzifundisha Timu ya Taifa ya Chile na Klabu ya Spain Sevilla, amebuni Mfumo Mpya kabisa wa 3-4-3 kwa Argentina huku akitumia Mtu 3 za Fowadi Lionel Messi, Paulo Dybala na Gonzalo Higuain.

Sampaoli amesisitiza Mfumo huo, hasa Wachambuzi wanadai ni 3-4-2-1, utamfungua Staa wao mkubwa Lionel Messi na kumpa uhuru kuhaha mbele Uwanja mzima.

Sampaoli amenena: “Lazima Argentina tutafute kitu kinachofanana na Staili ya Barcelona ili Messi acheze vizuri!”BRAZIL-ARGENTINA-6-ZILIZOPITA

Hii ni Mechi ya kwanza kwa Sampaoli baada ya kumrithi Edgardo Bauza aliefukuzwa Mwezi Aprili baada Argentina kunyukwa 2-0 na Bolivia na kuachwa wapo Nafasi ya 5 kwenye Kanda ya Nchi za Marekani ya Kusini kusaka kufuzu Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huku wakibakisha Mechi 4 tu.

Kanda hiyo, ambapo Timu 4 hufuzu moja kwa moja nay a 5 kwenda Mchujo, inaongozwa na Brazil ambao tayari washafuzu Fainali za Kombe la Dunia wakiwa na Mechi 4 mkononi.

Kwa upande wa Brazil chini ya Kocha Tite ambae mambo yake ni burdani tangu atwae wadhifa, wameamua kuwapumzisha Wachezaji wao kadhaa wakiwemo Neymar, Fowadi wa Liverpool Roberto Firmino, na Mabeki Dani Alves, Marcelo na Marquinhos.

Lakini Kikosini wamo Wachezaji Wawili wa Chelsea, David Luiz na Willian, Wawili wa Man City, Fernandinho na Gabriel Jesus, pamoja na Fowadi wa Liverpool Philippe Coutinho.

Kipa Mpya Ederson, aliesainiwa kutoka Benfica Jana Alhamisi, ataikosa Mechi hii baada kuruhusiwa kutoka Kambini kuhudhuria kuzaliwa kwa Binti yake.

VIKOSI VILIVYOTEULIWA AWALI:

BRAZIL

Makipa: Diego Alves (Valencia), Weverton (Atletico Paranaense), Ederson (Benfica/Man City)
Mabeki: Alex Sandro (Juventus), David Luiz (Chelsea), Fagner (Corinthians), Filipe Luis (Atletico Madrid), Gil (Shandong Luneng), Jemerson (Monaco), Rafinha (Bayern Munich), Rodrigo Caio (Sao Paulo), Thiago Silva (Paris Saint-Germain)
Viungo: Fernandinho (Manchester City), Giuliano (Zenit St Petersburg), Lucas Lima (Santos), Paulinho (Guangzhou Evergrande), Philippe Coutinho (Liverpool), Renato Augusto (Beijing Gouan), Rodriguinho (Corinthians), Willian (Chelsea)
Mafowadi: Diego Souza (Sport), Douglas Costa (Bayern Munich), Gabriel Jesus (Manchester City), Taison (Shakhtar Donetsk)

ARGENTINA

Makipa: Sergio Romero (Manchester United), Nahuel Guzman (Tigres), Geronimo Rulli (Real Sociedad)

Mabeki: Javier Mascherano (Barcelona), Emanuel Mammana (Lyon), Gabriel Mercado (Sevilla), Nicolas Otamendi (Manchester City)
Viungo: Eduaro Salvio (Benfica), Lucas Rodrigo Biglia (Lazio), Ever Banega (Inter Milan), Manuel Lanzini (West Ham United), Leandro Paredes (Roma), Guido Rodriguez (Tijuana)
Mafowadi: Leo Messi (Barcelona), Gonzalo Higuain (Juventus), Joaquin Correa (Sevilla), Alejandro Dario Gomez (Atalanta), Mauro Icardi (Inter Milan), Angel Di Maria (Paris Saint-Germain), Paulo Dybala (Juventus)

Habari MotoMotoZ