JESUS NJE MIEZI KADHAA, AVUNJIKA MFUPA MGUUNI!

IMG-20170215-WA0000FOWADI mpya wa Manchester City kutoka Brazil Gabriel Jesus amevunjika Mfupa wa Mguu wake wa Kulia na sasa huenda akawa nje kwa Miezi kadhaa.City imethibitisha hilo lakini imeeleza anapaswa kuchunguzwa zaidi ili kupata undani.Jesus, mwenye Miaka 19, aliumia Juzi Jumatatu Usiku City ilipoifunga Bournemouth 2-0 huko Vitality Stadium kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England.Jesus aliumia na kutolewa nje kwenye Dakika ya 15.Inaaminika Jesus amevunjika mmoja wa ile Mifupa Mitano ya inayounganisha Kifundo cha Enka na Vidole vya Mguu (Metatarsal).Jesus, ambae alihamia rasmi City akitokea Palmeiras ya Brazil Januari kwa Dau la Pauni Milioni 27, ameichezea City Mechi 5 na kufunga Bao 2 akichukua Namba ya Sentafowadi wa Argentina Sergio Aguero.Straika huyo alikuwa mbioni kuifikia Rekodi ya City ya kuwa Mchezaji wa 3 mpya aliefunga Bao katika kila Mechi katika Mechi zake 3 za mwanzo za Ligi.Wanaoshikilia Rekodi hiyo ya City ni Straika wao wa zamani Emmanuel Adebayor na Mchezaji wao wa sasa.Kevin de Bruyne.