VPL: LEO SIMBA KUIFUNGA PRISONS NA KUITOA YANGA KILELENI?

VPL-DTB-SITSIMBA hii Leo wana nafasi murua ya kutwaa uongozi wa VPL, Ligi Kuu Vodacom, ikiwa wataifunga Tanzania Prisons kwenye Mechi itakayochezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Ushindi kwa Simba, chini ya Kocha kutoka Cameroon Joseph Omog, utawafanya wawe na Pointi 51 na kuwatoa Yanga, walio na Pointi 49, uongozini.

Wikiendi hii Yanga hawachewzi VPL kwa vile Jumapili wako huko Comoro kucheza na Ngaya kwenye Mechi yao ya Kwanza ya Raundi ya Awali ya CAF CHAMPIONZ LIGI.

Simba watatinga kwenye Mechi hii wakiwa na ari kubwa kwani, baada ya kuyumba kwa kipigo, waliibuka Wikiendi iliyopita kwa kuitwanga Majimaji 3-0 huko Songea.

Leo pia zipo Mechi nyingine 3 za VPL ambazo Stand United watakuwa wenyeji wa Majimaji y Songea kwenye Uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga wakati Ndanda FC ikiialika Toto Africans kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara na Ruvu Shooting ikichea na Azam FC kwenye Uwanja wa Mabatini, Pwani.

Jumapili, Mwadui FC itacheza Mbeya City kwenye Uwanja wa Mwadui wakati African Lyon itacheza na Mtibwa Sugar Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na pia JKT Ruvu itakuwa mwenyeji wa Mbao FC kwneye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.

VPL-FEB10

VPL – Ligi Kuu Vodacom

Ratiba

Jumamosi Februari 11 

Stand United vs Majimaji

Simba vs Tanzania Prisons

Ndanda FC vs Toto African

Ruvu Shooting vs Azam FC

Jumapili Februari 12

Mwadui vs Mbeya City

African Lyon vs Mtibwa Sugar

JKT Ruvu vs Mbao FC