EPL 4 BORA: CHELSEA BINGWA MTARAJIWA, SPURS, CITY, LIVERPOOL, ARSENAL NA MAN UNITED NANI NDANI NANI NJE?

EPL-SOKATAMU-SITUPO mjadala mkali miongoni mwa Wachambuzi wa Soka huko England kuhusu Timu zipi 4 zitakuwemo kwenye 4 Bora ya EPL, Ligi Kuu England, mwishoni mwa Msimu.
Wengi wa Wachambuzi hao tayari wanaipa Chelsea Ubingwa kwa vile inaongoza Ligi hii kwa muda mrefu na sasa wapo Pointi 9 mbele ya Timu ya Pili Tottenham Hotspur.
Lakini ni Pointi 5 tu zinaitenganisha Spurs walio Nafasi ya Pili na Manchester United ambao ni wa 6 huku Manchester City, Arsenal na Liverpool wakishikilia Nafasi za 3 hadi ya 5.
Swali kubwa waliopewa Wachambuzi wakubwa wa SKY SPORTS TV ya huko England ni huku kila Timu imebakisha Mechi 14 kumaluza Ligi je Timu zipi 4 zitafuzu 4 Bora na kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao?
YAFUATAYO NI MAONI YA WACHAMBUZI HAO:
Matt Le Tissier:
-Nadhani njiani Chelsea watapepesuka kidogo lakini watakuwa Mabingwa. 
4 Bora watakuwemo pia Manchester City na Tottenham pamoja na Manchester United ambao wako kwenye wimbi refu la kutofungwa.
Le Tiss - Ubashiri wake: Chelsea Namba 1, Manchester City 2, Tottenham 3, Manchester United 4.
Phil Thompson
-Ni ngumu kwa sasa na Arsenal au Man United wanaweza kirahisi kuwa wa Pili na wa 3.
Thompson - Ubashiri wake: Chelsea 1, Manchester City 2, Tottenham 3, Liverpool 4.
Charlie Nicholas
-Sasa inaanza kuvutia na Arsenal kila mara wako hivi wanateleza lakini wanakuwemo 4 Bora.
Kwa hali ilivyo Chelsea ni Bingwa na Man City ambae sasa wana Gabriel Jesus wamo. Nadhani Spurs pia watakuwemo.
Charlie - Ubashiri wake: Chelsea 1, Manchester City 2, Tottenham 3, Arsenal 4.
Paul Merson
-Nadhani Chelsea watatwaa Ubingwa. Tizama walichokifanya kwa Timu za nje ya 6 Bora wakishinda 15 na Sare 1 tu na sasa wamebakisha Mechi 2 tu dhidi ya Timu zilizomo 6 Bora.
Merson - Ubashiri wake: Chelsea 1, Tottenham 2, Manchester City 3, Manchester United 4
EPL – Ligi Kuu England
Ratiba
Jumamosi Februari 11
1530 Arsenal v Hull City             
1800 Manchester United v Watford          
1800 Middlesbrough v Everton    
1800 Stoke City v Crystal Palace           
1800 Sunderland v Southampton
1800 West Ham United v West Bromwich Albion                 
2030 Liverpool v Tottenham Hotspur        
Jumapili Februari 12
1600 Burnley v Chelsea    
1900 Swansea City v Leicester City           
Jumatatu Februari 13
2300 Bournemouth v Manchester City