EPL: MTU 10 CITY YASHINDA, LIVERPOOL YAPIGWA KABALI KWA PENATI 2!

EPL – Ligi Kuu England

Ratiba/Matokeo:

**Saa za Bongo  

Jumatatu Januari 2

Middlesbrough 0 Leicester City 0           

Everton 3 Southampton 0           

Manchester City 2 Burnley 1                 

Sunderland 2 Liverpool 2            

West Bromwich Albion 3 Hull City 1                

2015 West Ham United v Manchester United

+++++++++++++++++++++++++++++

SUN-LIVEREPL, Ligi Kuu England, imeendelea Leo kwa Mechi 5 na ya 6 kuchezwa baadae Usiku huu.

Ifuatayo ni Taarifa fupi kwa Mechi za Liverpool na Man City.

SUNDERLAND 2 LIVERPOOL 2

Penalti 2 za Jermain Defoe zimeifanya Sunderland kutoka nyuma mara 2 na kuambua Pointi 1 walipotoka Sare na Liverpool 2-2.

Liverpool walitangulia kufunga Dakika ya 19 kwa Bao la Daniel Sturridge la Kichwa alipounganisha shuti fyongo la Dejan Lovren.

Sunderland walisawazisha Dakika ya 25 kwa Penati iliyotolewa baada ya Ragnar Klavan kumwangusha Didier Ndong na Jermaine Defoe kufunga Penati hiyo.EPL-JAN2A

Lakini, Dakika ya 72, Sadio Mane akaipeleka Liverpool 2-1 mbele na Sunderland kusawazisha Dakika ya 84 kwa Penati nyingine iliyotolewa baada ya Mane kuinawa Frikiki na Defoe kufunga tena.

Matokeo haya yamewabakisha Liverpool Nafasi ya Pili wakiwa Pointi 5 nyuma ya Vinara Chelsea na Pointi 2 mbele ya Timu ya 3 Man City.

Sunderland wao wamebaki Nafasi ya 18.

VIKOSI:

Sunderland: Mannone, Love, O’Shea, Djilobodji, Van Aanholt, Larsson, Ndong, Rodwell, Januzaj, Defoe, Borini.

Akiba: Khazri, Mika, Manquillo, Maja, Honeyman, Embleton, Ledger.

Liverpool: Mignolet, Clyne, Lovren, Klavan, Milner, Can, Wijnaldum, Lallana, Mane, Firmino, Sturridge.

Akiba: Karius, Moreno, Lucas, Origi, Stewart, Ejaria, Alexander-Arnold.

REFA: Anthony Taylor

MANCHESTER CITY 2 BURNLEY 1

Mtu 10 Man City wameweza kuishinda 2-1 Burnley licha ya kuwa pungufu kuanzia Dakika ya 32 kufuatia Kadi Nyekundu kwa Fernandinho kwa Rafu mbaya ya Miguu Miwili aliyomchezea Johan Gudmundsson kwenye Mechi iliyochezwa Etihad.

Hiyo imekuwa Kadi Nyekundu ya 3 kwa Fernandinho katika Mechi 6 zilizopita.

Licha ya upungufu huo, City walikwenda 2-0 mbele kwa Bao za Dakika za 58 na 62 za Gael Clichy na Sergio Aguero wakati Burnley walipata Bao lao moja Dakika ya Mfungaji akiwa Ben Mee Dakika ya 70.

Matokeo haya yamewaweka City Nafasi ya 3 wakati Burnley wapo Nafasi ya 11.

VIKOSI:

Man City: Bravo, Sagna, Otamendi, Kolarov, Clichy, Toure, Fernandinho, Jesus Navas, De Bruyne, Sterling, Iheanacho.

Akiba: Zabaleta, Nolito, Aguero, Caballero, Silva, Stones, Garcia.

Burnley: Heaton, Lowton, Keane, Mee, Ward, Boyd, Hendrick, Gudmundsson, Arfield, Barnes, Gray.

Akiba: Vokes, Bamford, Defour, Robinson, Tarkowski, Darikwa, O’Neill.

REFA: Lee Mason

EPL – Ligi Kuu England

Ratiba

**Saa za Bongo  

Jumanne Januari 3

2245 Bournemouth v Arsenal                

2300 Crystal Palace v Swansea City                

2300 Stoke City v Watford          

Jumatano Januari 4

2300 Tottenham Hotspur v Chelsea