EPL: LEO LONDON STADIUM NI WEST HAM-MAN UNITED, MOURINHO KUANZA 2017 VYEMA, KUZOA USHINDI WA 6 MFULULIZO?

EPL – Ligi Kuu England

Ratiba

**Saa za Bongo  

Jumatatu Januari 2

1530 Middlesbrough v Leicester City               

1800 Everton v Southampton               

1800 Manchester City v Burnley            

1800 Sunderland v Liverpool                

1800 West Bromwich Albion v Hull City           

2015 West Ham United v Manchester United

+++++++++++++++++++++++++++++

WESTHAM-MANUNITEDLEO Vigogo wa Soka wa EPL, Ligi Kuu England, Manchester United wanatua huko London Stadium Jijini London kucheza na Timu ngumu West Ham katika Mechi ya Ligi hiyo wakiwa kwenye wimbi tamu la ushindi wa Mechi 5 mfululizo na kutofungwa katika Mechi zao 12 zilizopita.

Leo, Jose Mourinho, Meneja wa Man United, anataka kuuanza Mwaka Mpya 2017 kwa mguu mzuri kwa kusaka ushindi dhidi ya West Ham ambayo Msimu uliopita kwenye Mechi kama hii ya EPL kwenye Uwanja wao wa zamani Upton Park walishinda 3-2.

Lakini Msimu huu, Timu hizi zimeshakumbana mara 2 na Man United kutoka 1-1 na West Ham, chini ya Meneja Slaven Bilic, kwenye EPL na Siku 4 baadae kupambana kwenye Robo Fainali ya EFL CUP na Man United kuibuka kidedea kwa Bao 4-1.EPL-JAN1

Kwenye Mechi hii, Man United itamkosa Beki wao mahiri Eric Bailly ambae Jana aliondoka Kikosini kwenda kujiunga na Timu ya Taifa ya Ivory Coast kwa ajili ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2017.

Wengine wa Man United ambao hawatakuwepo ni Majeruhi Luke Shaw na wenye hatihati kucheza ni Kepteni Wayne Rooney mwenye maumivu ya Paja na Michael Carrick ambae alikuwa Mgonjwa.

Kwa upande wa West Ham, wana Wachezaji kadhaa ambao ni Majeruhi na hao ni Diafra Sakho, Arthur Masuaku, Alvaro Arbeloa na Gokhan Tore huku wenye hatihati ni Nahodha wao Mark Noble alieumizwa Juzi kwenye Mechi yao na Leicester na kulazimika kubadilishwa na pia wengine wenye hatihati ni Daniel Amartey, Byram na Zaza.

Licha ya upungufu huo, West Ham wameibuka upya hasa baada ya kurejea Kikosini mwao kwa Majeruhi Andy Carroll na Andre Ayew lakini Man United ya sasa, iliyofufuka upya baada ya kucharazwa na Chelsea Mwezi Oktoba si mchezo.

Kimsimamo kwenye EPL, Man United wapo Nafasi ya 6 wakiwa na Pointi 36 na West Ham wapo Nafasi 12 wakiwa na Pointi 22 huku zote zikiwa zimecheza Mechi 19 kila mmoja.

VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:

WEST HAM: Randolph, Nordtveit, Reid, Ogbonna, Cresswell, Lanzini, Kouyate, Antonio, Ayew, Payet, Carroll

Akiba kutokana na: Adrián, Spiegel, Feghouli, Zaza, Byram, Fletcher, Calleri, Noble

MAN UNITED: De Gea, Valencia, Jones, Rojo, Darmian, Fellaini, Herrera, Pogba, Rashford, Ibrahimovic, Martial

Akiba kutokana na: Romero, Johnstone, Depay, Fosu-Mensah, Tuanzebe, Schneiderlin, Young, Blind, Schweinsteiger, Lingard, Smalling, Mkhitaryan, Mata, Rooney, Carrick

REFA: Mike Dean

EPL – Ligi Kuu England

Ratiba

**Saa za Bongo  

Jumanne Januari 3

2245 Bournemouth v Arsenal                

2300 Crystal Palace v Swansea City                

2300 Stoke City v Watford          

Jumatano Januari 4

2300 Tottenham Hotspur v Chelsea