EPL: LIVERPOOL WAIFUNGA CITY, WAKO POINTI 6 NYUMA VINARA CHELSEA!

EPL – Ligi Kuu England

Matokeo:

Jumamosi Desemba 31

Burnley 4 Sunderland 1              

Chelsea 4 Stoke City 2               

Leicester City 1 West Ham United 0       

Manchester United 2 Middlesbrough 1             

Southampton 1 West Bromwich Albion 2         

Swansea City 0 Bournemouth 3            

Liverpool 1 Manchester City 0     

+++++++++++++++++++++++++++++

LIVER-CITY-DEC31LIVERPOOL Leo imemaliza Mwaka 2016 kwa ushindi mtamu kwao Anfield walipoitungua Manchester City 1-0 na kubaki Nafasi ya Pili kwenye EPL, Ligi Kuu England, wakiwa Pointi 6 nyuma ya Vinara Chelsea.

Kipigo hiki kimewaacha City Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 4 nyuma ya Liverpool lakini wapo hatarini Jumapili kushushwa na Arsenal na Tottenham wakishinda Mechi zao.

Bao pekee na la ushindi kwenye Mechi hiyo lilifungwa Dakika ya 8 tu kwa Krosi ya Adam Lallana iliyounganishwa kwa Kichwa safi cha Georginio Wijnaldum.

Jumapili Januari Mosi zipo Mechi 2 za EPL kwa Watford kucheza na Tottenham na kisha Arsenal na Crystal Palace.

VIKOSI:EPL-DEC31C

Liverpool: Mignolet, Clyne, Lovren, Klavan, Milner, Can, Henderson [Origi, 64’], Wijnaldum, Mane [Lucas, 89’], Lallana, Firmino.

Akiba: Karius, Sturridge, Moreno, Lucas, Origi, Ejaria, Alexander-Arnold.

Man City: Bravo, Zabaleta [Jesus Navas, 86’], Otamendi, Stones, Kolarov, Fernandinho, Toure [Iheanacho, 89’], Sterling, Silva, De Bruyne, Aguero.

Akiba: Sagna, Fernando, Caballero, Jesus Navas, Clichy, Iheanacho, Garcia.

REFA: Anthony Taylor

EPL – Ligi Kuu England

Ratiba:

**Saa za Bongo

Jumapili Januari 1

1630 Watford v Tottenham Hotspur                

1900 Arsenal v Crystal Palace               

Jumatatu Januari 2

1530 Middlesbrough v Leicester City               

1800 Everton v Southampton               

1800 Manchester City v Burnley            

1800 Sunderland v Liverpool                

1800 West Bromwich Albion v Hull City           

2015 West Ham United v Manchester United             

Jumanne Januari 3

2245 Bournemouth v Arsenal                

2300 Crystal Palace v Swansea City                

2300 Stoke City v Watford 20:00

Jumatano Januari 4

2300 Tottenham Hotspur v Chelsea