EPL: LEO MTANANGE MKUBWA FUNGA MWAKA ANFIELD, LIVERPOOL v CITY!

LIVER-CITY-DEC31WAKATI Vinara wa EPL, Ligi Kuu England, Chelsea, wakiwa na hakika ya kumaliza Mwaka huu 2016 wakiongoza Ligi, vita kubwa ipo huko Anfield hii Leo ambako Liverpool wanapambana na Manchester City kuwania nani atafunga Mwaka akiwa Nafasi ya Pili.

Chelsea wapo kileleni wakiwa na Pointi 46, Liverpool wanafuata wakiwa na Pointi 40 na City ni wa 3 wakiwa na Pointi 39.

Leo Chelsea watacheza mapema kwao Stamford Bridge na Stoke City na kuacha zigo kubwa kwa Liverpool na Man City kupigana baadae Usiku.

Kitu chema kwa City ni kurejea tena dimbani kwa Straika wao mkuu Sergio Aguero aliyekuwa Kifungoni kwa Mechi 4.EPL-DEC31A

Lakini Klabu zote zina Majeruhi kadhaa na kwa Liverpool hao ni Grujic, Coutinho, Matip, Bogdan na Ings wakati wa City ni Kompany, Delph na Gündogan.

Kwenye Mechi kama hii iliyochezwa Anfield Msimu uliopita Last season Liverpool 3 Manchester City 0.

Nini Mameneja Wameongea?

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp: "Hii ni Gemu kubwa kwa kila Timu. Klabu 6 zinagombea Nafasi 4 au moja. Kila Gemu ni kama Fainali.”

“City wana vipaji kwenye Timu yao na Benchi lao. Kitu cha maana kwetu ni kuchezea Anfield. Ni lazima tutumie hilo!”

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola: "Wao ni Wagombea Ubingwa. Nishawahi kucheza dhidi ya Jurgen Klopp, tunajuana. Anfield itawapa matumaini makubwa!”

VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:

LIVERPOOL: Mignolet, Clyne, Lovren, Klavan, Milner, Lallana, Henderson, Wijnaldum, Mane, Origi, Firmino

Akiba: Karius, Manninger, Can, Sturridge, Moreno, Lucas, Stewart, Randall, Brannagan, Ejaria, Gomez, Woodburn, Alexander-Arnold

MAN CITY: Bravo, Sagna, Otamendi, Stones, Clichy, Fernandinho, Toure, Silva, Sterling, Aguero, De Bruyne

Akiba: Caballero, Gunn, Navas, Adarabioyo, Nolito, Garcia, Maffeo, Tasende, Kolarov, Fernando, Iheanacho, Zabaleta

REFA: Craig Pawson

EPL – Ligi Kuu England

Ratiba/Matokeo:

**Saa za Bongo

Ijumaa Desemba 30

Hull City 2 Everton 2                  

Jumamosi Desemba 31

1800 Burnley v Sunderland         

1800 Chelsea v Stoke City          

1800 Leicester City v West Ham United           

1800 Manchester United v Middlesbrough                 

1800 Southampton v West Bromwich Albion              

1800 Swansea City v Bournemouth                 

2030 Liverpool v Manchester City         

Jumapili Januari 1

1630 Watford v Tottenham Hotspur                

1900 Arsenal v Crystal Palace               

Jumatatu Januari 2

1530 Middlesbrough v Leicester City               

1800 Everton v Southampton               

1800 Manchester City v Burnley            

1800 Sunderland v Liverpool                

1800 West Bromwich Albion v Hull City           

2015 West Ham United v Manchester United             

Jumanne Januari 3

2245 Bournemouth v Arsenal                

2300 Crystal Palace v Swansea City                

2300 Stoke City v Watford 20:00

Jumatano Januari 4

2300 Tottenham Hotspur v Chelsea