MOURINHO: ‘JANUARI HATOKI MTU KWA MKOPO ISIPOKUWA…….!!’

MANUNITED-MOU-BLACKBOSI wa Manchester United Jose Mourinho amesema ni Kipa chipukizi Sam Johnstone pekee ndio ataruhusiwa kuondoka kwa Mkopo Mwezi Januari.

Januari Mosi hadi 31 ndio Dirisha la Uhamisho litakuwa wazi rasmi na hapo Wachezaji wanaweza Kuuzwa, Kununuliwa au Mkopo kukubaliwa.

Wachezaji kadhaa wa Man United, hasa Morgan Schneiderlin, Memphis Depay na Anthony Martial, ambao hawana nafasi za kudumu wamekuwa wakihusishwa na kuihama Old Trafford, hasa kwa Mkopo.

Lakini Jose Mourinho ametoboa kuwa ni Sam Johnston, mwenye Miaka 23, ambae hajawahi kuichezea Timu ya Kwanza, ndie pekee ataruhusiwa kuondoka kwa Mkopo huku Stoke, Sunderland na Aston Villa zikimtaka.

Mourinho, akiwa na Kipa Namba Wani David De Gea na Rizevu Sergio Romero, ameeleza: “Sam Johnstone pekee ndio nitamruhusu kuondoka kwa Mkopo kwa sababu hachezi na anahitajika kucheza. Tunae Kipa mwingine Chipukizi Joel Pereira ambae amecheza kwa Miezi 6 huko Ligi Kuu ya Ureno na sasa zamu ya Sam kucheza Miezi 6. Huo ndio Mkopo pekee tutakaofanya!”

Mourinho aliongeza: “Mbali ya hilo, sitaki kuuza Wachezaji, Klabu, Bodi wote wanakubaliana na mimi. Lakini kama nlivyosema awali, ikiwa Mchezaji hapati Dakika za kucheza nyingi, na akitaka kuondoka, hatuna haki ya kumzuia, hasa ikiwa maslahi yenyewe ni kama tunayoyataka!”

Alimalizia: “Hadi sasa, hatujapata hata Ofa moja ambayo tunaweza kuikubali!”

Inadaiwa Wiki iliyopita West Bromwich Albion walitoa Ofa inayoaminika kuwa ni Pauni Milioni 18 kumnunua Morgan Schneiderlin na sasa itabidi waongeze Dau hilo kukidhi matakwa ya Man United.

Habari MotoMotoZ