MAN UNITED KUTOMSAINI VICTOR LINDELOF!

Manchester United haitamsaini Beki wa Benfica VICTOR-LINDELOF kwenye Dirisha la Uhamisho la Januari kama ilivyokuwa ikivumishwa Mitandaoni.

Ripoti hizo zilidai Meneja wa Man United Jose Mourinho alikuwa akitaka kumsaini Beki huyo kutoka Sweden mwenye Miaka 22.

Habari za hivi Leo kutoka England, hasa BBC, Shirika la Habari la Uingereza, zimetoboa kuwa kucheza vizuri kwa Masentahafu Wawili, Phil Jones na Marcos Rojo, kumemfanya Mourinho kukubali kutosajili Beki yeyote kwenye Dirisha hilo la Januari.

Tangu Rojo na Jones waanze kucheza pamoja dhidi ya Swansea Novemba 6 waliposhinda 3-1, Man United haijafungwa katika Mechi 11 na wamebakiza Mechi 1 tu kuifikia Rekodi iliyowekwa chini ya Meneja Mstaafu Lejendari Sir Alex Ferguson.

Rojo na Jones wamecheza pamoja Mechi 9 kati ya hizo 11 na kuruhusu Bao 7 tu.

Wachezaji wengine wa Man United wanaoweza kucheza nafasi hizo ni Eric Bailly, Chris Smalling na Daley Blind.

Pengine kuacha kwa Man United kumchukua Lindelof pia kumechangiwa mno na Benfica kuwa na tamaa ya Fisi ya kutaka ‘kuizika’ Klabu ya Sweden Vasteras na pia kuikamua Man United baada ya Jarida la huko Ureno, O Jogo, kuripoti kuwa Benfica wanataka Lindelof asaini Mkataba Mpya ili Dau la Kuhama liwe Pauni Milioni 50 na pia kuidhibiti Klabu ya kwanza ya Lindelof, Vasteras, ambako ndio Lindelof alikonunuliwa na Benfica, kufaidika na Mkataba waliomuuza Lindelof.

Vasteras wana haki ya kulipwa Malipo kadhaa kwa Benfica kumtumia Mchezaji huyo kwenye Ligi na UEFA CHAMPIONZ LIGI baada ya kufikisha Mechi kadhaa kama Mkataba wa Uhamisho kutoka Vasteras kwenda Benfica unavyotamka ambao pia unawataka Benfica kulipa Asilimia 10 ya Mauzo ya Mchezaji huyo kwa Klabu nyingine.

Inaaminika baada ya Benfica kupanchi kukidhi matakwa ya Mkataba huo mvutano kati ya Vasteras na Benfica sasa umetua FIFA.