MAN UNITED WAKAMILISHA KUMSAINI LINDELOF, SEMEDO NJIANI!

>SIR ALEX MAZOEZINI, MOURINHO ATOBOA!

MANUNITED-FERGIE-MOUMANCHESTER UNITED wamekamilisha kumsaini Victor Lindelof na wapo njiani kukamilisha dili ya kumsaini Nelson Semedo kwa mujibu wa ripoti kutoka Portugal.

Lindelof, Mchezaji wa Kimataifa wa Sweden mwenye Miaka 22, amekuwa na Benfica ya Ureno tangu 2012 na anatarajiwa kuigharimu Man United Pauni Milioni 38.

Straika wa Man United Zlatan Ibrahimovic aliekuwa akicheza na Lindelof Timu ya Taifa ya Sweden amesema Beki huyo ni jembe kali.

Inadaiwa akiwa Man United Lindelof atapewa Jezi Namba 2 ambayo mara ya mwisho ilivaliwa na Mbrazil Rafael Mwaka 2015 baada ya kuirithi toka kwa Fulbeki Lejendari Gary Neville.

Vyanzo vya habari hizi pia vimetoboa kuwa Man United wako njiani kukamilisha dili ya kumchukua Mchezaji mwingine Beki wa Benfica Nelson Semedo, mwenye Miaka 23, lakini atabakia huko huko Benfica hadi mwishoni mwa Msimu huu.

FERGIE MAZOEZINI MAN UNITED!

MENEJA wa Man United Jose Mourinho ametoboa kuwa Bosi wa zamani wa Timu hiyo Lejendari Sir Alex Ferguson hivi karibuni amekuwa akienda Kambi ya Mazoezi ya Timu hiyo huko Carrington Jijini Manchester.

Ferguson, ambae alistaafu kuwa Meneja wa Man United Mwaka 2013 baada ya kuitumikia Klabu hiyo kwa Miaka 26, hajawahi kutua Carrington tangu alipostaafu.

Mourinho, akiongea na Jarida la Mashabiki wa Man United lijulikanalo kama United We Stand, alieleza: “Alikuwa hajarudi tangu aondoke lakini nimemrudisha tena kwa Watu wake, kuwaona Watu aliofanya nao kazi kwa Miaka mingi, kuangaliza Mazoezi yetu.”

Aliongeza: “Nilitaka Wachezaji wamuone Mtu huyu mkubwa na kwangu kuwa nae, kula nae chakula. Nilifurahia, nae alifurahia!”

Mourinho alibainisha: “Mimi ni Mtu ambae sioni Mizimu. Naheshimu ya nyuma na najua anaipenda mno Klabu. Tuna uhusiano mzuri nae na najua hii ni Nyumba yake. Akitaka kuja hapa, Vyumba vya Kubadili Jezi, kuwaona Wachezaji Mazoezini, anajua anakaribishwa mno!”

 

Habari MotoMotoZ