EPL: SANE NA STERLING WAICHAKAZA ARSENAL HUKO ETIHAD!

EPL LIGI KUU ENGLAND

Matokeo:

Jumapili Desemba 18

Bournemouth 1 Southampton 3  

Manchester City 2 Arsenal 1

Tottenham Hotspur 2 Burnley1

++++++++++++++++++++++

CITY-STERLING-SANEManchester City Leo huko kwao Etihad wametoka nyuma kwa Bao 1-0 na kuitandika Arsenal 2-1 katika Mechi ya EPL, Ligi Kuu England.

Hiki ni kipigo cha Pili mfululizo kwenye EPL kwa Arsenal baada ya Majuzi kupigwa 2-1 huko Goodison Park mikononi mwa Everton.

Sasa Arsenal wameporomoka hadi Nafasi ya 4 wakiwa nyuma ya Liverpool, Man City na Vinara Chelsea.

Hii Leo, Arsenal walitangulia kufunga katika Dakika ya 5 kwa Bao la Theo Walcott ambalo lilidumu hadi Haftaimu.

Kipindi cha Pili Man City walikuja wapya na kuirudisha Arsenal nyuma na Dakika ya 47 kusawazisha kwa Bao la Leroy Sane.

Bao la ushindi kwa City lilifungwa Dakika ya 71 na Raheem Sterling huku David Silva akionekana kuwa Ofsaidi akimkaribia Kipa Petr Cech na hilo bila shaka litawafanya Arsenal kulalamikia Bao hilo.EPL-DES18

Kwenye Mechi nyingine za EPL hii Leo, Tottenham iliichapa Burnley 2-1 na mapema Southampton kuibomoa Bournemouth 3-1.

Kesho Jumatatu Usiku ipo Mechi moja Usiku huko Goodison Park kati ya Everton na Liverpool ikiwa ni Dabi ya Merseyside.

VIKOSI:

Man City:Bravo, Zabaleta, Otamendi, Kolarov, Clichy, Fernando, Sané, Touré, Silva, De Bruyne, Sterling

Akiba: Sagna, Nolito, Caballero, Jesus Navas, Stones, Iheanacho, Garcia.
Arsenal:Cech, Bellerin, Gabriel, Koscielny, Monreal, Coquelin, Xhaka, Walcott, Özil, Iwobi, Sánchez

Akiba: Gibbs, Lucas Perez, Giroud, Ospina, Oxlade-Chamberlain, Holding, Elneny.
REFA:MARTIN ATKINSON

EPL, LIGI KUU ENGLAND

Ratiba:

**Saa za Bongo

Jumatatu Desemba 19

2300 Everton v Liverpool  

Jumatatu Desemba 26

1530 Watford v Crystal Palace              

1800 Arsenal v West Bromwich Albion            

1800 Burnley v Middlesbrough              

1800 Chelsea v Bournemouth               

1800 Leicester City v Everton               

1800 Manchester United v Sunderland            

1800 Swansea City v West Ham United           

2015 Hull City v Manchester City          

Jumanne Desemba 27

2015 Liverpool v Stoke City                  

Jumatano Desemba 28

2245 Southampton v Tottenham Hotspur                  

Ijumaa Desemba 30

2300 Hull City v Everton             

Jumamosi Desemba 31

1800 Burnley v Sunderland         

1800 Chelsea v Stoke City          

1800 Leicester City v West Ham United           

1800 Manchester United v Middlesbrough                 

1800 Southampton v West Bromwich Albion              

1800 Swansea City v Bournemouth                 

2030 Liverpool v Manchester City         

Jumapili Januari 1

1630 Watford v Tottenham Hotspur                

1900 Arsenal v Crystal Palace               

Jumatatu Januari 2

1530 Middlesbrough v Leicester City               

1800 Everton v Southampton               

1800 Manchester City v Burnley            

1800 Sunderland v Liverpool                

1800 West Bromwich Albion v Hull City           

2015 West Ham United v Manchester United             

Jumanne Januari 3

2245 Bournemouth v Arsenal                

2300 Crystal Palace v Swansea City                

2300 Stoke City v Watford 20:00

Jumatano Januari 4

2300 Tottenham Hotspur v Chelsea