RUSSIA TWAJA: BRAZIL NCHI YA KWANZA KUTINGA FAINALI KOMBE LA DUNIA 2018!

BRAZIL-NEYMAR-RIO-GOLI-REKODIAlfajiri ya Leo, Brazil wamekuwa Nchi ya Kwanza kabisa kufuzu kwenda kwenye Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia huku wakiwa wamebakiza Mechi 4 za Kundi lao la Nchi 10 za Marekani ya Kusini.

Uhakika wa hili umetimia hii Leo baada ya Brazil kuwachapa Paraguay 3-0 na Uruguay kufungwa 2-1 na Peru katika Mechi ya mwisho iliyochezwa Alfajiri ya Leo.

Sasa Brazil wanaungana na Wenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 Russia ambao wamepitishwa moja kwa moja kucheza Fainali hizo.

Kwenye Kundi la Kanda ya Nchi za Marekani ya Kusini, Brazil walifungwa Mechi yao ya kwanza kabisa na Chile lakini baada ya hapo hawakufungwa tena katika Mechi zao 13 wakishinda Mechi 10 na Sare 3 wakivuna Pointi 33 wakifuatiwa na Colombia wenye Pointi 24.

++++++++++++++++++++++++

JE WAJUA?

-CONMEBOL itatoa Nchi 4 kutinga Fainali za Kombe la Dunia huko Russia Mwaka 2018.

-Nchi hizo zinaweza kuwa 5 ikiwa Timu itakayomaliza Nafasi ya 5 kwenye Kundi lao itashinda Mechi ya Mchujo dhidi ya Timu nyingine toka Bara jingine ambayo itakuwa ni moja toka Kanda ya Oceania yenye Nchi za Visiwani ambazo ni New Zealand, New Caledonia, Fiji, Papua New Guinea, Siolomon Islands na Tahiti.

++++++++++++++++++++++++

Zikiwa zimebaki Mechi 4 kwa kila Timu, Timu nyingine ambazo zipo kwenye Nafasi za kufuzu moja kwa moja kwenda Russia ni Colombia, Uruguay na Chile.

Argentina, ambao wapo Nafasi ya 5, ikiwa watabaki Nafasi hiyo hadi mwishoni itabidi wacheze Mechi ya Mchujo na Nchi kutoka Kanda ya Oceania ili kufuzu kwenda Russia.

CONMEBOL

Kombe la Dunia – Russia 2018

Matokeo:

Jumanne Machi 28, 2017         

Bolivia 2 Argentina 0

Jumatano Machi 29, 2017         

Ecuador 2 Colombia 0

Chile 3 Venezuela 1    

Brazil 3 Paraguay 0   

Peru 2 Uruguay 1

MSIMAMO:

image011

MKWANJA BORA: RONALDO AMZIDI MESSI, MOURINHO NDIE NAMBARI WANI KWA MAKOCHA!

RONALDO-BALLONDORJARIDA la Michezo la France Football ambalo ndio Waasisi na Waendeshaji wa Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani, Ballon d'Or, wametoboa kuwa Cristiano Ronaldo ndie Mwanasoka mwenye Mapato makubwa Duniani kwa Mwaka 2016/17 huku Jose Mourinho akitamba kwa Makocha.

Ronaldo, anaechezea Real Madrid ya Spain na Timu ya Taifa ya Portugal na pia ndie alietwaa Tuzo zote Mbili za Mchezaji Bora Duniani za Ballon d'Or na ile ya FIFA, alivuna EURO Milioni 87.5 kwa 2016/17 akimzidi Lionel Messi wa Barcelona na Argentina alieambua EURO Milioni 76.5.

Mbrazil Neymar anaechezea Barcelona anashika Nafasi ya 3 akivuna EURO Milioni 55.5 wakifuatia Gareth Bale aliezoa EURO Milioni 41 na kisha Muargentina Ezequiel Lavezzi anaecheza huko China kwenye Klabu ya Hebei Fortune ambae amezoa EURO Milioni 28.5.

Kwa Makocha, Nambari Wani ni Jose Mourinho wa Manchester United aliepata EURO Milioni 28.

Hesabu za France Football zinachukulia Mapato ya Mshahara, Bonasi nay ale ya Matangazo ya Biashara kwa Msimu huu wa 2016/17.

GARETH SOUTHGATE: ROONEY BADO YUPO YUPO ENGLAND!

C3WbBDiWQAQF4S0MENEJA wa Timu yaTaifa ya England Gareth Southgate amesema Wayne Rooney anabakia kwenye mawazo yake ya Timu hiyo.
Southgate amesisitiza kuwa zama za Rooney kuichezea England hazijaisha tofauti na Vyombo vya habari Nchini humo vikidai huu ndio mwisho wake.
Rooney, mwenye Miaka 31, ndie Mfungaji Bora katika Historia ya Nchi yake pamoja na Klabu yake Manchester United lakini sasa, hasa Msimu huu, kupewa kwake Namba kumekuwa ni adimu.
Hata huko Man United zipo habari za chinichini kuwa Msimu huu ni wa mwisho kwake na ataondoka.
Lakini Jana Southgate amempa imani alipotamka: "Yeye bado yupo kwenye fikra zangu. Kwanini tuzungumzie kustaafu kwake wakati ana kila nafasi kuwemo kwenye Timu hii?"
Rooney ameichezea England Mechi 119 na yeye ndie anashika Rekodi ya kuwa Namba 2 kwa kuichezea England Mechi nyingi.
Anaeongoza kwa Mechi nyingi ni Kipa Peter Shilton aliecheza Mechi 125.
Kwenye Mechi za Wiki hii ambapo Juzi England walifungwa 1-0 na Germany kwenye Mechi ya Kirafiki na Leo wapo Wembley kucheza Mechi ya Kundi F la Ulaya la Kombe la Dunia 2018, Rooney hakuitwa Kikosini kwa vile aliumia Goti.

KOMBE LA DUNIA 2018 – MAREKANI KUSINI: BRAZIL YAITEKETEZA URUGUAY, JICHO KODO FAINALI RUSSIA!

WC-2018-SA-QUALIFIERSVINARA wa Kanda ya Marekani ya Kusini chini ya Mwamvuli wa Shirikisho lao CONMEBOL kusaka Nchi 4 zitakazotinga moja kwa moja huko Russia Mwaka 2018 kwenye Fainali za Kombe la Dunia, Brazil, wameendeleza ubabe wao kwa kuifyeka Uruguay waliokuwa kwao Montevideo Bao 4-1.

Uruguay walitangulia Bao 1-0 kwa Bao la Penati iliyofungwa Dakika ya 9 na Edinson Cavani.

Brazil walisawazisha Dakika ya 19 kwa kigongo cha Paulinho cha Mita 30 alipopokea Pasi ya Neymar.

Hadi Mapumziko, Uruguay 1 Brazil 1.

Kipindi cha Pili Dakika ya 52 Paulinho aliipa Brazil Bao la Pili na Neymar kupiga Bao tamu na la 3 kwa Brazil.

Kwenye Dakika za Majeruhi, Paulinho alipiga Bao la 4 na Brazil kushinda 4-1.

++++++++++++++++++++++++

JE WAJUA?

-CONMEBOL itatoa Nchi 4 kutinga Fainali za Kombe la Dunia huko Russia Mwaka 2018.

-Nchi hizo zinaweza kuwa 5 ikiwa Timu itakayomaliza Nafasi ya 5 kwenye Kundi lao itashinda Mechi ya Mchujo dhidi ya Timu nyingine toka Bara jingine ambayo itakuwa ni moja toka Kanda ya Oceania yenye Nchi za Visiwani ambazo ni New Zealand, New Caledonia, Fiji, Papua New Guinea, Solomon Islands na Tahiti.

++++++++++++++++++++++++

Baada ya kucheza Mechi 13, Brazil wamezidi kupaa kileleni wakiwa na Pointi 30 wakifuata Uruguay wenye 23.

Baadae huko Buenos Aires Argentina watacheza na Chile.

Raundi nyingine ya Kanda hii itaanza kuchezwa Jumanne Machi 28 na Siku inayofuatia ambapo Vinara Brazil watakuwa kwao kuivaa Paraguay.

VIKOSI:

URUGUAY (Mfumo 4-4-2): M. Silva; M. Pereira, Coates, Godin, G. Silva; Sanchez, Vecino, Arevalo, Rodriguez; Cavani, Rolan

Akiba: Gimenez, Conde, De Arrascaeta, Hernandez, Alvaro, Laxalt, Fucile, Urretaviscaya, Campana, Corujo, Stuani, Lodeiro

BRAZIL (Mfumo 4-3-3): Alisson; Alves, Marquinhos, Miranda, Marcelo; Paulinho, Casemiro, Renato; Coutinho, Neymar, Firmino

Akiba: Fagner, Dudu, Diego, Luis, Fernandinho, Ederson, Diego Souza, Willian, Gil, Silva, Giuliano, Weverton.

REFA: Patricio Loustau [Argentina]

MSIMAMO:

CONMEBOL

Kombe la Dunia – Russia 2018

Mechi za Makundi

Ratiba/Matokeo:

Alhamsi Machi 23, 2017      

Colombia 1 Bolivia 0

Ijumaa Machi 24, 2017   

Paraguay 2 Ecuador 1

Uruguay 1 Brazil 4     

Venezuela 2 Peru 2     

Argentina 1 Chile 0

**Saa za Bongo

Jumanne Machi 28, 2017         

2330 Bolivia  v Argentina

Jumatano Machi 29, 2017         

0001 Ecuador v Colombia

0100 Chile v Venezuela     

0345 Brazil v Paraguay     

0515 Peru v Uruguay        

BRAZIL: TITE AENDELEA KUZUNGUSHA UTEPE WA KEPTENI, SASA MIRANDA KUUVAA!

WC-2018-SA-QUALIFIERSBEKI wa Inter Milan Miranda ndie amepewa Utepe wa Kepteni wa Brazil wakati Ijumaa Alfajiri ikicheza Ugenini huko Mjini Montevideo na Uruguay katika Mechi ya Kundi lao la Nchi za Marekani ya Kusini ya kusaka Washiriki wa Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia.
Baada ya Kepteni wa Brazil Neymar kujiuzulu wadhifa huo Julai Mwaka Jana na tangu ashike madaraka Juni 2016 Kocha wa Brazil Tite alisema atakuwa hana Nahodha wa kudumu na badala yake kuuzungusha Utepe wa Kepteni miongoni mwa Wachezaji vingunge wa Kikosi chake.
Miranda ndie alikuwa Kepteni wa kwanza wa Kikosi cha kwanza kabisa cha Tite Brazil ilipoichapa Ecuador 3-0 huko Quito Septemba 2016.
Wengine waliowahi kuuvaa Utepe huo ni Dani Alves mara 2 (dhidi ya Colombia na  Argentina), Fernandinho (Peru), Filipe Luis (Venezuela) na Renato Augusto (Bolivia) zote zikiwa Mechi za Kundi lao za Kombe la Dunia 2018.
Pia, Robinho na Diego walikuwa ndio Manahodha Brazil ilipocheza Kirafiki na Colombia Mwezi Januari kwenye Mechi ambayo Kikosi cha Tite kiliundwa na Wachezaji waliokuwa wakicheza ndani Nchini Brazil pekee.