RIPOTI SPESHO

KLABU YA ENGLAND EVERTON KUCHEZA TANZANIA JULAI 13!

>KUMVAA BINGWA WA SportPesa SUPER CUP!

EVERTON-SPORTPESA2KLABU YA EPL, LIGI KUU ENGLAND, Everton itazuru Tanzania kucheza Mechi ya Kabla Msimu Mpya wa 2017/18 kuanza ikiwa ni moja ya matayarisho yao.EVERTON-SPORTPESA

Tripu hiyo itawafanya Everton watue Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kucheza Mechi 1 ya Kirafiki hapo Julai 13.

Mechi hiyo inatokana na mipango ya Kampuni kubwa ya Michezo ya Bahati Nasibu, SportPesa, ambayo imeingia ushirikiano na Everton hivi karibuni na pia kutua Tanzania kwa kishindo kwa kuzidhamini Klabu kadhaa kubwa zikiwemo Mabingwa Yanga, Simba na Singida United.

Ingawa Miaka ya nyuma Timu kadhaa za England zishawahi kuja kucheza Tanzania lakini Everton itakuwa Klabu ya Kwanza kabisa ya EPL kufanya hivyo.

Hapo Julai 13, Everton, chini ya Meneja Ronald Koeman, watacheza na Bingwa wa Mashindano Mapya ya SportPesa SUPER CUP ambayo yatashirikisha Klabu 4 za Kenya na 4 za Tanzania.

Everton waliingia Mkataba na SportPesa wa udhamini mapema Mwezi huu ambao pia utaifanya Everton kuvaa Jezi zenye Nembo ya SportPesa Kifuani.

SportPesa, Kampuni iliyoanzishwa Mwaka 2014, imeingia kwa kishindo kwenye Michezo hasusan Soka, ikitangaza Biashara yao ya Bahati Nasibu hasa zinazochezwa Mitandaoni.

SportPesa SUPER CUP 2017

RATIBA:

SPORTPESA-SUPERCUP 

TFF: SERENGETI BOYS UPYA, MSUVA NA MUSSA KUGAWANA BUTI YA DHAHABU!

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI  MEI 22, 2017

SERENGETI BOYS: NI KUJIPANGA UPYA
TFF-TOKA-SITSafari ya Serengeti Boys - timu ya Tanzania ya Vijana wenye umri wa miaka 17, inaendelea licha ya jana Mei 21, mwaka huu kuondolewa kwenye hatua ya makundi ya kuwania taji la Afrika hapa Port Gentil nchini Gabon.
Serengeti Boys ilifungwa bao 1-0 na Niger katika mchezo uliofanyika , hivyo kufanya matokeo ya timu zote mbili kufanana kwa pointi, idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa tangu kuanza kwa fainali hizi za AFCON, Mei 15, mwaka huu.
Serengeti Boys ilikuwa Kundi B pamoja na Mali iliyoongoza kundi hilo kwa kufikisha pointi saba, ikifuatiwa na Niger yenye pointi nne sawa na Tanzania pamoja na Angola iliyoambulia pointi moja.
Licha ya Serengeti Boys kulingana na Niger, lakini wapinzani wa Tanzania walipenya kwenda hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa faida ya ushindi katika mchezo ambao umekutanisha timu hizo.
Kanuni hiyo ya mashindano ya CAF inajieleza kuwa matokeo ya ‘head to head’ kwa maana zinapokutana timu mbili zenye uwiano wa pointi na magoli kinachoangaliwa hapo ni timu gani ilimfunga mwenzake walipokutana na ndipo matokeao hujulikana,
Kwa jana Mei 21, mwaka huu hali hiyo ilijitokeza hivyo Niger kusonga mbele kwa kuwa aliifunga Tanzania bao 1-0 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Prt Gentil nchini Gabon.
Akizungumzia matokeo hayo, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amesema: “Kuvunjika kwa koleo si mwisho wa uhunzi.”
Alizungumza hayo kwa nyakati tofauti, Malinzi alisema: “Tujipange sasa kwa yafuatayo: Michezo ya kufuzu (Qualifiers za 2019 Afcon U20  zinafanyika mwakani kuanzia mwezi June. Vijana hawa watashiriki.
“AFCON U17 finals (Fainali za AFCON za vijana wenye umri wa chini ya miaka 17) zinafanyika Tanzania mwaka 2019,” amesema Malinzi na kuongeza: “Serengeti Boys hii ya sasa inakuwa Ngorongoro Heroes (Vijana wa u20 na ikishapumzika kwa muda, itaingia tena kambini.”
Amesema kwamba vijana wa Tazania wenye umri wa chini ya miaka 15, walioko Shule za Alliance Mwanza wanakuwa Serengeti Boys wapya.
“Hakuna muda wa kusononeka ni kuchapa kazi tu. Kikubwa tunaandaa Taifa stars ya kwenda World cup 2026 na qualifiers zake zitaanza mwaka 2024. Kwa sasa timu inajiandaa kuingia kambini kwa ajili ya kuivaa Lesotho,” amesema.
Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Bakari Shime amesema timu yake imepoteza mchezo huo kwa makosa ya kimchezo na bahati haikuangiwa kwa vijana wa Tanzania katika mchezo dhidi ya Niger.
VPL: MCHEZAJI BORA WA MWEZI MEI NI MOHAMMED HUSSEIN
Mchezaji wa timu ya Simba SC, Mohamed Hussein amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom wa mwezi Mei kwa msimu wa 2016/2017.
Hussein aliwashinda wachezaji Haruna Niyonzima wa Yanga na Shabani Idd wa Azam FC. 
Katika mwezi Mei kulikuwa na raundi tatu ambazo Hussein alicheza kwa dakika zote 270 na kutoa mchango mkubwa katika kuisadia timu yake kubaki katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom.
Pia alionesha nidhamu ya hali ya juu, hivyo kutopewa onyo la aina yoyote.
Kwa kushinda tuzo hiyo, Kaseja atazawadiwa kitita cha sh. 1,000,000 (milioni moja) kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom Tanzania.
Wachezaji wengine walioshinda tuzo za mwezi za Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2016/2017 ni John Bocco wa Azam (Agosti), Shiza Kichuya wa Simba (Septemba), Simon Msuva wa Yanga (Oktoba) na Riphat Said wa Ndanda (Novemba).
Wengine ni Method Mwanjali wa Simba (Desemba), Juma Kaseja wa Kagera Sugar (Januari), Hassan Kabunda wa Mwadui (Februari), Mbaraka Yusuf wa Kagera Sugar (Machi) na Abdulrahman Musa wa Ruvu Shooting (Aprili).
MSUVA, MUSSA WAGAWANA KIATU CHA DHAHABU
Washambuliaji Abdulrahman Mussa wa Ruvu Shooting na Simon Msuva wa Yanga wameibuka wafungaji bora kwenye Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2016/2017 iliyomalizika Mei 20 mwaka huu.
Kutokana na wachezaji hao kuibuka vinara kwa ufungaji ambapo kila mmoja amefunga mabao 14, watapata zawadi ya mfungaji bora ambayo ni sh. 5,800,000 kwa kila mmoja.
Yanga imemaliza Ligi hiyo ikiwa bingwa kwa ponti 68 na kufunga jumla ya mabao 57, wakati Ruvu Shooting iliyomaliza katika nafasi ya saba kwa ponti 36 imepachika jumla ya mabao 28.
Watakabidhiwa zawadi hiyo katika hafla ya tuzo za Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2016/2017 itakayofanyika keshokutwa (Mei 24 mwaka huu) kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
…………………………………………………………………………….
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA

TOTAL U-17 AFCON GABON 2017: MALI, NIGER ZASONGA, SERENGETI BOYS NJE!

TOTAL AFCON U17 GABON2017Serengeti Boys imekosa kusinga Nusu Fainali ya TOTAL U-17 AFCON GABON 2017 na hivyo kushindwa kwenda Fainali za Kombe la Dunia baada ya Jana kufungwa 1-0 na Niger katika Mechi yao ya mwisho ya Kundi B.

Niger na Mabingwa Watetezi Mali sasa wametinga Nusu Fainali kuungana na Ghana na Guinea toka Kundi A.

Hiyo Jana, Mali iliifumua Angola 6-1 na kutwaa ushindi wa Kundi A ikiwa na Pointi 7 wakati Niger na Serengeti Boys zikiwa na Pointi 4 kila moja lakini Niger kusonga kutokana na Rekodi yao Bora dhidi ya Serengeti.

++++++++++++++++++++++

**FAHAMU:

-Washindi Wawili wa kila Kundi watatinga Nusu Fainali na Timu hizo 4 zitakazocheza Nusu Fainali ndizo hizo hizo zitafuzu kucheza Fainali za FIFA za Kombe la Dunia kwa Vijana U-17 huko Nchini India Mwezi Oktoba.

++++++++++++++++++++++

Mechi za Nusu Fainali zitachezwa Jumatano Mei 24.

TOTAL U-17 AFCON GABON 2017

Ratiba/Matokeo:

**Saa za Bongo

***KUNDI A Mechi kuchezwa Mjini Port Gentil KUNDI B Mjini Libreville

MAKUNDI:

Jumapili Mei 14

KUNDI A

Gabon 1 Guinea 5

Cameroun 0 Ghana 4

Jumatatu Mei 15

KUNDI B

Mali 0 Tanzania 0

Angola 2 Niger 2

Jumatano Mei 17

KUNDI A

Guinea 1 Cameroun 1

Ghana 5 Gabon 0

Alhamisi Mei 18

KUNDI B

Tanzania 2 Angola 1

Niger 1 Mali 2

MECHI ZA MWISHO ZA MAKUNDI

Jumamosi Mei 20

KUNDI A

Gabon 0 Cameroun 1

Guinea 0 Ghana 0

Jumapili Mei 21

KUNDI B

Mali 6 Angola 1

Tanzania 0 Niger 1]

MSIMAMO:

TOTAL-GROUPS

NUSU FAINALI:

Jumatano Mei 24

Stade de POG, Port Gentil

1730 Ghana v Niger

Stade de L’Amitle, Libreville

2030 Mali v Guinea

Jumapili Mei 28

Stade de L’Amitle, Libreville

1730 KUGOMBEA MSHINDI WA 3

2030 FAINALI

 

 

 

TOTAL U-17 AFCON GABON 2017: LEO SERENGETI BOYS YAWANIA NUSU FAINALI, FAINALI KOMBE LA DUNIA!

TOTAL AFCON U17 GABON2017>GUINEA YAUNGANA NA GHANA NUSU FAINALI!

LEO Usiku Serengeti Boys inaingia Stade de POG Mjini Port Gentil Nchini Gabon ikisaka Sare tu katika Mechi yao ya mwisho ya Kundi B la Mashindano ya TOTAL U-17 AFCON GABON 2017 ili watinge Nusu Fainali.

Wakipita na kuingia Nusu Fainali, Serengeti Boys pia watakuwa wamefuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia za U-17 huko India Mwezi Oktoba kwani Timu 4 zinazotinga Nusu Fainali ya Mashindano haya ya Gabon zinakwenda moja kwa moja India.

Katika Mechi zake za kwanza za Kundi B, Serengeti Boys ilitoka 0-0 na Mabingwa Watetezi Mali na kisha kuifunga Angola 2-1.

Hii Leo Serengeti Boys watacheza na Niger yenye Pointi 1 tu baada kutoka Sare na Angola na kisha kufungwa na Mali.

++++++++++++++++++++++

**FAHAMU:

-Washindi Wawili wa kila Kundi watatinga Nusu Fainali na Timu hizo 4 zitakazocheza Nusu Fainali ndizo hizo hizo zitafuzu kucheza Fainali za FIFA za Kombe la Dunia kwa Vijana U-17 huko Nchini India Mwezi Oktoba.

++++++++++++++++++++++

Jana Kundi A lilimaliza Mechi zake na Matokeo ni Ghana na Guinea 0-0 na Cameroun kuwafunga Wenyeji Gabon 1-0.

Hivyo, Guinea inaungana na Ghana, iliyofuzu kabla Mechi hii kucheza Nusu Fainali.

TOTAL U-17 AFCON GABON 2017

Ratiba/Matokeo:

**Saa za Bongo

***KUNDI A Mechi kuchezwa Mjini Port Gentil KUNDI B Mjini Libreville

MAKUNDI:

Jumapili Mei 14

KUNDI A

Gabon 1 Guinea 5

Cameroun 0 Ghana 4

Jumatatu Mei 15

KUNDI B

Mali 0 Tanzania 0

Angola 2 Niger 2

Jumatano Mei 17

KUNDI A

Guinea 1 Cameroun 1

Ghana 5 Gabon 0

Alhamisi Mei 18

KUNDI B

Tanzania 2 Angola 1

Niger 1 Mali 2

MECHI ZA MWISHO ZA MAKUNDI

Jumamosi Mei 20

KUNDI A

Gabon 0 Cameroun 1

Guinea 0 Ghana 0

Jumapili Mei 21

KUNDI B

2030 Mali v Angola [Stade de L’Amitle, Libreville]

2030 Tanzania v Niger [Stade de POG, Port Gentil]

NUSU FAINALI:

Jumatano Mei 24

Stade de POG, Port Gentil

1730 Mshindi Kundi A v Mshindi wa Pili Kundi B

Stade de L’Amitle, Libreville

2030 Mshindi Kundi B v Mshindi wa Pili Kundi A

Jumapili Mei 28

Stade de L’Amitle, Libreville

1730 KUGOMBEA MSHINDI WA 3

2030 FAINALI

TOTAL U-17 AFCON GABON 2017: SERENGETI BOYS YAIPIGA ANGOLA….YACHUNGULIA NUSU FAINALI, FAINALI KOMBE LA DUNIA!

TOTAL AFCON U17 GABON2017LEO huko Stade de L’Amitle, Mjini Libreville Nchini Gabon, Tanzania, maarufu kama Serengeti Boys, iliibwaga Angola 2-1 katika Mechi ya Kundi B la Mashindano ya TOTAL U-17 AFCON GABON 2017 na kujiweka poa kutinga Nusu Fainali.

Hii ni Mechi ya Pili kwa Serengeti Boys ambao walianza Kundi B kwa Sare ya 0-0 na Maabingwa Watetezi Mali.

Hii Leo, Serengeti walitangulia kufunga Dakika ya 6 kwa Bao la Kelvin Nashon Naftal na Angola kusawazisha Dakika ya 18 kwa Bao la Pedro

Mpaka Haftaimu Serengeti Boys 1 Angola 1

Kipindi cha Pili Dakika ya 69, Abdul Hamis Suleiman akaipa ushindi Serengeti Boys kwa Bao safi na kuwafanya watoke kifua mbele 2-1.

++++++++++++++++++++++

**FAHAMU:

-Washindi Wawili wa kila Kundi watatinga Nusu Fainali na Timu hizo 4 zitakazocheza Nusu Fainali ndizo hizo hizo zitafuzu kucheza Fainali za FIFA za Kombe la Dunia kwa Vijana U-17 huko Nchini India Mwezi Oktoba.

++++++++++++++++++++++

Baadae Leo hapo hapo Stade de L’Amitle, Mjini Libreville huko Gabon, Mechi ya Pili ya Kundi B itachezwa kati ya Mali na Niger.

Serengeti Boys watamaliza Mechi zao za Kundi B hapo Jumapili Mei 21 kwa kucheza na Niger huko Stade de POG, Port Gentil.

TOTAL U-17 AFCON GABON 2017

Ratiba/Matokeo:

**Saa za Bongo

***KUNDI A Mechi kuchezwa Mjini Port Gentil KUNDI B Mjini Libreville

MAKUNDI:

Jumapili Mei 14

KUNDI A

Gabon 1 Guinea 5

Cameroun 0 Ghana 4

Jumatatu Mei 15

KUNDI B

Mali 0 Tanzania 0

Angola 2 Niger 2

Jumatano Mei 17

KUNDI A

Guinea 1 Cameroun 1

Ghana 5 Gabon 0

Alhamisi Mei 18

KUNDI B

Tanzania 2 Angola 1

2030 Niger v Mali [Stade de L’Amitle, Libreville]

Jumamosi Mei 20

KUNDI A

2030 Gabon v Cameroun [Stade de POG, Port Gentil]

2030 Guinea v Ghana [Stade de L’Amitle, Libreville]

Jumapili Mei 21

KUNDI B

2030 Mali v Angola [Stade de L’Amitle, Libreville]

2030 Tanzania v Niger [Stade de POG, Port Gentil]

NUSU FAINALI:

Jumatano Mei 24

Stade de POG, Port Gentil

1730 Mshindi Kundi A v Mshindi wa Pili Kundi B

Stade de L’Amitle, Libreville

2030 Mshindi Kundi B v Mshindi wa Pili Kundi A

Jumapili Mei 28

Stade de L’Amitle, Libreville

1730 KUGOMBEA MSHINDI WA 3

2030 FAINALI

Habari MotoMotoZ