RIPOTI SPESHO

STARS WA KWENDA ETHIOPIA WATANGAZWA, SERENGETI BOYS WA TAYARI HUKO CONGO!

TAIFA STARS WATAKAOIVAA ETHIOPIA HAWA HAPA

TFF-HQ-1Kocha Mkuu wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania (Taifa Stars), Charles Boniface Mkwasa ametaja majina ya nyota 24 watakaounda kikosi ambacho kitasafiri mwishoni mwa wiki ijayo kwenda Addis Ababa, Ethiopia kucheza na wenyeji wetu kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika Oktoba 8, mwaka huu.

Mkwasa maarufu kwa jina la Master amesema wachezaji aliowaita wataingia kambini Oktoba 2, 2016 kabla ya kuanza kukiandaa kuanzia Oktoba 3, 2016 ikiwa mara baada ya michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara ya mwishoni mwa wiki hii ambako Mwadui itacheza na Azam huku Mbao ikishindina na JKT Ruvu Oktoba 2, mwaka huu.

Mkwasa maarufu kwa jina la Master amesema wachezaji aliowaita wataingia kambini Oktoba 2, 2016 kabla ya kuanza kukiandaa kuanzia Oktoba 3, 2016 ikiwa mara baada ya michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara ya mwishoni mwa wiki hii ambako Mwadui itacheza na Azam huku Mbao ikishindina na JKT Ruvu Oktoba 2, mwaka huu.

Nyota wa Stars walioitwa na Mkwasa ni:

Makipa

Deogratius Munishi – Young Africans

Said Kipao – JKT Ruvu

Aishi Manula – Azam FC

Mabeki

Shomari Kapombe – Azam FC

Juma Abdul – Young Africans

Vicent Andrew - Young Africans

Mwinyi Haji - Young Africans

Mohamed Hussein – Simba SC

David Mwantika - Azam FC

James Josephat – Tanzania Prisons

Viungo wa Kati

Himid Mao - Azam FC

Mohammed Ibrahim – Simba SC

Jonas Mkude – Simba SC

Muzamiru Yassin – Simba SC

Viungo wa Pembeni

Shiza Kichuya – Simba SC

Simon Msuva - Young Africans

Juma Mahadhi - Young Africans

Jamal Mnyate – Simba

Hassan Kabunda – Mwadui FC

Washambuliaji

Ibrahim Ajib – Simba SC

John Bocco - Azam FC

Mbwana Samatta - CK Genk ya Ubelgiji

Elius Maguli – Oman

Thomas Ulimwengu – TP Mazembe Congo

Mchezo huo utakaofanyika jijini Addis Ababa, umeratibiwa kwa mujibu wa kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ambalo huwa na kalenda ya wiki ya mechi za kimataifa kwa wanachama wake – Tanzania ni miongoni mwao. Shirikisho la Mpira wa Miguu la Ethiopia (EFF), wameo

Hii ni faida kwa Tanzania kama itashinda mchezo huo kwa maana kina alama za nyongeza kama inatokea unaifunga timu mwenyeji.

Matokeo ya mchezo huo, ni sehemu malumu kupima viwango vya ubora na uwezo wa timu za taifa. Kwa sasa Tanzania inashika nafasi ya 132 kati ya nchi 205 wanachama wa FIFA zilizopimwa ubora. Ethiopia yenyewe inashika nafasi ya 126.

Argentina inaongoza ikifuatiwa na Ubelgiji anakocheza Mbwana Samatta – nyota wa kimataifa wa Tanzania. Samatta anacheza klabu ya K.R.C Genk inayoshiriki Ligi Kuu ya Ubelgiji. Timu nyingine bora kimataifa ni Ujerumani, Colombia na Brazil.

Katika Bara la Afrika, Ivory Coast ambayo ni ya 34 kwa ubora duniani ndiyo inayoongoza ikifuatiwa na Algeria, Senegal, Tunisia na Ghana.

KAULI NZITO YA MAKOCHA SERENGETI BOYS

Makocha wa timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya vijana wa Tanzania ‘Serengeti Boys’, Bakari Nyundo Shime na Muharami Mohammed anayewanoa makipa watatu wa timu hii, wamesema kwa pamoja: “Tuko tayari kwa vita.”

Shime maarufu kama Mchawi Mweusi, amezungumza hayo wakati anaendelea kufanya maandalizi ya mwisho ya mchezo dhidi ya Jamhuri ya Congo utakaofanyika Jumapili Oktoba 2, kwenye Uwanja wa Alphonse Massamba-Débat ulioko kwenye Makutano ya Barabara za Nkolo na Boko, hapa jijini Brazzaville.

Katika mazungumzo yake, Shime anasema: “Timu iko vizuri. Tumejiandaa vizuri kwa yale ya msingi yote tumekamilisha. Kwa hivyo, kila kitu kiko sawa, kama tulivyokusudia. Tupo hapa Congo kwa sasa kumalizia au kukumbushia mambo mawili au matatu hivi...

“Lakini pia tupo hapa Congo kuzoea hali ya hewa. Kwa bahati nzuri si tofuati na ya nyumbani Tanzania,” anasema Shime kwa kujiamini kabisa leo mchana Septemba 29, 2016 huku akijiandaa kwenye mazoezi.

Shime anasema kwamba mfumo atakaoutumia ni wa 4-4-2 katika mchezo huo wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana. Fainali hizo zitafanyika jijini Antananarivo, Madagascar mwezi Aprili, mwakani.

Anasema kwamba mfumo huo ni rafiki kwa Serengeti Boys kwani katika michezo takribani 15 ya kimataifa hajapoteza hata mmoja, “Kwa hivyo siwezi kubadili mfumo huu. Ni mfumo wa kushambulia na kulinda tusifungwe. Vijana wanauelewa zaidi na ndio mfumo wetu.”

Shime aliyekuwa mchezaji zamani kabla ya ndoto zake za kusonga mbele kufutwa kwa majeruhi, anasema kwamba benchi nzima la ufundi linafahamu kuwa mchezo wa Jumapili dhidi ya Congo ni mgumu kwa sababu ya umuhimu wake.

Na akiwaelezea Congo - wapinzani wake, Kocha Shime anasema: “Ni timu ya kawaida kwa maana wanafungika. Kwenye mchezo huu ukiangalia kwa makini sisi ndio tunahitaji zaidi ushindi kuliko Congo. Lakini nataka uwaambie Watanzania kwamba pamoja na hayo, nawaheshimu Congo, najua wako nyumbani lakini mwisho wa siku ni wachezaji 11 kila upande ndio watakaoingia uwanjani.”

Amesema kwamba amekiandaa kikosi chake vema kabisa katika eneo la mbinu, ufundi na saikolojia. “Akili za vijana wangu wooooote ni kuhakikisha tunafanya vema kwenye mchzo wa Jumapili.”

Naye Kocha wa Makipa, Muharami Mohammed au Shilton, alisema: “Silaha zangu ziko tayari kwa vita, makipa wangu wangu wote akiwamo Kelvin Kayego, Ramadhani Kabwili na Brazio wote wako fiti. Ye yote kati yao anaweza kucheza.”

IMETOLEWA NA TFF

BIG SAM AACHIA NGAZI ENGLAND BAADA MECHI 1 NA SIKU 67 TU!

BIG-SAMSam Allardyce, maarufu kama Big Sam, ameacha kazi ya Umeneja wa Timu ya Taifa ya England baada ya kuwa Madarakani kwa Siku 67 tu na kusimamia Mechi 1 tu.

Kung’atuka huku, ambako kumesemwa ni kwa makubaliano ya pande mbili, kumekuja baada ya Gazeti la Uingereza The Daily Telegraph kudai alizungumzia njia zisizo halali za Uhamisho wa Wachezaji.

Gazeti hilo limechapisha habari kuwa Maripota waliojifanya Wafanyabiashara walizungumza na Allardyce na yeye alikiri inawezekana kuizunguka Sheria ya FA, Chama cha Soka England, ya Mwaka 2008 ya kuzuia Mchezaji kuwa Mali ya Mmiliki mwingine Kibiashara mbali ya Klabu yake.

Pia, ripoti ya Telegraph ilidai alimdhihaki Meneja wa England aliemrithi, Roy Hogson, huku pia akisema FA inajali kutengeneza Fedha tu.

Gazeti hilo pia lilirusha mtandaoni Video inayoonyesha Mkutano huo na Wafanyabiadhara feki wakati Big Sam akimponda Hodgson na kuikandya FA.

Vile vile, Gazeti hilo limedai Allardyce, mwenye Miaka 61, alitaka kutumia wadhifa wake ilia pate Dili ya kumwingizia Pauni 400,000 kwa kuiwakilisha Kampuni ya huko Mashariki ya Mbali Ya Asia.

FA imetamka kuwa Gareth Southgate atakaimu nafasi ya Umeneja wa England.

BIG SAM MATATANI BAADA KUNASWA MTEGONI!

BIG-SAMGAZETI moja huko Uingereza, The Daily Telegraph, limemtia matatani Meneja wa England Sam Allardyce baada kudai alizungumzia njia zisizo halali za Uhamisho wa Wachezaji.
Gazeti hilo limechapisha habari kuwa Maripota waliojifanya Wafanyabiashara walizungumza na Allardyce, maarufu kama Big Sam, ambae alikiri inawezekana kuizunguka Sheria ya FA, Chama cha Soka England, ya Mwaka 2008 ya kuzuia Mchezaji kuwa Mali ya Mmiliki mwingine Kibiashara mbali ya Klabu yake.
Pia, ripoti ya Telegraph ilidai alimdhihaki Meneja wa England aliemrithi, Roy Hogson, huku pia akisema FA inajali kutengeneza Fedha tu.
Gazeti hilo pia lilirusha mtandaoni Video inayoonyesha Mkutano huo na Wafanyabiadhara feki wakati Big Sam akimponda Hodgson na kuikandya FA.
FA wamethibitisha kuwepo kwa sakata hili na kueleza kuwa wamelitaka The Daily Telegraph kuwapa ukweli wote kuhusu Mkutano huo.
Inasemekana Allardyce mwenyewe hajajibu chochote alipotakiwa kujibu tuhuma hizi.

KPL: SOFAPAKA WAIBANA MBAVU GOR MAHIA

NA Ripota Spesho toka Kenya

KENYA-LIGI2Sofapaka inayokabiliwa na tisho la kushuka Daraja iliibana Gor Mahia kwa sare tasa huku mechi zilizohusisha Thika United-Sony Sugar na Mathare United-Posta Rangers pia zikitoka sare kwenye Jumapili ya kugawanya alama.

Mathare United 0-0 Posta Rangers

Matumaini ya Mathare United kushinda ligi kuu yalizidi kudidimia baada ya kuzuiliwa na Ranger waliocheza kibabe. Timothy Otieno alikaribia kupata bao la uongozi mapemaKENYA-LIGI kwa upande wa Rangers lakini akapIga nje. Baadaye Mathare,walioanza msimu huu vizuri, waliwaelemea bila kuzalisha bao. Sare hii ina maana kuwa Mathare wameshinda mechi mbili tu kati ya 10 na hivyo basi wamejitoa kwenye nafasi ya uwezekano wa kushinda taji lao la pili.

Matokeo haya yameidumisha Posta Rangers kwenye nafasi ya saba kwenye jedwali.

Thika United 1-1 Sony Sugar.

Sony Sugar waliokuwa wanacheza kwa kujituma waliingia uongozini dakika ya 26 kupitia kwa Victor Ademba aliyepokea pasi ya toka kwa Amon Muchiri. Thika walipambana vilivyo lakini ikawabidi wasubiri mpaka robo ya mwisho pale Saad Musa alipomalizia pasi ya Eugene Mukangula na kusawazisha Bao.

Sofapaka 0-0 Gor Mahia.

Mawindo ya Gor Mahia yaliingia doa jengine kwa kudondosha alama mbili dhidi ya waburuza mkia Sofapaka, wanaopigania wasiteremshwe ngazi. Mechi hii ilichezwa kwenye Uwanja wa Nyayo, Nairobi na Sofapaka almaarufu 'Batoto ba Mungu’ wakatumia mbinu ya kujaza kiungo cha kati ili kukatiza mtiririko wa K’Ogalo na wakafaulu.

Kocha wao David Ouma alifurahia kujituma kwa wachezaji wake kikamilifu. Gor walitawala mchezo huo na kupoteza nafasi za wazi, na matokeo haya huenda yakawagharimu huku ziiisalia mechi tano kukanilisha msimu wa mwaka 2016 wa ligi kuu ya Kenya.

Gor wapo alama nne nyuma ya Vinara Tusker walioshinda mechi yao ya wikendi kwa kuibwaga Muhoroni Youth FC 2 - 1 .

LIGI KUU SPORTPESA

Matokeo:

Ijumaa Septemba 23

FT Tusker FC 2 - 1 Muhoroni Youth FC

Jumamosi Septemba 24

FT Chemelil Sugar 1 - 0 Ulinzi Stars

FT AFC Leopards 0 - 1 Western Stima

FT Bandari 1 - 3 Nairobi City Stars

FT Kakamega Homeboyz 1 - 1 Ushuru

FC Jumapili Septemba 25

FT Mathare United 0 - 0 Posta Rangers

FT Thika United 1 - 1 SoNy Sugar

FT Sofapaka 0 - 0 Gor Mahia

MOURINHO AKANUSHA NUKUU YA ‘KUBOMOA SURA YA WENGER’!

WENGER-MOURINHOJose Mourinho amesema hana tatizo na Arsene Wenger licha ya kuchapishwa Kitabu kikimnukuu yeye akisema ‘ataibomoa Sura ya Wenger’.

Mourinho, ambae sasa ni Meneja wa Manchester United, amekuwa na upinzani wa muda mrefu na Wenger ambae ni Meneja wa Arsenal na hasa wakati Mourinho akiwa ni Meneja wa Chelsea.

Akiwa huko Chelsea, Mourinho aliwahi kumbatiza Wenger kuwa ni ‘Spesho wa Kushindwa’.

Nukuu hiyo ya kwamba ‘ataibomoa Sura ya Wenger’ ipo kwenye Kitabu kiitwacho Jose Mourinho: Up Close and Personal  kilichaoandikwa na Mwanahabari Rob Beasley.

Jana, Wenger alipogusiwa kuhusu Kitabu hicho alisema hatakisoma.

Na Jana hiyo hiyo, Mourinho akaulizwa kuhusu Kitabu hicho na kujibu: “Utaona yuko karibu na mimi. Nina furaha. Ametengeneza Pesa zake, hilo sawa kwangu!”

Mourinho aliongeza: "Nilikutana na Arsene Wenger Wiki chache zilizopita, na kama Watu wastaarabu, tukapeana mikono. Tukakaa Meza moja na kula Chakula cha Usiku pamoja na Watu wengine. Tukabadilishana mawazo, tuliongea kwa sababu sisi ni Watu tuliostaarabika. Kwa mara nyingine sidhani Kitabu hiki kitakaa Maktaba moja na vile vya Shakespeares na vingine!”

Aliongeza: “Sitaongeza lolote jingine. Hilo ni neon langu la mwisho. Narudia huyo ametengeneza Pesa yake. Hilo sawa kwangu!”