RIPOTI SPESHO

CHIPOLOPOLO KUIVAA STARS IJUMAA DAR!

CHIPOLOPOLOFAZ, Chama cha Soka Zambia, kimethibitisha kuwa Timu yao ya Taifa, maarufu kama Chipolopolo, itasafiri kwenda Dar es Salaam kucheza Mechi mbili na Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars.
Mechi hizo zitachezwa Machi 24 na 26
Kocha wa Chipolopolo, Wedson Nyirenda, ameita Kikosi cha Wachezaji 20 kwa ajili ya msafara huo na miongoni mwao ni Straika wa Zamalek ya Egypt, Emmanuel Mayuka, huku wengi wakitokea Klabu za ndani ya Zambia.
Mchezaji mwingine anaecheza nje ni Kennedy Mweene wa Mamelodi Sundowns ya Afrikavya Kusini ambao ndio Klabu Bingwa Afrika. 
Wachezaji wapya kabisa walioitwa Chipolopolo na Nyirenda ni Justin Banda, Mwila Phiri, Augustine Mulenga, Mukubanga Siambombe, Isaac Shamujompa, Chitiya Mususu na Kelvin Mubanga wakati Taonga Bwembya, Mweene Mumbi na John Ching'andu wakipandishwa toka Timu ya Vijana.
Hivi sasa Zambia inajisuka kwa Mechi 2 za CHAN dhidivya Swaziland Mwezi Julai ja ile ya Mchujo wa AFCON dhidi ya Msumbiji Mwezi Julai.
ZAMBIA - KIKOSI KAMILI WACHEZAJI 20:
MAKIPA: Jacob Banda (Zesco United), Racha Kola (Zanaco), Allan Chibwe (Power Dynamos), Kennedy Mweene (Mamelodi Sundowns);
MABEKI: Taonga Bwembya (Zanaco), Donashano Malama (Nkana), Fackson Kapumbu (Zesco United), Mweene Mumbi (Green Buffaloes), Ziyo Tembo (Green Buffaloes), Isaac Shamujompa (Napsa (Stars), Adrian Chama (Green Buffaloes), Billy Mutale (Power Dynamos), George Chilufya (Zanaco);
VIUNGO: Mischeck Chaila, John Ching’andu, Kondwani Mtonga (all Zesco United), Clatous Chama (Lusaka Dyanmos), Kelvin Mubanga , Fwayo Tembo (both Power Dynamos), Justin Banda (Napsa Stars), Mwila Phiri (Choma Eagles), Augustine Mulenga (Zanaco), Mukubanga Siambombe (Zamcoal Diggers);
MASTRAIKA: Jackson Mwanza (Zesco United), Justin Shonga (Nkhwazi), Chitiya Mususu (Napsa Stars), Ronald Kampamba (Nkana) and Emmanuel Mayuka (Zamalek).
TAIFA STARS:
 

AHMAD AMBWAGA HAYATOU CAF, ZANZIBAR SASA MWANACHAMA WA 55 WA CAF!

CAF-ASSEMBLYKIONGOZI wa Chama cha Soka cha Madagascar anaetambulika kwa Jina moja tu, Ahmad, amechaguliwa kuwa Rais mpya wa Shirikisho la Soka Afrika CAF na rasmi kuimaliza himaya ya Issa Hayatou aliedumu Miaka 29.

Ahmad alizoa Kura 34 kati ya 54 kwenye Uchaguzi uliofanyika hii Leo huko Addis Ababa Mji Mkuu wa Ethiopia.

Mabadiliko hayo ni ya kwanza tangu Hayatou ashika hatamu Mwaka 1988 na Ahmad anakuwa Rais wa 7 wa CAF katika enzi ya Miaka 60 ya Shirikisho hilo.

Mara baada ya kuchaguliwa, Ahmad, mwenye Miaka 57, alishindwa kuongea lolote kwa kukabwa na furaha huku Wajumbe wakimbeba juu kwa juu kwa furaha.

ZANZIBAR SASA MWANACHAMA WA 55 WA CAF

Mapema Leo, Zanzibar imeingizwa rasmi kama Mwanachama wa 55 kufuatia Kikao cha 39 cha Mkutano Mkuu wa CAF.

Mapendekezo ya kukubaliwa Zanzibar kama Mwanachama kamili wa CAF yalipendekezwa na Rais wa TFF, Jamal Malinzi, na kupitishwa kwa kauli moja na Wanachama 54 wa CAF.

Awali Zanzibar ilikuwa ikiruhusiwa kucheza Mashindano ya Klabu Afrika lakini kwenye yale ya Timu za Taifa ilibidi ishiriki pamoja na Tanzania Bara kama Nchi moja Tanzania.

Baada ya hatua hii ya kupata Uanachama kamili, sasa Zanzibar ipo huru kuwakilishwa na Timu yake ya Taifa na pia kupata Misaada ya Fedha moja kwa moja kutoka CAF na FIFA badala ya kupitishwa TFF.

PAWASA, IVO MAPUNDA, NIZAR HALFAN, MGOSI, BI DORIS MALYAGA WA MWANASPOTI NA 22 WENGINE KUFUZU UKOCHA!

PRESS RELEASE NO. 267 MACHI12, 2017
TFF-TOKA-SITRais wa  Shirikisho  la Mpira wa  Miguu Tanzania (TFF),   Jamal Emil Malinzi kesho Jumatatu, Machi 13, 2017 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya kufunga kozi ya ukocha ngazi ya ‘Intermediate’ kwa makocha 27 wanaotarajiwa kuhitimu.
Kozi hiyo iliyoendeshwa na Wilfred Kidao - Mkufunzi anayetambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), itafungwa saa 5.00 asubuhi kwenye Viwanja vya Michezo vya Bandari, vilivyoko Tandika jijini Dar esSalaam.
Mbali   ya   Kidao,   wakufunzi   wengine   walikuwa   ni   Manyika Peter aliyefundisha   programu   au   mtaala   kwa   makocha   wa   makipa;   Dk. Nassoro   Ally   Matunzya   aliyewanoa   makocha   hao   kuhusu   tiba   za wanamichezo/wanasoka na Mkufunzi wa muda mrefu wa soka, Hemed Mteza.
Wanafunzi   wa   kozi   hiyo   wanaotarajiwa   kuhitimu   kesho   Jumatatu   ni pamoja Doris Malyaga ambaye ni Mwanamke pekee kati ya wanafunzi 27 walisoma kozi hiyo kwa kipindi cha siku 14 cha mwanzo wa mwaka.
Doris ni mwanahabari za michezo aliyehudhuria kozi hiyo. Anaandikia gazeti   la   MwanaSPOTI   linalotolewa   na   Kampuni   ya   Magazeti   ya Mwananchi (MCL).
Wengine ni nyota wa zamani wa timu ya mpira wa miguu ya Tanzania ‘Taifa   Stars’   waliopata   kuchezea   klabu   kongwe   na   kubwa   nchini.
Wanafunzi hao ni Boniface Pawasa, Fred Mbuna, Innocent Haule, Herry Morris, Ivo Mapunda, Nizar Khalfan na Mussa Hassan Mgosi.
Wengine ni Omar Kapilima, Amosi Mgisa, Uhuru Mwambungu, Yussuf Macho,   George   Minja,   Haruna   Adolf,   Selemani   Omari,   Ally   Ruvu, Masoud   Selemani,   Haji   Mustapha,   Mhasham   Khatib,   Issa   Ndunje, Salum Kapilima, Said Salum, Julio Elieza, Hassan Mwakami, Rajab Mponda, Ally Mbonde na Evod Mchemba.…………………………………………………………………………........................IMETOLEWA   NA   SHIRIKISHO   LA   MPIRA   WA   MIGUUTANZANIA (TFF)   National Team Main Sponsor

KARIAKOO MZAWA, KWETU NI MISHENI KOTA

TANZANIA-UPENDO-SPESHO-FBKARIAKOO MZAWA, KWETU NI MISHENI KOTA

Nimekulia Mganda, ukaja Mkwaju Ngoma

Dar Jazi ilipoanza, TANU ilipotanua

Kwetu ni Misheni Kota, Kariakoo Mzawa

KARIAKOO MZAWA, KWETU NI MISHENI KOTA

Namba Nane hapo Ndanda, Sasa ni Joni Rupia

Ndiko mi nilianzia, Na Magila Chekechea

Mchikichini ni Kwanza, Stina Nane kumaliza

KARIAKOO MZAWA, KWETU NI MISHENI KOTA

Kizaviera nikenda, Siku hizi Kibasila

Shinyanga pia nikenda, Fomu Siksi nikapiga

Kisha Jeshi nikapiga, Ikaja Anga taluma

KARIAKOO MZAWA, KWETU NI MISHENI KOTA

Vyeti Feki la sinaga, Zama hizo hakunaga

Hata Shuleni uliza, Jeshini Ruvu we nenda

Fosi Namba utapewa, Na Efu ni Kombania

KARIAKOO MZAWA, KWETU NI MISHENI KOTA

TANU ilituanzia, Chama Mapinduzi kuja

Vyote mbiu ni usawa, Binadamu wapo sawa

Nyerere ndio ye Baba, Heshima ni kwako Baba

KARIAKOO MZAWA, KWETU NI MISHENI KOTA

Tumekulia Mganda, ukaja Mkwaju Ngoma

Mdundiko tukaona, Mchiriku ukapita

Ukaja nao Mnanda, Vigodoro kuibuka

KARIAKOO MZAWA, KWETU NI MISHENI KOTA

Soka Wananchi Yanga, Sandalendi ni wakuja

Sandalendi ndio Simba, wakazaa Redi Staa

Mgawanyiko wa Yanga, ukazaa Pan Afrika

KARIAKOO MZAWA, KWETU NI MISHENI KOTA

Nyerere ndio ye Baba, Heshima ni kwako Baba

Mwinyi nae akashika, Akafatia Mkapa

Jakaya Kikwete poa, Sie bado twakupenda

KARIAKOO MZAWA, KWETU NI MISHENI KOTA

Magufuli ametinga, Kwapani ana Mikoba

Matapeli wanalia, Vyanzo vyote vimekatwa

Ewe Mola twakuomba, Idumishe Tanzania

KARIAKOO MZAWA, KWETU NI MISHENI KOTA

++++++++++++++++++++++++++++++

JUMAA MUBARAK Wanduguz!

*Kwa wenzangu wa Jumamosi na Jumapili, Sala njema tuombeane tu!

**Akina mie, tuselebuke aste aste, Mola yupo tu!

Aminia!

ILA KUMBUKA: Umoja ni Ushindi!

>>A Luta Continua….Wanduguz!!!

++++++++++++++++++++++++++++++

TFF – KAMATI YA UTENDAJI MACHI 26, ROBO FAINALI MACHI 18!

PRESS RELEASE NO. 264                                      MACHI 7, 2017

KIKAO CHA KAMATI YA UTENDAJI TFF

TFF-TOKA-SITKikao cha kawaida cha Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kinatarajiwa kukaa Machi 26, mwaka huu ambako pamoja na ajenda nyingine, itaamua tarehe rasmi ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika baadaye mwaka huu.

Kikao hiki cha kawaida, kwa mujibu wa katiba hufanyika mara nne kwa mwaka na huamua masuala mbalimbali ya uendeshaji na usimamizi wa mpira wa miguu nchini.

Kadhalika Mkutano Mkuu wa uchaguzi kwa mujibu wa Katiba ya TFF, hufanyika kila baada ya miaka minne kwa mwaka.

ROBO FAINALI AZAM SPORTS FEDERATION CUP

Mechi mbili za kwanza hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Azam (Azam Sports Sports Federation Cup 2016/2017), zitachezwa Machi 18, mwaka huu kwenye viwanja viwili tofauti.

Mechi hizo ni kati ya Kagera Sugar itakayocheza na Mbao FC ya Mwanza kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba mkoani Kagera kadhalika Simba itakayosafiri hadi Arusha kucheza na Madini kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Mechi nyingine zitapangiwa tarehe za baadaye. Mechi hizo ni kati ya Azam FC na Ndanda FC kadhalika Tanzania Prisons ya Mbeya itakayocheza na mshindi kati ya Young Africans ya Dar es Salaam na Kiluvya United ya Pwani.

Bingwa wa michuano hiyo kwa mujibu wa kanuni, atazawadiwa Tsh. 50 milioni.

Pia bingwa wa michuano hiyo, ndiye atakayeiwakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika ya Total wakati Bingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara ndiye ataiwakilisha nchi kwenye michuano ya Total Ligi ya Mabingwa Afrika.

..…………………………………………………………………………........................

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)