RIPOTI SPESHO

BAUZA ATIMULIWA ARGENTINA!

ARGENTINA-LOSSArgentina imemfukuza Menejabwao wa Timu ya Taifa Edgardo Bauza kufuatia matokeo mabovu yanayohatarisha.kufuzu kwao kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia.
Bauza alisimamia Mechi 8 za Kanda ya Nchi za Marekani ya Kusini CONMEBOL za kusaka WC-2018-SA-TEBO-MAR24kwenda Fainali za huko Russia na wameshinda 3 tu kati ya hizo.
Hivi sasa Argentina wapo Nafasi ya 5 ya Nchi za Kanda ya Marekani ya Kusini nafasi ambayo itawanyima kufuzu moja kwa moja kwenda Russia.
Timu 4 za juu ndizo zinazofuzu moja kwa moja kwenda Fainali za Kombe la Dunia za huko Russia.
Timu inayomaliza Nafasi ya 5 hulazimika kucheza Mechi ya Mchujo na Nchi kutoka Kanda ya OCEANIA na Mshindi kutinga Russia.
Mbali ya kusuasua kwenye Mechi hizo za kwenda Russia, Argentina pia wapo kwenye pigo kubwa kutokana na Kifungo cha Mechi 3 cha Nahodha wao Lionel Messi kitakachomfanya acheze Mechi ya mwisho tu ya Kanda yao kwani wamebakiza Mechi 4 tu.
Bauza alishika Umeneja wa Argentina Agosti Mwaka Jana baada ya kujiuzulu kwa Gerardo "Tata" Martino alieng'oka baada ya Argentina kufungwa na Chile kwenye Fainali ya Copa America Centenario.
Muargentina ambae ni Kocha wa Sevilla ya Spain Jorge Sampaoli anatajwa kushika wadhifa huu.
 

TOKA TFF: MAREFA YANGA-MC ALGERS NI WARWANDA, VPL WIKIENDI MECHI 6!

WAAMUZI MCHEZO WA YOUNG AFRICANS, MC ALGERS

TFF-TOKA-SITMchezo wa kimataifa wa Raundi ya Pili kati ya Young Africans ya Dar es Salaam, Tanzania na Mouloudia Club D’Alger ya Algeria unatarajiwa kufanyika kesho Jumamosi Aprili 8, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam ambako utachezeshwa na waaamuzi kutoka Rwanda.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), waamuzi hao ni Louis Hakizimana ambaye atakuwa mwamuzi wa kati akisaidiwa na Theogene Ndagijimana akiwa mshika kibendera wa mstari wa kulia na Jean Bosco Niyitegeka ambaye atakuwa mshika kibendera mstari wa kushoto.

Mwamuzi wa akiba ambaye pia atakuwa anatokea Rwanda ni Ruzindana Nsoro wakati Kamishna wa mchezo atakuwa Ata Elmanan Hassan Osama kutoka Sudan. Waamuzi hao pamoja na Kamishna wa mchezo wamefikia Hoteli ya Urban Rose iliyoko Mtaa wa Jamhuri, katikati ya jiji la Dar es Salaam, Tanzania.

Wapinzani wa Young Africans ambao ni Alger waliingia ujana usiku saa 3.30 kutoka Algeria kwa ndege maalumu ya kukodi na kufikia Hoteli ya Holiday Inn. Kwa mujibu wa kanuni, leo Ijumaa Aprili 7, mwaka huu saa 10.00 jioni watafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mchezo huo muhimu kwa Young Africans kusonga mbele kama ilivyotokea msimu uliopita kwa kuifunga Sagrada Esperanca ya Angola na kutinga hatua ya makundi, viingilio vimepangwa kuwa Sh 30,000 kwa VIP ‘A’; Sh 20,000 kwa VIP ‘B’ na ‘C’ wakati mzungunguko itakuwa ni Sh 5,000.

Akizungumzia mchezo huo, Kocha msaidizi wa Young Africans, Juma Mwambusi alisema: “Wachezaji wa Yanga wako na morali wa hali juu na kikubwa tunawaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu hii kwa sababu ni klabu pekee iliyobaki ikiiwakilisha nchi.

MECHI ZA WIKIENDI LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa michezo sita.

Kwa mujibu wa ratiba ya ligi hiyo, Jumamosi Aprili 8, mwaka huu Mbeya City itashindana na Ndanda ya Mtwara kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya wakati Majimaji ya Songea itaialika African Lyon ya Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma.

Mechi nyingine kwa siku ya Jumamosi Aprili 8, mwaka huu itakuwa ni kati ya Kagera Sugar na JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera wakati wakati siku ya Jumapili Aprili 09, mwaka huu Stand United itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.

Ligi inatarajiwa kuendelea Jumatatu Aprili 10, mwaka huu kwa michezo miwlili ambako Simba itakuwa mgeni wa Mbao kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ilihali Mtibwa Sugar itaialika Azam FC kwenye Uwanja wa Manungu mkoani Morogoro.

IMETOLEWA NA TFF

KIMATAIFA KIRAFIKI: TANZANIA KIDEDEA, SPAIN YABEBWA NA TEKNOLOJIA YA VAR KUIBWAGA FRANCE, RONALDO APIGA, URENO YAPIGWA!

KIMATAIFA KIRAFIKI
Matokeo:
Jumanne Machi 28
Republic of Ireland 0 Iceland 1
Tanzania 2 Burundi 1
Georgia 5 Latvia 0
Albania 1 Bosnia-Herzegovina 2
Egypt 3 Togo 0
Estonia 3 Croatia 0
Macedonia 3 Belarus 0
Russia 3 Belgium 3
South Africa 0 Angola 0
Luxembourg 0 Cape Verde Islands 2
Austria 1 Finland 1
Netherlands 1 Italy 2
France 0 Spain 2
Portugal 2 Sweden 3
+++++++++++++++++++++++++++
STARS-SAMATTA-BOTSWANA-1Jana zilichezwa Mechi kadhaa za Kirafiki za Kimataifa kila kona ya Dunia na wakati Tanzania ikiifunga Burundi 2-1 Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam huko Ulaya Vigogo kadhaa walipambana.
Huko Amsterdam ArenA Wenyeji Netherlands, wakiwa hawana Kocha Mkuu baada Juzi kumtimua Danny Blind, Jana walichezea kichapo kwa kufungwa 2-1 na Italy.
Netherlands walitangulia Dakika ya 10 baada Alessio Romagnoli kufunga mwenyewe lakini Dakika 1 baadae Italy walisawazisha kwa Goli la Eder Citadin Martins na kupiga Bao la Pili na ushindi katika Dakika ya 32 kupitia Leonardo Bonucci.
Huko Aviva Stadium Mjini Dublin Wenyeji Ireland walitunguliwa 1-0 kwa Frikiki ya Dakika ya 22 ya Horour Magnusson.
Nako Estadio dos Barreiros, Funchal Visiwani Madeira, Wenyeji Portugal walitangulua 2-0 hadi Haftaimu kwa Bao za Cristiano Ronaldo na Andreas Granqvist lakini Sweden wakapiga 3 Kipindi cha Pili kupitia Victor Claesson, Bao 2, na la Dakika ya 90 la Joao Cancelo aliejifunga mwenyewe.
Stade de France Jijini Paris ilushuhudia Wenyeji France wakichapwa 2-0 na Spain kwa Bao za Dakika za 68 na 77 za Penati ya David Silva na lile la Gerard Deulofeu.
Mechi hii itakumbukwa kwa matumizi mazuri ya Teknolojia iliyopo Majaribioni ya VAR, VIDEO ASSISTANT REFEREE, iliyosaidia kuamua Bao 1 ni Ofsaidi na jingine si Ofsaidi baada Mshika Kibendera kulikataa akiashiria ni Ofsaidi.
Bao la Straikacwa France Antoine Griezmann lilikataliwa na VAR kwa kuwa lilikuwa ni Ofsaidi wakati Bao la Pili la Spain alilofunga Gerard Deulofeu kukubaliwa na VAR baada Refa Msaidizi kulikataa kwa madai ni Ofsaidi.
++++++++++++++++++++++++++++++

JE WAJUA?
VARS:

-Mfumo wa Majaribio uitwao VARs, Video Assistant Referees.

Mfumo wa Video kusaidia maamuzi ya Marefa Uwanjani, VARs [Video Assistant Referes] umefanyiwa Majaribio rasmi ya FIFA kwa mara ya kwanza katika Mechi ya Kimataifa hapo Septemba 1 wakati Italy ilipocheza na France huko Bari.

Kwenye Mfumo huo wa Video, Refa Msaidizi anakuwepo pembeni mwa Uwanja na anakuwa na Mawasiliano na Refa wa Mechi wakati wote wa Mechi hiyo akipitia Video bila kusitisha Mechi.

Ikiwa litatokea tukio ambalo Refa Msaidizi ameliona atamtonya Refa wa Mechi ambae ana ruksa ya kuukubali ushauri huo au au akaamua mwenyewe kwenda pembeni kutizama na kuliptia tukio na kutoa uamuzi wake.

Ama Refa huyo anaweza kumuomba Refa Msaidizi kulipitia tukio ili ampe ushauri.

++++++++++++++++++++++++++++++

 

KIMATAIFA - KIRAFIKI: LEO TANZANIA-BURUNDI, HOLLAND-ITALY, RUSSIA-BELGIUM, IRELAND-ICELAND, EGYPT-TOGO

Ratiba
Jumanne Machi 28
**Saa za Bongo
2145 Republic of Ireland v Iceland
1600 Tanzania v Burundi
1700 Georgia v Latvia
1900 Albania v Bosnia-Herzegovina
1900 Egypt v Togo
1900 Estonia v Croatia
1900 Macedonia v Belarus
1900 Russia v Belgium
2000 South Africa v Angola
2100 Luxembourg v Cape Verde Islands
2145 Austria v Finland
2145 Netherlands v Italy
+++++++++++++++++++++++++++
STARS-SAMATTA-BOTSWANALEO zipo Mechi kadhaa za Kimaifa za Kirafiki ambayo ni Kalenda rasmi ya FIFA kwa Mechi hizo na miongoni mwake ipo ile itakayochezwa Mjini Dar es Salaam Uwanja wa Taifa kati ya Tanzania na Burundi.
Hii ni Mechi ya Pili kwa Tanzania katika kipindi hiki rasmi cha Kalenda ya FIFA ambapo Juzi waliitwanga Botswana 2-0 huku Bao zote zikifungwa na Nahodha wao Mbwana Samatta anaechezea KRC Genk ya Belgium.
Hiyo ilikuwa ni Mechi ya kwanza kwa Kocha mpya wa Tanzania, maarufu kama Taifa Stars, Salum Mayanga akisaidiwa na Patrick Mwangata, na Leo watataka tena kuibuka na ushindi dhidi ya Burundi yenye Wachezaji kadhaa wanaocheza Soka la Kulipwa Nchini Tanzania.
Hao ni Amisi Tambwe wa Yanga na Laudit Mavugo wa Simba.
Nyingine za Kimataifa za Kirafiki zenye mcuto hii Leo ni ile ya Netherlands na Italy Mechi ambayo Waholanzi wanacheza kwa mara ya kwanza tangu juzi wamfukuze Kocha wao Danny Blind ambae ni Baba Mzazi wa Staa wa Man United Daley Blind ambae nae ni Mchezaji wa Kikosi hicho cha Netherland.
Pia Leo Wenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 Russia watakuwa Nchini kwao kujipima na Timu ngumu Belgium.
Huko Egypt, Wamisri watapambana na Togo wakati Mechi nyingine safi ni ile kati ya Republic of Ireland na Iceland.

NAPE MOSES NNAUYE – NI SHUJAA!

NAPE-SHUJAA

>>By StormingFo

Ndugu yangu Nape,

Wewe ni Shujaa wangu….

Ingawa hatujawahi kukukatana uso kwa uso.

Tumekutana humu Facebook…

Kipindi cha kuelekea Uchaguzi wa 2010 tukimtetea Jakaya Mrisho Kikwete..

Tulikesha tukitoa mada, kupambana kila tope Nchi yetu, CCM yetu ikipakazwa..

Wewe pamoja na Ndugu Mwigulu Nchemba!

Nakumbuka…

Nilikuasa…

Ili CCM idumishe Mapinduzi ni lazima ijikite kitaalam kwenye Mitandao..

Ukajibu Naam…

2015 tukaona Mapinduzi makubwa ya ‘Vita’ ya CCM Mitandaoni!

Hapo ushiriki wangu ukapungua Vitani…

Maana Wanataaluma walimwagwa!

++++++++++++++++++++

Wewe Shujaa..

Uimara wa Nchi yako..

Ni Ustahamilivu tu..

KUWA SHUJAA TU…

++++++++++++++++++++

Pole kwa msukosuko huu mkubwa..

Lakini Hongera kwa ustahamilivu wako..

Wewe ni Shujaa Tu..

Si kwa hilo wanalodai la Clouds…Wanalopakaza hao upande wa pili..

La Hasha..

Kwangu ni Shujaa..

Kwa kupokea habari za kuvunjwa moyo za kuondolewa Uwaziri..

Hukukurupuka…

Hukubabaika licha ya kusakamwa na hao Vijana..

ULINENA:

““Sina kinyongo na Serikali wala Chama changu. Sikumuuliza Rais siku aliniteua na sitamlaumu kwa kuamua kuniondoa.”

“Niliikuta CCM iko shimoni nikaitoa huko. Uzalendo wangu ndani ya CCM si wa kutiliwa shaka.

“Namshukuru Rais kwa Mwaka 1 alioniamini. Nampongeza kaka yangu Dokta Mwakyembe. Nawaomba mumuunge mkono Waziri Mwakyembe.”

“Nawaomba mtulie maisha yaendelee. Nape ni mdogo sana kuliko Nchi. Kuna mambo mazuri mbele hivyo tuiunge mkono Serikali.”

>>HAKIKA WEWE NI SHUJAA TU……WA CCM

NA TANZANIA YAKO!

Mola Atakubariki Daima

Aminia..

++++++++++++++++++++++++++++++

JUMAA MUBARAK Wanduguz!

*Kwa wenzangu wa Jumamosi na Jumapili, Sala njema tuombeane tu!

**Akina mie, tuselebuke aste aste, Mola yupo tu!

Aminia!

ILA KUMBUKA: Umoja ni Ushindi!

>>A Luta Continua….Wanduguz!!!

++++++++++++++++++++++++++++++

Habari MotoMotoZ