RIPOTI SPESHO

TOTAL U-17 AFCON GABON 2017: LEO NI KUNDI A, SERENGETI BOYS ALHAMISI NA ANGOLA!

TOTAL AFCON U17 GABON2017MICHUANO ya kugombea Ubingwa wa Afrika kwa Vijana chini ya Miaka 17, TOTAL U-17 AFCON GABON 2017, iliyoanza Jumapili Leo itaendelea huko Nchini Gabon kwa Mechi 2 za Kundi A zitakazochezwa Stade de POG, Mjini Port Gentil.
Hapo Majuzi, katika Mechi za Kundi hilo Wenyeji Gabon walinyukwa 5-1 na Guinea wakati Ghana ikiichapa Cameroun 4-0.
Hii Leo, Guinea itacheza na Cameroun na Ghana kuivaa Gabon.
Hapo Kesho Alhamisi zitapigwa Mechi za Kundi B ambalo katika Mechi zao za kwanza matokeo yalikuwa Sare kwa Timu zote.
Juzi, Tanzania, maarufu kama Serengeti Boys, walitoka Sare 0-0 na Mali ambao ndio Mabingwa Watetezi.
Mechi hizo 2 za Kundi B zitachezwa Stade de L’Amitle, Mjini Libreville kwa Serengeti Boys kuanza na Angola na kufuatia Mali kucheza na Niger.
Washindi Wawili wa kila Kundi watatinga Nusu Fainali na Timu hizo 4 zitakazocheza Nusu Fainali ndizo hizo hizo zitafuzu kucheza Fainali za FIFA za Kombe la Dunia kwa Vijana U-17 huko Nchini India Mwezi Oktoba.
TOTAL U-17 AFCON GABON 2017
Ratiba/Matokeo:
**Saa za Bongo
***KUNDI A Mechi kuchezwa Mjini Port Gentil KUNDI B Mjini Libreville
MAKUNDI:
Jumapili Mei 14
KUNDI A
Gabon 1 Guinea 5
Cameroun 0 Ghana 4
Jumatatu Mei 15
KUNDI B
Mali 0 Tanzania 0
Angola 2 Niger 2
Jumatano Mei 17
KUNDI A
1730 Guinea v Cameroun [Stade de POG, Port Gentil]
2030 Ghana v Gabon [Stade de POG, Port Gentil]
Alhamisi Mei 18
KUNDI B
1730 Tanzania v Angola [Stade de L’Amitle, Libreville]
2030 Niger v Mali [Stade de L’Amitle, Libreville]
Jumamosi Mei 20
KUNDI A
2030 Gabon v Cameroun [Stade de POG, Port Gentil]
2030 Guinea v Ghana [Stade de L’Amitle, Libreville]
Jumapili Mei 21
KUNDI B
2030 Mali v Angola [Stade de L’Amitle, Libreville]
2030 Tanzania v Niger [Stade de POG, Port Gentil]
NUSU FAINALI:
Jumatano Mei 24
Stade de POG, Port Gentil
1730 Mshindi Kundi A v Mshindi wa Pili Kundi B
Stade de L’Amitle, Libreville
2030 Mshindi Kundi B v Mshindi wa Pili Kundi A
Jumapili Mei 28
Stade de L’Amitle, Libreville
1730 KUGOMBEA MSHINDI WA 3
2030 FAINALI

TOTAL U-17 AFCON GABON 2017: SERENGETI BOYS NGOMA NGUMU NA MABINGWA WATETEZI MALI!

IMG 20170515 200528MICHUANO ya kugombea Ubingwa wa Afrika kwa Vijana chini ya Miaka 17, TOTAL U-17 AFCON GABON 2017, iliyoanza Jana kwa Mechi za Kundi A huko Nchini Gabon, Leo imeendelea kwa Mechi ya Kundi B kati ya Tanzania, maarufu kama Serengeti Boys, kutoka Sare 0-0 na Mali ambao ndio Mabingwa Watetezi.

Mechi hii ilichezwa Stade de L’Amitle, Mjini Libreville huko Gabon.

Hapo Jana, Wenyeji Gabon walianza vibaya kwa kutandikwa 5-1 na Guinea na kisha Ghana kuibonda Cameroun 4-1 zote zikiwa Mechi za Kundi A.

Baadae Leo, Mechi ya Pili ya Kundi A kati ya Angola v Niger itachezwa.

Mashindano haya yataendelea tena Jumatano kwa Mechi za Kundi A na Serengeti Boys kushuka tena dimbani Alhamisi kuivaa Angola ndani ya Stade de L’Amitle, Mjini Libreville huko Gabon.

Washindi Wawili wa kila Kundi watatinga Nusu Fainali na Timu hizo 4 zitakazocheza Nusu Fainali ndizo hizo hizo zitafuzu kucheza Fainali za FIFA za Kombe la Dunia kwa Vijana U-17 huko Nchini India Mwezi Oktoba.

TOTAL U-17 AFCON GABON 2017

Ratiba/Matokeo:

**Saa za Bongo

***KUNDI A Mechi kuchezwa Mjini Port Gentil KUNDI B Mjini Libreville

MAKUNDI:

Jumapili Mei 14

KUNDI A

Gabon 1 Guinea 5

Cameroun 0 Ghana 4

Jumatatu Mei 15

KUNDI B

Mali 0 Tanzania 0

Angola v Niger [Stade de L’Amitle, Libreville]

Jumatano Mei 17

KUNDI A

1730 Guinea v Cameroun [Stade de POG, Port Gentil]

2030 Ghana v Gabon [Stade de POG, Port Gentil]

Alhamisi Mei 18

KUNDI B

1730 Tanzania v Angola [Stade de L’Amitle, Libreville]

2030 Niger v Mali [Stade de L’Amitle, Libreville]

Jumamosi Mei 20

KUNDI A

2030 Gabon v Cameroun [Stade de POG, Port Gentil]

2030 Guinea v Ghana [Stade de L’Amitle, Libreville]

Jumapili Mei 21

KUNDI B

2030 Mali v Angola [Stade de L’Amitle, Libreville]

2030 Tanzania v Niger [Stade de POG, Port Gentil]

NUSU FAINALI:

Jumatano Mei 24

Stade de POG, Port Gentil

1730 Mshindi Kundi A v Mshindi wa Pili Kundi B

Stade de L’Amitle, Libreville

2030 Mshindi Kundi B v Mshindi wa Pili Kundi A

Jumapili Mei 28

Stade de L’Amitle, Libreville

1730 KUGOMBEA MSHINDI WA 3

2030 FAINALI

TFF YATAKA WANAHABARI KUACHA KAMPENI CHAFU, TENGA APATA WADHIFA CAF!

PRESS RELEASE NO. 295                                                              MEI 10, 2017

TFF YAVITAHADHARISHA VYOMBO VYA HABARI KUACHA KAMPENI CHAFU

TFF-TOKA-SIT-1Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limevitaka baadhi ya vyombo vya habari nchini kuacha mara moja kampeni za upotoshaji zenye lengo la kuwachafua viongozi wa juu wa shirikisho hilo.

TFF imeshtushwa na taarifa inayoendelea kutolewa kwenye gazeti moja la kila siku ikidai kuwa kuna ufisadi ndani ya shirikisho wakati madai hayo ni ya uongo na yenye lengo la kujenga mtazamo hasi dhidi ya shirikisho na viongozi wake.

Gazeti hilo la kila siku limetumia taarifa ya ukaguzi wa fedha iliyofanywa na wakaguzi kutoka TAC kujenga picha kuwa ni ushahidi tosha wa kuwepo kwa ufisadi ndani ya shirikisho.

Taarifa ya ukaguzi wa fedha ya TAC haikuwahi kuituhumu TFF kwa ufisadi. Taarifa ilibaini maeneo ya kiuhasibu ambayo yalihitaji maelezo ya ziada ya namna baadhi ya malipo yalivyofanyika (audit queries), na ufafanuzi ulitolewa kwa ufasaha na watendaji wa shirikisho na kupelekwa mbele ya Mkutano Mkuu wa Shirikisho.

Hata hivyo gazeti hilo ambalo limeonekana kuweka kando kabisa misingi ya uandishi wa habari, limechapisha taarifa bila hata kutoa nafasi kwa wanaotuhumiwa kujibu na kutoa ufafanuzi stahiki.

Rais na katibu mkuu wa shirikisho wanahudhuria mikutano ya CAF nje ya nchi wakati gazeti hilo likiendelea kuporomosha mlolongo wa tuhuma bila kutoa haki ya kusikilizwa kwa wanaoandikwa vibaya.

TFF inaliangalia suala hili kama kampeini chafu inayofanywa ili kushawishi matokeo ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi Agasti mwaka huu.

Pia taarifa hii potofu inalenga kulihamisha taifa kutoka kwenye masuala ya msingi kama kuiunga mkono Serengeti Boys kwenye mashindano ya Afrika na kuanza kujadili masuala yanayohusiana na siasa za uchaguzi wa TFF.

TFF kwa sasa inatafakari hatua za kisheria za kuchukua dhidi ya vyombo vya habari husika na inachukua nafasi hii kuvisihi vyombo vya habari kuacha mara moja kujihusisha na kampeni ya kuchafuana ambayo ni kinyume na misingi ya maadili ya uandishi wa habari.

HONGERA LEODEGAR TENGA - RAIS WA HESHIMA TFF

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linachukua nafasi ya kipekee kabisa kumpongeza Rais wa Heshima wa shirikisho, Leodegar Chilla Tenga kwa kuteuliwa kuwa Rais wa Kamati ya Usimamizi wa Leseni za Klabu katika Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

Kwa mujibu wa taarifa ya CAF, Tenga atasaidiwa Dany Jordaan wa Afrika Kusini katika kusimamia mpango huo muhimu kwa maendeleo ya mpira wa miguu barani Afrika.

Uteuzi wake ulitangazwa na Rais wa CAF, Ahmad Ahmad Jumatatu Mei 8, 2017 mara baada ya Kikao cha Kamati ya Utendaji CAF, chini uongozi mpya kilichofanyika katika Hoteli ya Sheraton, Manama, Bahrain.

Kwa niaba ya Kamati ya Utendaji, Rais wa TFF Jamal Malinzi alimpongeza Tenga akisema: “Hii ni fursa nzuri inayojenga taswira ya thamani na uwezo viongozi wetu wa mpira wa miguu nchini na kutambulika nje ya nchi katika taasisi za kimataifa kama CAF.

“Kwa niaba ya Kamati ya Wanafamilia wote wa mpira wa miguu, Wajumbe wa Kamati Utendaji, nachukua nafasi hii kumpongeza sana sana Rais wa Heshima wa TFF, Mzee wetu, Ndugu Leodegar Tenga kwa nafasi nyeti ya kusimamia Kamati ya Leseni za Klabu. Tunamtakia kila la kheri tukiamini nafasi hiyo ana uwezo nayo na bila shaka Mwenyezi Mungu, atakuwa pamoja na Tenga,” amesema Tenga.

Katika katika mkutano wa Bahrain, Rais wa CAF alipendekeza majina ya viongozi wawili kuwa Makamu wa rais, wa kwanza ni Kwesi Nyantakyi kutoka Ghana na wa pili ni Omari Selemani kutoka DR Congo na pendekezo hili lilipitishwa na kamati.

Uteuzi wa wajumbe wawili wa ushirikiano wa Kamati ya Utendaji. Kwa mujibu wa masharti ya sheria, Rais wa CAF alifanya mapendekezo ya wanachama mawili wa ushirikiano kwenye kamati ya utendaji ya CAF ambako wanachama waliopitishwa ni Moses Magogo (Rais wa shirikisho la mpira wa miguu Uganda na Ahmed Yahya – Rais wa Shirikisho la Mpira wa Maurtania.

Muundo wa Kamati ya dharura, Mwenyekiti ni Rais wa CAF, Ahmad Ahmad na wajumbe wake ni Kwesi Nyantakyi (Ghana), Omari Seleman (DR Congo), Fouzi Lekjaa (Morocco), Souleiman Waberi (Djibouti) na Musa Bility (Liberia).

Awali, Rais wa CAF alitoa mapendekezo ya uanzishwaji wa kamati mbili za dharula, kamati hizi zitajumuisha hasa marais wa mashirika wanachama. Moja itakuwa katika malipo ya marekebisho ya katiba na nyingine katika malipo ya fidia, semina zitaandaliwa kwa marais wa mashirika wanachama ili kuwasilisha kazi ya kamati ya marekebisho ya katiba na mchango wao kabla ya kukamilisha rasimu ya kuwasilishwa kwa Kamati ya utendaji na baraza kuu, muundo wa kamati ya dharura ni kama ifuatavyo.

Kamati ya Marekebisho ya Katiba Rais wake ni Kwesi Nyantakyi (Ghana) huku wanachama ni Lamine Kaba Badjo (Gambia), Sita Sangare (Burkina Faso), Moses Magogo (Uganda), Mclean Letshwiti (Botswana), Edouard Ngaissona (Jamhuri ya Afrika ya Kati), Elvis Chetty (Shelisheli) na Ahmed (Misri)

Rasilimali Watu: Ludovic Lomotsy (Mshauri wa Rais CAF).

Kamati ya fidia, Rais ni Fouzi Lekjaa (Morocco) huku wanachama wake ni Monteiro Domingos Fernandes (Sao Tome), Ahmed Yahya (Mauritania), Hani Abo Rida (Misri)

Rasilimali Watu: Essam Ahmed (CAF Kaimu Katibu Mkuu), Mohamed El Sherei (CAF Mkurugenzi Fedha)

Kongamano la mashindano ya CAF. Kamati hii inatarajiwa kupangwa nchini Morocco Julai 15-16, 2017. Shirikisho la soka nchini humo lina mpango wa kubeba gharama kuhusiana na kongamano hili, ambapo litaleta wadau pamoja mbalimbali ya mpira wa miguu Afrika (Wachezaji, Waamuzi, makocha, vyombo vya habari.

Kongamano hilo litajadili masuala yote kuhusiana na mashindano ya CAF ikiwa ni pamoja na shirika, muundo na ratiba na kufuatiwa na mkutano wa Kamati ya Utendaji ya CAF wa Julai 17, 2017 ambako utajadili pamoja na mambo mengine, utekelezaji wa maazimio makuu ya kongamano.

Uteuzi ya marais na makamu wa rais wa Kamati za Kudumu. Kamati ya Fedha, Rais ni Fouzi Lekjaa (Morocco) huku Makamu wa Rais ni Monteiro Domingos Fernandes (Sao Tome). Kamati nyingine ni ya maandalizi kwa ajili ya Kombe la Mataifa ya Afrika ambapo Rais ni Amaju Pinnick (Nigeria) na Makamu wa Rais ni Philip Chiyangwa (Zimbabwe)

Kamati ya maandalizi kwa ajili ya michuano ya Mataifa ya Afrika Rais ni Musa Bility (Liberia) huku makamu akiwa ni Wadie Jari (Tunisia). Kamati ya maandalizi kwa ajili ya Interclub Mashindano Rais ni Fouzi Lekjaa (Morocco) na Makamu ni Mutassim Jaafar (Sudan).

Kamati ya maandalizi kwa ajili ya U-20 Kombe la Mataifa Rais ni Tarek Bouchamaoui (Tunisia) na makamu ni Rui Da Costa (Angola). Kamati ya maandalizi kwa ajili ya mpira wa miguu wanawake Rais ni Isha Johansen (Sierra Leone) na makamu ni Moses Magogo (Uganda).

Kamati ya Maandalizi kwa ajili ya Mpira wa Ufukweni Rais ni Moses Magogo (Uganda) na Makamu Rais ni Kalusha Bwalya. Kamati ya waamuzi Rais ni Soleimani Waberi (Djibouti) na Makamu Rais ni Lim Kee Chong (Mauritius).

Kamati ya ufundi na maendeleo ya mpira wa miguu Rais ni Kalusha Bwalya (Zambia), makamu ni Souleiman Waberi (Djibouti) wakati Kamati ya Mambo ya Sheria, Rais ni Ahmed Yahya (Mauritania) na Makamu Rais ni Augustin Senghor (Senegal). Kamati ya mchezo wa uungwana (fair play), Rais ni Almamy Kabele Camara (Guinea) na Makamu Raisi ni Isha Johansen (Sierra Leone)

Kamati ya Habari Rais ni Amaju Pinnick (Nigeria) na Makamu Rais ni Hedi Hamel (Algeria). Kamati ya matibabu, Rais ni Adoum Djibrine (Chad) na Makamu Rais ni Yacine Zerguini (Algeria) na Kamati ya Masoko na TV Rais ni Danny Jordaan (Afrika Kusini) huku Makamu Rais ni Rui Da Costa (Angola).

………………………………………………………………………………

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA

PENATI MFUMO MPYA 'ABBA' WAJA!

PENATIUEFA ipo mbioni kufanya Majaribio  Mfumo mpya wa Upigaji wa Mikwaju Mitano Mitano wa Penati  ili kuondoa faida ya Timu inayoanza kupiga Penati hizo.
Utafiti uligundua Timu inayoanza kupiga Penati inayo Asilimia 60 ya nafasi ya kufuzu upigaji wa Penati hizo Tano Tano.
Mfumo huo Mpya, ambao unatambuliwa kama ABBA, utatumika kwa Timu ya Kwanza itayotambulika kama Timu A kupiga Penati ya Kwanza na kisha Timu B kupiga Penati ya Pili na ya Tatu na kisha Timu B kupiga Penati ya Nne halafu kuja zamu ya Timu A kupiga Penati ya 5 na ya 6 kwa kupokezana hivyo hivyo hadi kila moja inakamilisha Penati zake 5.
Mfumo huu umependekezwa na IFAB Chombo ambacho ndio pekee chenye Mamlaka ya kubadili Sheria za Soka.
Hivyo Mfumo wa sasa wa kupiga Penati moja moja kwa kila Timu kupokezana unaweza ukawa Historia ikiwa Majaribio ya Mfumo ABBA utafanikiwa.
UEFA imethibitisha ABBA itajaribiwa kwenye Mashindano ya EURO U-17 yaliyoanza Jana huko Croatia.
Kabla kupigwa kwa Penati kwa Mfumo wa ABBA Refa atarusha Shilingi Timu ipi itaanza kupiga na pia kupiga Kura kuamua Goli lipi la Uwanjani litatumika kupigiwa Penati hizo kama ilivyo sasa.
MFUMO ABBA:
-Penati ya Kwanza: 
Timu A kutangulia
Timu B kufuatia
-Penati ya Pili: 
Timu B kupiga mwanzo
Timu A kufuatia
-Penati ya 3:
Timu A kuanza
Timu B kufuatia
-Penati ya 4:
Timu B kuanza
Timu A kufuatia
-Penati ya 5:
Timu A kuanza
Timu B kufuatia
 
 

VPL JUMAMOSI ZIPO 5, YANGA-PRISONS, JUMAPILI SIMBA-LYON!

>FAINALI ASFC SIMBA-MBAO NI JAMHURI, DODOMA!

>SERENGETI BOYS YAHAMISHWA MJI FAINALI U-17 HUKO GABON!

PRESS RELEASE NO. 287                                                              MEI 02, 2017

FAINALI ZA AZAM SPORTS FEDERATION CUP

TFF-TOKA-SITMchezo wa Fainali za kuwania Kombe la Shirikisho la Azam (Azam Sports Federation Cup HD - ASFC), kati ya Simba SC ya Dar es Salaam na Mbao FC ya Mwanza, utafanyika Mei 28, mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Kwa mujibu wa Kanuni ya 5 ya michuano ya ASFC kuhusu Uwanja wa mashindano inasema: “Uwanja wa mashindano ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports HD utakuwa ni uwanja wenye hadhi inayokubalika na TFF.”

LIGI KUU YA VODACOM BARA KUENDELEA JUMAMOSI, JUMAPILI

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, inatarajiwa kuendelea Jumamosi Mei 6 na Jumapili Mei 7, mwaka huu  kwa jumla ya michezo sita.

Kwa mujjibu wa ratiba, michezo ya Jumamosi kutakuwa na michezo mitano ilihali Jumapili kutakuwa na mechi moja.

Michezo ya Jumamosi itakuwa ni kati ya Toto African na JKT Ruvu Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati Majimaji ya Songea itakuwa mwenyeji wa Mwadui kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma.

Kagera Sugar itaalikwa na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani wakati Young Africans ya Dar es Salaam itaialika Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Siku hiyo ya Jumamosi Mei 6, mwaka huu Azam FC itaialika Mbao FC ya Mwanza kwenye Uwanja wa Azam Complex ulioko Mbagala, Dar es Salaam ilihali Jumapili kutakuwa na mchezo kati ya Simba SC na African Lyon kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Wakati mechi zote zitaanza saa 10.00 jioni, mchezo kati ya Azam na Mbao utaanza saa 1.00 usiku.

SERENGETI BOYS YAPANGIWA LIBREVILLE

Timu ya Tanzania ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 maarufu kwa jina la Serengeti Boys, imebadilishiwa kituo kutoka Port Gentil na sasa imepangiwa Libreville.

Serengeti Boys imepangwa kundi B pamoja na timu za Niger, Angola na Mali ambako watafungua nayo mchezo Mei 15, mwaka huu. Kwa mabadiliko hayo, Kundi A lenye timu za Cameroon, Ghana, Guinea pamoja na wenyeji Gabon, litakuwa Port Gentil.

Kwa sasa Serengeti Boys wako Cameroon kwa kambi ya wiki moja iliyoanza Aprili 29, mwaka huu ambako tayari imecheza na wenyeji Cameroon mchezo mmoja na kushinda bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika jijini Yauonde.

Wenyeji hao, Cameroon watarudiana na Serengeti Boys katika mchezo mwingine wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika kesho Jumatano, Mei 3, mwaka huu.

…………………………………………………………………………….

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA