RIPOTI SPESHO

SportPesa SUPER CUP: GOR MABINGWA, WAWATANDIKA MAHASIMU AFC!

Matokeo:

Jumatatu Juni 5

Robo Fainali

AFC Leopards 1 Singida United 1 [Penati 5-4]

Yanga 0 Tusker FC 0 [Penati 4-2]

Jumanne Juni 6

Simba 0 Nakuru All Stars 0 [Penati 4-5]

Gor Mahia 2 Jang’ombe Boys 0

Alhamisi Juni 8

Nusu Fainali

AFC Leopards 0 Yanga 0 [Penati 4-2]

Gor Mahia 2 Nakuru All Stars 0

Jumapili Juni 11

Fainali

AFC Leopards 0 Gor Mahia 3

+++++++++++++++++++++++++++++++++

GOR-SPORTPESAGOR MAHIA ya Kenya Leo kwenye Uwanja wa uhuru Jijini Dar es Salaa, wameibuka Mabingwa wa SpoertPesa SUPER CUP, inayodhaminiwa na SportPesa Kampuni ya Kuchezesha Michezo ya Bahati Nasibu Mitandaoni, baada ya kuwacapa Mahasimu wao AFC Leopards, pia kutoka Kenya, Bao 3-0 kwenye Fainali.

Hadi Mapumziko, Fainali hii ilikuwa 0-0.

Kipindi cha Pili, Gor walipanda munkari na kupachika Bao zao kupitia Timothy Otieno, Oliver Maloba na John Ndirangu.

Kwa ushindi huo, Gor, mbali ya kubeba Kombe, pia wamenyakua Donge la Dola 30,000 na AFC kupata Dola 20,000.

Pia, sasa Gor imepata nafasi ya kupambana na Everton ya England hapo Julia 13 Jijini Dar es Salaam.

Habari MotoMotoZ