RIPOTI SPESHO

KLABU YA ENGLAND EVERTON KUCHEZA TANZANIA JULAI 13!

>KUMVAA BINGWA WA SportPesa SUPER CUP!

EVERTON-SPORTPESA2KLABU YA EPL, LIGI KUU ENGLAND, Everton itazuru Tanzania kucheza Mechi ya Kabla Msimu Mpya wa 2017/18 kuanza ikiwa ni moja ya matayarisho yao.EVERTON-SPORTPESA

Tripu hiyo itawafanya Everton watue Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kucheza Mechi 1 ya Kirafiki hapo Julai 13.

Mechi hiyo inatokana na mipango ya Kampuni kubwa ya Michezo ya Bahati Nasibu, SportPesa, ambayo imeingia ushirikiano na Everton hivi karibuni na pia kutua Tanzania kwa kishindo kwa kuzidhamini Klabu kadhaa kubwa zikiwemo Mabingwa Yanga, Simba na Singida United.

Ingawa Miaka ya nyuma Timu kadhaa za England zishawahi kuja kucheza Tanzania lakini Everton itakuwa Klabu ya Kwanza kabisa ya EPL kufanya hivyo.

Hapo Julai 13, Everton, chini ya Meneja Ronald Koeman, watacheza na Bingwa wa Mashindano Mapya ya SportPesa SUPER CUP ambayo yatashirikisha Klabu 4 za Kenya na 4 za Tanzania.

Everton waliingia Mkataba na SportPesa wa udhamini mapema Mwezi huu ambao pia utaifanya Everton kuvaa Jezi zenye Nembo ya SportPesa Kifuani.

SportPesa, Kampuni iliyoanzishwa Mwaka 2014, imeingia kwa kishindo kwenye Michezo hasusan Soka, ikitangaza Biashara yao ya Bahati Nasibu hasa zinazochezwa Mitandaoni.

SportPesa SUPER CUP 2017

RATIBA:

SPORTPESA-SUPERCUP 

Habari MotoMotoZ