RIPOTI SPESHO

JIULIZE TU: UNAIJUA YOUNG AFRICANS, MAARUFU YANGA?

YANGA-HQ-MANJIHivi unaijua Young Africans Sports Club, maarufu Mtaani kama Yanga?

Inadaiwa ilianzishwa Februari 11, Mwaka 1935 na kutwaa Ubingwa wa Nchi hii mara 21.

Timu hii Makao Makuu yake yalikuwa Mtaa wa Sukuma na Mafia Jijini Dar es Salaam walipopanga baadae wakanunua wenyewe Jengo Mafia na Nyamwezi na kisha wakaenda Kona ya Jangwani na Twiga, ila Jengo la Mafia na Nyamwezi bado lao.

Hivi unajua Klabuni hapo walipita Viongozi na Watu Maarufu na wa Kihistoria Nchi hii kina Kondo Kipwata, Tabu Mangara?

Hivi unajua Waasisi wa Muungano wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere na Mzee Abeid Karume, kwanini walitia Mguu wenyewe pale Jangwani na Twiga?

[HAWAKUKANYAGA MSIMBAZI HATA SIKU MOJA!]

Hivi unajua kwa nini Mzee Karume aliipa Yanga Milioni 2 na Nusu kujenga Jengo la Yanga pale Jangwani [Simba wakipewa Laki 2 tu]?

Hivi unajua Klabu hiyo kwanini inaitwa ni ya Wananchi?

USHAURI TU - NYIMBO RASMI ZA KLABU ZA YANGA NA SIMBA

 Feb 10, 2012 6:08am

 www.sokaintanzania.com

 ++Imewasilishwa na Storming Fo

Nimeusikia mjadala na mapendekezo ya Wadau wa Soka ambao kwa nia njema tu wanataka Klabu zetu kubwa Nchini Yanga na Simba ziwe na Nyimbo zao rasmi za Klabu zao na hili ni jambo jema tu.

 Haya ni maendeleo na yanapaswa kupewa sapoti ipasayo maana Soka la siku hizi si kabumbu uwanjani tu bali ni biashara na pia ni nguzo muhimu kwa jamii kwa kila nyanja tu.

 NAKUMBUKA, nikiwa mdogo enzi za Yanga na Sunderland [sasa ndio hii Simba], enzi ambazo hamna luninga, simu za mkononi wala hii intaneti, enzi za Miaka hiyo ya Naintini kweusi tulikuwa na Redio tu, nayo ilikuwa moja tu, Redio Tanzania tu, ushabiki huu ulikuwepo na Nyimbo za Klabu zilikuwepo.

Lakini, wakati huo, Nyimbo hizo hazikuwa za Klabu bali ni za Bendi maarufu za wakati huo ambazo zilikuwa na

mlengo wa Klabu waliyokuwa wakiependa na kuishabikia.

Wakati huo, ni siri ya wazi, Dar Jazz ilikuwa ni Sunderland na Western Jazz ni Yanga.

Washabiki wengi, na kwa kweli Nchi nzima, waliikuwa wakingojea Redio Tanzania itoe matokeo kwenye Kipindi cha Michezo usiku mara baada ya mechi kuchezwa.

Ulikuwa utamaduni, ushabiki na bashasha za Watangazaji enzi hizo kabla hata Nyimbo rasmi ya kuashiria Kipindi cha Michezo kuanza, kufyatua Nyimbo ya Bendi Shabiki ya Klabu na Watu wote bila kujua matokeo halisi walikuwa wakishangilia kwani wanajua wazi Timu yao imeshinda.

SIKU YANGA IKISHINDA ILIKUWA INAPIGWA NYIMBO YA WESTERN JAZZ:

Niko kati ya Bahari

Maji yamenizunguka

Sina moja la kufanya

Mola nisaidie…..

SIKU SIMBA WAKISHINDA NI NYIMBO YA DAR JAZZ:

Yamewafika wenzetu, mambo yanawashangaza

Wamebaki wanalia

Tutafanya jambo gani sasa….

+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++