RIPOTI SPESHO

WIKIENDI RATIBA VPL, LIGI 1, LIGI 2, BUNGE LACHANGIA SERENGETI, CHUNYA PONGEZI KWA UJENZI WA UWANJA!

RATIBA YA MECHI ZA WIKIENDI HII VPL, LIGI DARAJA I, LIGI DARAJA LA II

TFF-TOKA-SITLigi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), inatarajiwa kuendelea kesho Jumamosi Februari 11, 2017 kwa mechi nne kabla ya Jumapili Februari 12, mwaka huu kuendelea kwa michezo mitatu katika viwanja mbalimbali hapa nchini.

Stand United kesho Februari 11, 2017 inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga wakati Simba itaikaribisha Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam huku Ndanda ikiialika Toto Africans kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, kadhalika Ruvu shooting ikichea na Azam FC kwenye Uwanja wa Mabatini, Pwani.

Jumapili, Mwadui FC itacheza Mbeya City kwenye Uwanja wa Mwadui wakati African Lyon itacheza na Mtibwa Sugar Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam ilihali JKT Ruvu itakuwa mwenyeji wa Mbao FC kwneye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga. Kwa ufupi, ratiba ya kesho iko kama ifuatavyo:   

11.02.2017 - STAND UNITED VS MAJIMAJI

11.02.2017 - SIMBA VS TANZANIA PRISONS

11.02.2017 - NDANDA FC VS TOTO AFRICAN

11.02.2017 - RUVU SHOOTING VS AZAM FC

12.02.2017 - MWADUI VS MBEYA CITY

12.02.2017 - AFRICAN LYON VS MTIBWA SUGAR

12.02.2017 - JKT RUVU VS MBAO FC

Kwa upande wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL), Kundi A mechi zinatarajiwa kupigwa leo Februari 10, mwaka huu ambako Lipuli itaikaribisha Ashanti United kwenye Uwanja wa Samora mjini Iringa wakati Pamba itacheza na Mshikamano ilihali Friends rangers itacheza na Kilivya United wakati Polisi Dar itapambana na Africans Sports.

10.02.2017 - LIPULI VS ASHANTI

10.02.2017 - PAMBA VS MSHIKAMANO

10.02.2017 - FRIENDS RANGERS VS KILUVYA

10.02.2017 - POLISI DAR VS AFRICAN SPORTS

Kundi B

Kundi B kesho Jumamosi Februari 11, mwaka huu itacheza na Mlale JKT kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea wakati Njombe Mji itacheza na Coastal Union kwenye Uwanja wa Makambako mkoani Njombe.

11.02.2017 - MLALE JKT VS KURUGENZI FC

11.02.2017 - NJOMBE MJI VS COASTAL UNION

Kundi C

Kundi C kutakuwa na mechi nne ambako Mgambo Shooting itacheza na Polisi Dodoma wakati Polisi Mara itakuwa mwenyeji wa Mvuvumwa ya Kigoma wakati Rhono Rangers itakuwa mgeni wa Panone huko Kilimanjrao na Singida United itacheza na Alliance mjini Singida.

11.02.2017 - MGAMBO SHOOTING VS POLISI DODOMA

11.02.2017 - POLISI MARA VS MVUVUMWA

11.02.2017 - PANONE VS RHINO RANGERS

11.02.2017 - SINGIDA UNITED VS ALLIANCE SCHOOL

Ligi Daraja la Pili leo Februari 10, kutakuwa na mchezo mmoja wa Kundi A kati ya Mirambo ya Tabora na Bulyanhulu ya Shinyanga wakati Jumapili Februari 12, mwaka huu kutakuwa na mechi tatu ambazo ni za Kundi D.

Mechi nyingine ni kati ya Namungo na Mawenzi; Sabasaba na The Mighty Elephant wakati Mkamba Rangers itacheza na Mbalali United. 

10.02.2017 - MIRAMBO VS BULYANHULU

12.02.2017 - NAMUNGO VS MAWENZI

12.02.2017 - SABASABA VS THE MIGHTY ELEPHANT

12.02.2017 - MKAMBA RANGERS VS MBARALI UNITED

WABUNGE WAHAMASIKA KUCHANGIA SERENGETI BOYS

Wakati timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ya Tanzania maarufu kama Serengeti Boys ikirejea salama jijini Dar es Salaam jana jioni, Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, leo Februari 8, 2017 wamehamasika kuchagia timu hiyo.

Jana asubuhi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Job Ndugai alikuwa mstari wa mbele kutoa hamasa hiyo wakati wa matangazo mbalimbali mara baada ya kipindi cha maswali na majibu katika kikao cha bunge.

Wazo lilitoka kwa Mbunge wa Bunda, Mheshimiwa Esther Bulaya aliyetaka mwongozo wa Mheshimiwa Spika kwa timu ya Serengeti Boys kufanya vema katika michuano ya kufuzu kwa fainali za Vijana ambazo zitafanyika kuanzia Mei 21, mwaka huu huko Gabon.

Alisimama kutoa mwongozo huo huku akipendekeza kwa Wabunge wenzake wakubali kukatwa angalau posho ya siku moja kuchangia timu hiyo ambayo bajeti inaonesha kwamba maandalizi yake na kiushiriki michuano hiyo kunahitajika zaidi ya Sh bilioni moja.

Wabunge waliopewa nafasi ya kuchangia hoja hiyo walikubali kuchangia kwa sababu mfumo huo unafanywa pia na mataifa mengine na waliwatia shime vijana hao kwenda kupambana Gabon na kurejea nyumbani Tanzania na kikombe cha Afrika wakiwa ni mabingwa wa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17.

Awali, vijana hao kabla ya kuingia ukumbini walikutana na Bibi yao, Mheshimiwa Margaret Sitta - Mbunge wa Urambo na kuwazawadia fedha Sh 100,000 aliyeonesha furaha yake kwa vijana hao kufanya vema awali kabla ya kufuzu kucheza fainali kabla ya vijana hao kumshukuru Mama Sitta.

Baadaye, Mheshimiwa Mbunge Almas Maige aliwatuza Sh 500,000 na Mheshimiwa Bulaya akatoa Sh 300,000 hivyo kufanya jumla ya fedha hiyo kuwa Sh 900,000 ambazo Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kuamuru kupewa vijana hao.

Rais Malinzi aliyeongoza msafara huo bungeni, alitoa shukrani nyingi kwa Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Nape Nnauye kwa kuwaalika Serengeti Boys bungeni.

Alishukuru kwa jinsi wabunge walivyojitoa kuahidi kuchagia gharama za maandalizi na kushiriki kwa timu hiyo katika michuano hiyo mikubwa ya soka kwa vijana ambayo fainali zake zitachezwa Juni 4, mwaka huu.

TFF YAPONGEZA JUHUDI ZA UJENZI WA UWANJA CHUNYA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limepongeza juhudi zinazofanywa na Serikali ya Wilaya Chunya mkoani Mbeya na Halmashauri ya Mji huo kujenga uwanja bora wa mpira kwa miguu kwa wakazi wa wilaya hiyo.

Pongezi za TFF, zimetolewa jana Februari 9, 2017 na Rais wa TFF, Jamal Malinzi alipokutana na uongozi wa wilaya hiyo, aliokutana nao kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma ambako wote walialikwa na Bunge kwa mambo mbalimbali ya maendeleo.

Viongozi waliokutana na Rais Malinzi walikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Bibi Rehema Manase Madusa, Mkurugenzi wa Maendeleo wa Wilaya ya Chunya (DED), Bibi Sophia Kumbuli na Mwenyekiti wa Halmashauri, Bwana Bosco Mwanginde.

Katika mazungumzo yao, Rais Malinzi aliawaahidi viongozi hao kwamba Idara ya Ufundi ya TFF itakwenda Chunya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo kabla ya kuangalia eneo ambalo shirikisho linaweza kusaidia.

Aliwasifu viongozi hao kwa kuratibu ujenzi huo akisema: “Ninyi mmenza na kuanzisha kitu kizuri. Mkiurugenzi wa Ufundi, Bwana Salum Madadi atakuja huko kuangalia. Ila mmefanya jambo zuri sana kwa  maendeleo ya mpira wa miguu.”

IMETOLEWA NA TFF

Habari MotoMotoZ