RIPOTI SPESHO

AFCON 2017: CAMEROON YAING’OA GHANA, FAINALI NI WAO NA EGYPT!

CAM-GHANACAMEROON wameingia Fainali ya AFCON 2017, Kombe la Mataifa ya Afrika, baada kuifunga Ghana 2-0 Leo huko Nchini Gabon.

Mechi hii, Ghana walionekana wako juu kidogo lakini kukosa kwao umakini kwa nafasi chache walizopata ndio hasa kumesababisha wapigwe.

Frikiki ya Dakika ya 71 ilizaa Bao kwa Cameroon pale Difensi ya Ghana ilipojichanganya na kumruhusu Ngadeu kufunga.

Ndani ya Dakika za Nyongeza, kaunta ataki ya Cameroon ilizaa Bao lao la pili kwa Bassogog kuchanja mbuga na Mpira na kumchambua Kipa Brimah na kuipa Cameroon ushindi wa 2-0.

Sasa Cameroon watacheza Fainali na Egypt hapo Jumapili kupata Bingwa wa Afrika wakati Ghana wakicheza Jumamosi na Burkina Faso kusaka Mshindi wa Tatu.

VIKOSI:

CAMEROON: Ondoa, Oyongo, Fai, Ngadeu, Teikeu, Siani, Djoum, Zoua, Moukandjo, Bassogog, Tambe

GHANA: Brimah; Acheampong, Afful, Amartey, Boye; Wakaso, Acquah, Partey, Atsu, Andre Ayew, Jordan Ayew

REFA: B Gassama (Gambia)

AFCON 2017

Ratiba:

**Saa za Bongo

Robo Fainali

Jumamosi Januari 28

Burkina Faso 2 Tunisia 0 [RF 1]

Senegal 0 Cameroon 0 [Penati 4-5] [RF 2]

Jumapili Januari 29

Congo DR 1 Ghana 2 [RF 3]

Egypt 1 Morocco 0 [RF 4]

Nusu Fainali

Jumatano Februari 1

Burkina Faso 1 Egypt 1

Alhamisi Februari 2

Cameroon 2 Ghana 0

Mshindi wa 3

Jumamosi Februari 4

2200 Burkina Faso v Ghana

Fainali

Jumapili Februari 5

2200 Egypt v Cameroon

NCHI ZILIZOWAHI KUTWAA UBINGWA WA AFRIKA:

-Egypt-Mara 7
-Cameroon, Ghana-Mara 4
-Nigeria-Mara 3
-Congo DR-Mara 2
-Zambia, Algeria, Congo, Ethiopia, Ivory Coast, Morocco, South Africa, Sudan, Tunisia-Mara 1